Nimefika mwisho, madeni yamenichosha!

Nimefika mwisho, madeni yamenichosha!

Kila siku ni afadhali ya Jana. Sitamani hata kukuche, nimechoka mwili na roho, madeni yananimaliza, bora nipumzike nizikwe nayo.
Pole lakini tatizo halisolviwi kwa kulikimbia mkuu... Pambana kwa maana hata ukifa bado madeni yako yatakua pale pale.
 
Mimi nadaiwa million 13..


Ila nakatwa kila mwezi so hainihumi sana maana Toka nianze kufuga KUKU na enjoy sana nakupa ukweli wana faida asikudaganye mtu Mimi shuhuda
Mie madeni yangu yanaweza fika 40+ lakini sina hata wasiwasi na mie pia nadai jumla 68+
 
Marehemu ni tajiri, Mimi Sina kitu kwa Sasa...ila kwenye misiba pesa huwa zinapatikana.
Acha asili ifanye mambo yake kwa maana kufa Kila mtu atakufa, yachukulie maisha kama game tu, Kila kinachokutokea kwenye upande hasi na chanya jua ni kutokana na namna ulivyocheza hiyo game.

Kaa chini tuliza akili rudi tena mzigoni, acha kuwa muoga, wewe ni askari uliyeaminiwa na dunia ni uwanja wa vita so pambana.

Kama changamoto watu wote wanapitia kwahiyo usijione kama wewe ndio unaepitia hiyo changamoto, ni vile tu tuko hapa oujifariji ili kujisahaulisha shida zetu ila katu hatujawahi kukata tamaa hadi kuanza kufikiria kujiua, wewe ni askari so utashida hii vita👊🏾
 
Kaka madeni ni kitu cha kiroho. Usianze kukabiliana nayo kimwili utashindwa.

Kama Unaamini katika Mungu basi Kuwa mtu wa maombi.

Mungu atakupa hekima na atakufungulia milango ya kuweza kulipa madeni hayo.

Usikate tamaa Mungu anaweza kukutoa kwenye Madeni Ndugu.
 
Mwanaume akizaliwa tu anakuta madeni, ukikua unayakuta mengine, sasa unaanza kuchagua yanayolipwa na yasiyololipika,
uchune tu

Maraisi wote wa nchi hii wamekufa wanatuachia mideni isiyolipika na tumefurahi tu,

lipa kidogokidogo Kwa mapozi ili uonekane una nia
 
Kila siku ni afadhali ya Jana. Sitamani hata kukuche, nimechoka mwili na roho, madeni yananimaliza, bora nipumzike nizikwe nayo.
Mimi hapa ndio nashindwa kuelewa yani madeni yanamuuaje mtu? Si uhame unapoishi
 
Back
Top Bottom