Nimechoka kumsubiri, nahitaji kuolewa

rubylove

Senior Member
Jun 1, 2015
127
41
Mimi ni binti wa miaka 26.Nina mchumba tuliwekeana ahadi tutaoana, ila naona mda unaeenda na yeye ukimuuliza hajajipanga kimaisha.

Nimechoma kumsubiri natafuta mume wa kunioa.
angalau awe na Miaka 27-37.

Sijaweka number kwa sababu maalumu, ukihitaji namba tutawasiliana, naishi Dar.
 
Last edited by a moderator:
Hitaji la kutaka kuolewa....linakufanya upoteze uwezo wako wa kufikiri na kuchanganua mambo......kufunga ndoa ni jambo la kwanza na kuhimiri mikikimikiki ya ndoa ni jambo la pili.........
Maamuzi ya ndoa ni moja kati ya maamuzi yanayohitaji umakini wa hali ya ju kwani ni maamuzi yanayopelekea kubadilisha mfumo mzima wa maisha yako.........

Ndoa ni mahali penye furaha.....ni muunganiko unaoleta faraja ndani ya mioyo ya wapendanao.....unatakiwa uishi na mtu anayeishi ndani yako......kwa sababu hakuna shule au chuo kinachofundisha namna ya kupenda........

KUPANGA NI KUCHAGUA.......
 
Yasije yakaja kuwa kama yale ya juzi mtu anatangaza nia, then afwatwa inbox halafu anakuja kuwatukana wanaume waliom PM kuwa ni mabazazi.
 
Huyo jamaa ndio mana hakuowi maana hujielewi ww ni Muislamu unataka kuolewa na Mkristo cha kufanya kwanza hapo badili dini halafu kwenye hilo dhehebu utapata huyo anaekufaa, dini hujabadili halafu unataka kuolewa na mkristo au unataka ndoa ya Bomani?
 
Huyo mchumba ako umeshaachana naye kwanza au bado unamshikilia hadi ukipata mwingine? Muombe sana Mungu afu usiwe na papara ya ndoa sana; japo unaonesha unaihitaji sana. Ukiwa desperate sana unaweza kujikuta unaishia kuumizwa tu na watakaotake advantage ya hitaji lako la ndoa . Sometimes Ni bora uchelewe kufika, ila ufike salama. Kila la kheri though
 
Akikujibu muulize na hili anamiaka 26 au 22
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom