Nimeanza kujifunza uchawi!!!

Nimeanza kujifunza uchawi!!!

Ningependa utujuze ile topic ya - chuma ulete, hasa hasa mbinu zao na jinsi ya kujikinga na '' wachuma ulete''

Chuma ulete ni uchawi wa kitoto sana lakini umewaangamiza na una waangamiza watu wengi sana..Nikipata muda wa kutosha nitafunguka zaidi hapo baadaye!
 
shindwa pepo kwa jina la YESU kristo wa nazareth!

Mkuu wa mapepo, Lucifer alimchukua Yesu akaenda naye mlimani na kumjaribu kwa muda wa siku arobaini. Mkuu wa mapepo aliwahi kuishi mbinguni na Mungu, anamfahamu Mungu kuliko unavyo mfahamu wewe, alifanikiwa kuwashawishi theluthi ya malaika wa mbinguni wakamuasi Mungu, ana uwezo wa kuvuruga mipango ya Mungu, anaongea na Mungu katika namna ya kirafiki zaidi. Unadhani wewe ni bora sana kuliko huyo mkuu wa mapepo?
 
Merlin wa bongo "magic can be used for good"
Good idea fanya mapinduzi ya kielimu.......elimu hii ya mzungu kwa waafrika haifai, lete elimu yetu bwana.
 
Unasema "utawaloga wachawi wenzio tu " halafu hapo hapo unasema uchawi hauamini kabisa, which is which and which is not which? How can you contradict yourself in less than 5 minutes? Anyway kinacho determine mtu kulogwa au kutokulogwa is not whether u believe in witchcraft or not ? Kama ulikuwa unadhani ukiamini au kufikiri kuwa uchawi hauwezi kuwa na nguvu kwako ndio kinga ya uchawi, utakuwa unajidanganya sana!

Kinga yake ni nini kaka Mchawi? Ukisikia jina la Yesu katikati ya Uchawi athari zake ni nini? Ni mtu wa aina gani ambaye harogeki na ni yupi anayerogeka kirahisi? All the worst kaka mchawi
 
Baada ya jitiada za muda mrefu kidogo hatimaye nimefanikiwa kumpata mwalimu wa uchawi. Nimeanza kusoma wiki mbili zilizo pita. Lengo langu ni kuzijua vyema siri za adui shetani ili niweze kuwasaidia watanzania wenzangu, kujua njia mbalimbali za kukabiliana naye....Sun Tsu said"know thy enemy as you know yourself and in a thousand battles you willnever be in jeopardy." Kwa hizi wiki mbili za kujifunza uchawi, nimegundua kuna uchafu mwingi sana kwenye uchawi..

Yote ili????
 
Back
Top Bottom