Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 414
- 877
Hii ni story ya kweli nilisimuliwa na jamaa yangu nami naileta kwenu kama funzo.
Ilikuwa mwaka 2004 ujenzi wa barabara ya Shinyanga-Mwanza umepamba moto chini ya Grinaker LTA nami nikiwa mmojawapo kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Kazi yangu ilikuwa ni kugawa mafuta kwenye magari na mashine. Kazi niliyoipenda sana kwani ilikuwa inaniingizia pesa ya kutosha. Kwa wastani kwa siku nilikuwa na uwezo wa kuingiza 200k (kuna siku inakuwa zaidi na siku inakuwa chini). Hela hiyo nikipata kwa siku 2 inazidi mshahara wangu wa mwezi mmoja.
Hela ya mafuta ilinizuzua nikapata kimada mwalimu pale kando ya mgodi wa Mwadui panaitwa Maganzo, nikamsahau mke wangu aliyekuwa na watoto wawili nikaacha hata kwenda nyumbani nikahamia kwa kimada. Marafiki walinishauri lakini sikusikia la mtu, kwa kweli nilimpenda sana huyu mwalimu.
Mke wangu alikuwa anaishi mgodini Mwadui ambako nami nilikuwa nikiishi na kufanya vibarua humo kabla sijapata kazi ya barabara. Sheria ya nyumba za mgodini kama hufanyi kazi za kuinufaisha kampuni basi hutakiwi kuishi kwenye nyumba hizo.
Mke wangu hakuwa na kazi alikuwa akikaa kwa jina langu nami nimepotea sionekani basi uongozi ukamwambia aachie nyumba ili wakae wafanyakazi wengine. Nilipata taarifa hizo lakini sikujali mapenzi ndiyo yaliongezeka kwa huyu mwalimu.
Ni kweli aliondoka na sikutaka kujua ameenda wapi na ataishi vipi sikujali, mwalimu alijua kunilea mpaka nikasahau kila kitu kuhusu familia yangu na mke wangu tuliyefunga nae ndoa. Ilikuwa nikirudi jioni namuwekea hela zote mezani kesho yake naondoka na pesa kidogo tu kula kabla sijapata mlungula wa siku.
Sikutaka kujua pesa zinatumije niliamini huyo ndie mke wangu mpya tutakayeishi nae siku zote za maisha yetu. Kumbe mwalimu alinunua kiwanja na kujenga nyumba mimi nikiwa sijui. Haikuwa nyumba kali sana lakini ni nyumba ambayo ni standard mtu kuishi wa kipato cha kawaida.
Siku moja naambiwa nimejenga nyumba mme wangu wiki ijayo tutahamia, kwa kweli nilifurahi japo sikujua amejenga vipi. Siku ikafika tukahamia kwenye nyumba yetu maisha yakaanza. Muda ukaenda, miaka ikaenda kazi ya barabara ikaisha, nikapokea mafao yangu yote na NSSF nikamkabidhi mwalimu nikiamini ni mke wangu hela zangu ni zake pia.
Ilipita miezi miwili siendi kazini nashinda tu nyumbani kazi imeisha wa wakandarasi wameondoka, mwalimu akaniambia nitafute kazi nyingine sio vizuri kushinda nyumbani. Nikaanza kutafuta lakini sikupata sikuwa na cheti chochote cha taaluma hata hiyo ya mafuta sijui walitumia kigezo gani kunipa kwa sababu niliishia darasa la saba.
Ilifikia kipindi pesa ikakata, nilikuwa sijazoea kuombwa pesa na mwalimu ndiye alikuwa mmiliki wa pesa zangu hivyo alikuwa anajiamulia mwenyewe nini cha kufanya. Nikaanza kuombwa pesa mara unga na mchele umeisha, mara naomba pesa nikalipe mchezo, yaani vitu vingi sana. Nilimweleza hali halisi kuwa sina pesa kwa sasa asubiri nipate kazi nyingine.
Ilipita miezi 7 tangu kazi iishe na nyumbani nikaona kabisa mambo yamebadilika tukaanza kula dagaa mara nyingi kitu ambacho sikukizoea. Tuliendelea hivyo hivyo kigumu akiwa na tegemeo kuna siku nitapata kazi lakini mambo hayakuwa hivyo kwani sikupata kazi yoyote.
Baada ya miezi takribani 9 akaniambia nimtafute mke wangu kwani kuna watoto wananitegemea, nilimwambia aachane na stori za mke wangu mimi nipo nae na ninampenda yeye. Akaniuliza yeye ni nani kwangu mpaka nimpende? Nikamwambia ni mke wangu,. Lahaulaaa ni kama nimemtukana akaniambia nimkome akaniuliza tumefunga ndoa wapi nikabaki nashangaa. Akaniambia ana mchumba wake natakiwa kuondoka pale na wanategemea kufunga ndoa.
Kwa kweli niliumia sana.
Nilichoamua kufanya ............
Itaendelea