Nimechoka na kazi ya ualimu!

Nimechoka na kazi ya ualimu!

Wadau,nimechoka na hii kazi nataka niiache mara moja sababu naona hakuna future,kila siku ni matatizo tu hakuna kinachokaa mkao

Naombeni mwongozo mlowahi acha kazi.
Ni maamuzi mazuri,ila hakikisha kwamba your Plan B is better.Kama ni kazi nyingine umepata na ni nzuri zaidi,na kama unataka kufanya biashara ni biashara inayolipa,una mtaji na unaweza kuifanya kwa mafanikio,vinginevyo utalia.
 
Binafsi naona tatizo lako sio kazi ya ualimu,ualimu unauchukulia kama kisingizio,wana JF hebu fikiria mtu wa degree akianza ualimu baada ya miezi mitatu akiwa na salary slip zake 3 anakopesheka na NMB 15,400,000 CRDB ni 16,500,000 yaana gross salary mara 21 sasa hizo hela umefanyia nini mpaka ukate tamaa hivyo. wenzio wakipata milioni mbili tu wanatoka kimaisha, acha ualimu kajaribu mtaani baada ya mwaka ulete mrejesho
 
Hehhehehe......siku hizi watu wasiotumia akili zao vizuri wanazidi kuongezeka....
HV unawezaje kuwa na mawazo ya kuacha kazi wakati huna mwongozo na unategemea miongozo ya watu wengine juu ya maisha yako??
Jipange tena.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Kweli kuajiriwa nï utumwa, hasa kama kipato ni kïdogo na una malengo makubwa, kumbuka kujiajiri ni kitu kizuri lakinï kuna hitaji mipango, umejipanga?
 
Kwa hali iliyoko mtaani endelea tu na kazi baba... Wengine wanasota bado mtaani hawajapata hasa waliosoma ualimu... Acha kazi uone kazi kuipata kazi
 
Wadau,nimechoka na hii kazi nataka niiache mara moja sababu naona hakuna future,kila siku ni matatizo tu hakuna kinachokaa mkao

Naombeni mwongozo mlowahi acha kazi.
Kazi ipi unayoijua kuwa ni rahisi Duniani?
 
Hii ni aina ya maamuzi ya kukurupuka na kuiga iga unaachaje kazi bila ya wewe mwenyewe kujua unaenda kufanya nini mbadala unataka watu wengine wawaze kwa niaba yako
Hehhehehe......siku hizi watu wasiotumia akili zao vizuri wanazidi kuongezeka....
HV unawezaje kuwa na mawazo ya kuacha kazi wakati huna mwongozo na unategemea miongozo ya watu wengine juu ya maisha yako??
Jipange tena.
 
Kweli kuajiriwa nï utumwa, hasa kama kipato ni kïdogo na una malengo makubwa, kumbuka kujiajiri ni kitu kizuri lakinï kuna hitaji mipango, umejipanga?
Kuajiriwa ni utumwa hata kama kipato ni kikubwa
 
Back
Top Bottom