Kanali mwime
Member
- May 5, 2018
- 71
- 171
Wakuu habari za huko mama land? Nimefika Joburg hapo jana tarehe 5 ilikuwa saa 8:15 Usiku kwa saa za huku.
Namshukuru Mungu nimefika salama japo nimechoka balaa sababu nimekaa kwenye bus siku 4. Pia nilipata vikwazo pale Lusaka nikiwa katika foleni ya kugongewa passport yangu. Palitokea vurugu ilisababisha nikarusha ngumi kwa jamaa mkongo aliyetaka kuniletea ukameme. Maofisa wakanizingua wakanirudisha nyuma nikaanza upya hivyo nilikaa masaa 3 kwenye foleni.
Nashukuru nimeona maajabu mengi sana. Nilikuwa sijawahi kusafiri nchi za watu lakini nimethubutu kufika hapa. Naamini nitafanikiwa kufanya kile kilichonileta. Nitafanya kazi kwa jasho langu sitajiunga na makundi ya kihalifu na nitakapoona mambo yanagoma nitaingia Botswana mpaka ifahamike.
Kwa Mtanzania aliyepo Joburg mwenye nia nzuri ya kuongea na mimi nimesajili namba ya simu ambayo ni +2725420374.
Asanteni sana wakuu mlionitia moyo pindi nikiwa safarini. Hapa Joburg nimefikia hoteli ya kawaida kesho naanza safari ya kutafuta kazi mtaa kwa mtaa mpaka ifahamike.
Kila la kheri wakuu.