Nimeamua kuwa Atheist

Nimeamua kuwa Atheist

loose Nut

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
769
Reaction score
1,729
Nimefanya tafiti yakinifu nimekuja kugundua Mungu hayupo. Ni story tu za kutupa matumaini hewa.

Nimeamua kuwa Atheist. Nitaupa muda nao ukizingua namrudia Yesu.

Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Ni maamuz yangu binafsi.
 
Thibitisha kwa nini Mungu hayupo? Cc. Kiranga
Kwanza kabisa, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Narudia tena, kisichopo, hakithibitishiki kuwa hakipo.

Kwa sanabu hakipo, na kama hakipo, hakithibitishiki kuwa hakipo, uthibitisho unaendana na kilichopo.

Tunaweza kujenga hoja kama za proof by contradiction kuonesha contradiction zinazoonesha kitu fulani hakiwezi kuwapo. Katika hii dhana ya Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) hayupo, nimeelezea sana Epicurean Paradox mpaka michoro nimeiweka hapa. Google Epicurean Paradox, soma, ielewe, kama una swali kuhusiana an Epicurean Paradox lilete hapa.

Zaidi.

Mzigo wa uthibitisho unamuangukia yule anayesema kitu kipo.

Ndiyo maana Polisi wakija nyumbani kwako, wakisema una madawa ya kulevya, wao wanaosema una madawa ya kulevya wanatakiwa wafanye msako mpaka wayapate, wathibitishe yapo.

Hawakwambii wewe unayesema huna madawa ya kulevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.

In principle, we cannot prove a negative, but we can show contradictions that shows the impossibility of a negative.

Swali la kuuliza hapa, ni kuwauliza wanaosema Mungu yupo, wathibitishe Mungu yupo.

Unasema Mungu yupo?

Kama unasema hivyo, thibitisha Mungu yupo.
 
"Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.

Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea."

Waroma.2.14-16.BHN
 
Nimefanya tafiti yakinifu nimekuja kugundua Mungu hayupo. Ni story tu za kutupa matumaini hewa.

Nimeamua kuwa Atheist. Nitaupa muda nao ukizingua namrudia Yesu.

Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Ni maamuz yangu binafsi.
Welcome to the real world.
 
Back
Top Bottom