Blackmamba
Member
- May 26, 2009
- 12
- 0
Title: Nimechanganykwa jamani msaada............. Is it about yourself?
Kama ni wewe mwenyewe pole sana dada yangu kaza moyo chunguza kama huyo mume anakupenda kiukwelii au la (kwangu mtu akupendaye akikukashifu kwa ajili ya kitu kidogo kama hiki cha wewe kumweleza udhaifu wako) hainiingii akilini.
Mwambie jinsi jibu lake lilivyokuathiri maana umesema hadi tendo la ndoa linakuwa gumu kwako. Ni heri akajua damage aliyoisababisha kwa majibu yake yasokuwa na utu. Kujifunza kitu kunategemea interest ya mtu na uwezo wake wa kuelewa sasa kama inakuwa ngumu kwa wewe kuelewa ni vema akalielewa hilo na kutafuta njia ya kukusaidia (ikiwa ni pamoja na kukufundisha yeye kwa upendo kwa sababu inaelekea yeye tayari ameshamaster lugha hiyo).
Sometime MJ1 unakuwaga kama shushushu,,,, anatuzuga ni mdada mmoja kumbe bwana ni yeye!lol alijuaje hata tendo la ndoa shida. Sema mume wangu kaniita norway natakiwa nijifunze kilugha cha huko na mimi ni mzito kwenye lugha tutakuelewa. Kona nyiingi! Kaza buti bibie jifunze lugha ufanye kazi. Jamaa anajutia faranga zake za ticket alizokutumia mkasaidiane kusaka maisha. Si bora kama angejua kilugha hakipandi angekutumia kamtaji ka mama ntilie uendelee kuka kibarazani!
Moods mmeniudhi sana...nilipoweka hii article kule mambo ya wakubwa nilikuwa namaana yangu. Maana mzee naye ni mpenzi mzuri huku ndani. ID yake naijua hajaomba kuingia kwenye chumba cha ma love maana ni mpenda siasa zaidi. So if possible can you muvuzisha this to mambo ya kikubwa please. Au nainze kucharanga ni norwigian!lol
Asanteni kwa michango yenu nilimpa dada ushauri mizuri mlionipa...ila katika mazungumzo alianza kuhisiwa eti anatembea na mwanafunzi mwenzake kisa tuu kamtambulisha kwa mr. wakiwa kwenye party alafu huyo dada akaondoka zake kurudi nyumbani na kumuacha mr. huko maana alishindwa kuvumili uchungu aliokuwa nao...mzee alimbadilikia nakuwa mkali kweli.Binafsi kulazimishana kujifunza lugha za kikoloni ni zaidi ya utumwa.
Huyo mume naye mshamba tu atamwambiaje laaziz wake maneno ya kashfa badala ya kumuinkareji!! Wanaume wengine bwana.........
Mama hiyo iwe changamoto ajifunze kwa bidii na amweleweshe huyo mume maana ya mke ni nini!! Kumleta ulaya isiwe chanzo cha kumnyanyasa ama!!
Nikweli dadangu/kakangu asante kwa hoja yakousiseme hivyo. Inafika pwent mtu unaboreka. Huyo mwanamke ni gunia la misumari. Hata ww mwanaume wako angekuboa
Za leo wandugu wapendwa,
Napenda kuuliza swali tafadhali, hivi mwanamme anaishi Norway,ameamua kuoa mwanamke toka mfano kwetu Tanzania na kumpeleka huko wakaanze maisha pamoja. Then huyo bibie akaanza kusoma hiyo lugha ili aweze kupata kazi...lugha imegoma akamueleza mumewe hali halisi ili kama nikutafuta kazi nchi nyingine iwe hivyo. Huyo baba baada ya kuelezewa hayo akawa mkali nakutoa maneno ya kejeli kwa huyo mwanamke eti kama haiwezi lugha kaenda huko Norway kufanya nini! Kwa kweli huyo dada roho ilimuuma karibia ajinyonge. Je tunaweza kumsaadia vipi huyu bibie katika swala hili maana yaelekea mume ameshamuona mzigo sasa, ambayo imempelekea hata tendo la ndoa kuwa gumu kwake. Asanteni.
Duniani kuna vituko mbona wahindi hawajifunzi kiswaili
Hizi threads nyingine noma sana, hii ya miaka minne na ushee iliyopita!!!