Nimeathirika kisaikolojia ushauri

May 28, 2023
55
63
Habarini,

Nilikuwa na mke tuliependana sana kwa muda wa miaka 9. Mwanamke alibadilika na kuondoka, alinichenga sana alipo mpaka sasa ni miezi 6 hataki kuwasiliana, nami ameamua kudanga.

Nataka nimtafute mchumba mpya nioe, je, nikitafuta wa jina kama la mke wangu itanipa shida? Mke wangu anaitwa Elizabeth, basi mimi hukumbuka sana mtakatifu Elizabeth. Alienda kumsalimu Bikira Maria kipindi yu mjamzito hadi kitoto kilichoko tumboni kikacheza, nami nilikuwa najisikia nimeoa mtu mwenye jina la utakatifu huo.

Je, nikiwa na wanangu na mke mpya sitakumbuka kumbuka mambo ya mke wangu Elizabeth?

Naombeni msaada kwa wazoefu waliopitia changamoto kama hii.
 
Ila we jamaa bana, Nani kakudanganya eti jina la mtu linaendana na tabia zake?
 
je nikitafuta wa jina kama la mkewngu itanipa shida? Kwani mkewngu anaitwa Elizabeth basi mm hukumbuka sana mtakatifu Elizabeth alienda kumsalimu bikira maria kipindi yu mjamzito hadi kitoto kilichoko tumboni kikacheza nami nilikuwa najisikia nimeoa mtu mwenye jina la utakatifu huo
Jina la mke halipaswi kuleta shida katika ndoa. Badala yake, zingatia utu wake, tabia na malengo yake.
=
Je nikiwa na wanangu na mke mpya sitakumbuka kumbuka mambo ya mkewangu Elizabeth?
Ni kawaida kukumbuka mambo ya zamani, lakini usiruhusu kumbukumbu zikuzuie kuwa na furaha na mke wako mpya. Zingatia kuwa unampenda na unamthamini.
 
Pole maana "Ulioa jina hukuona mwanamke "

Tafuta mwanamke uoe siyo jina, jina waachie wasoms nyota
 
Habarini,
Nilikuwa na mke tulipendana sana kwa muda wa miaka 9 mwanamke alibadilika na kuondokaalinichenga sana alipo mpak Sasa ni miezi 6 hataki kuwasiliana nami ameamua kudanga swali na ushauri nataka nimtafute mchumba mpya nioe je nikitafuta wa jina kama la mkewngu itanipa shida? Kwani mkewngu anaitwa Elizabeth basi mm hukumbuka sana mtakatifu Elizabeth alienda kumsalimu bikira maria kipindi yu mjamzito hadi kitoto kilichoko tumboni kikacheza nami nilikuwa najisikia nimeoa mtu mwenye jina la utakatifu huo
Je nikiwa na wanangu na mke mpya sitakumbuka kumbuka mambo ya mkewangu Elizabeth? Naombeni msaada kwa wazoefu waliopitia changamoto kama hii


Kweli wewe unaitaji msaada, nenda Mirembe. Ninaamini mke wako kaondoka sababu ya matatizo yako, ulichoandika sounds very weird, ningekuwa ndugu yako ninge shauri watoto walelewe na watu wengine.
 
Pole sana mkuu,

Ulizaa nae watoto?

Kama hukuzaa nae,msahau kabisa wala usiwasiliane nae,maisha ni mafupi sana,usiishi kwa kujitesa,
Jichanganye na watu,fanya mazoezi,fanya vitu uvipendavyo,mkumbuke Mungu wako,toa sadaka japo hata kidogo tu,

Utarudi tu sawa mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom