Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 22,506
- 34,112
tatizo liko wapi hapo ?Baada ya kuhitimu form 4 nilielekea Mwanza kusaka life. Katika misele yangu nilimtongoza binti mmoja wa chuo cha sauti mwaka wa pili, akanielewa.
Tukaendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi mpaka alipomaliza na kuludi kwao KIGOMA mi nikabaki Mwanza. Kila nilipokuwa napata nafasi nilikuwa naenda kuonana nae. Mala kwa mala tulikutania guest moja pale mitaa ya Mwanga. Sasa mwezi ulioisha mwaka huu tulielekea kwao mimi na yeye.
Akawa amenitambulisha kwa mama yake kuwa mi ni mchumba wake. Mama yake akaniuliza unaitwa nani? Nikamwambia kila kitu kuhusu mimi na familia yangu kwa ujumla na sehem napoishi.
Nilipomwambia tu akaanza kulia huku akisema kuwa alizaa na baba yangu na mtoto ni yule mchumba wangu (jina nalihifadhi kwajili ya kutunza heshima) lakini alipo olewa tena kwa mwanaume mwingine baada ya kuachana na baba alimbadilishia jina mtoto wake na jina la ubini likanadilika akamuita jina la yule mme wake wa pili.
Nimeshindwa cha kufanya mpaka sasa nahisi kuchanganyikiwa kwani yule binti anaujauzito wangu, na mi na yeye tumechangia baba mmoja tofauti ni mama tu. Nifanyeje jamani???
Wenye makosa wazazi wenu. Isitoshe kitanda hakizai haramu