Ukitaka kujua tuna safari ndefu kufikia mafanikio jaribu angalia jinsi watu wanamjibu mleta Uzi hapa jukwaani, yani tumeshindwa kabisa kujua ni wakati gani tufanye midhaa Na wakati gani tuwe serious kidogo
Ndugu zangu kwa wale ambao wanamkejeli huyu jamaa eti poleni sana maisha ni safari Na kwenye hii safari kuna ups and down nyingi sana kama hujawahi pita kwenye hili huto kaa umuelewe huyu jamaa anapita kwenye kipindi Gani Sasa
Wito Na ombi langu tujaribu kuwa waungwana kwa maana kati yetu sisi hakuna aliye mkamilifu, tumsaidie kwa mawazo Na ndio maana amekuja hapa sababu anaamini JF ni tanuru la fikra.
Kuna wakati wa kupanda Na wakati wa kuvuna hivyo tujitahidi tofautisha nyakati