mps
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 406
- 588
ni mwaka wa tatu sasa tangu nilipokutana na huyu binti na kuwa nae ktk mahusiano lkn mda wote niliokuwa nae hakika sikuwahi kumwambia kuwa kuna siku tutaoana lkn kadri siku zilivyosonga mbele huyu binti amekuwa committed kwangu na hata imefika wakati ananiuliza maswali magumu kuhusu future yetu lkn siku zote sijataka kumkatisha tamaa ama kumuumiza kwa kile kinachoonekana kawekeza mawazo yake kwangu kiukweli anani care sana maana yy anafanya kazi nami bado nipo chuo lkn kitu ambacho kimenishinda ni kuchukua uamuzi kwa upande mwingine namhurumia kumuumiza na kusema nimuoe kiukweli sitakuwa nimeutendea moyo wangu haki maana pamoja na mazuri yote lkn sioni km ni mtu sahihi wa kua nae milele binafsi naona si chaguo langu.wakati mwingine nilikuwa mkoani(home) nikampigia simu kumjaribu nikamwambia bhana wazee wamenitafutia mchumba wa kuoa sijui itakuwaje aiseeee alituma sms ambazo machozi yalinitoka mwenyewe hivyo nimeshindwa kupata hitimisho la swala hili naombeni wenye uzoefu namiono tafauti mnishauri ili mwisho wa siku nichague ilipo hasara ndogo karibuni kwa mawazo