Hivi nikisema najitolea kwenda kuishi kijijini kwa makubaliano kwamba nitakuwa MTIIFU kufanya kazi zote za usimamizi wa shamba kuanzia kuandaa shamba mpaka kuvuna kwa makubaliano ya mimi kutumia nguvu,busara na hekima niliyopewa na Mungu na mtu mwingine ajitolee fedha ili kufanikisha hilo zoezi naweza kupata mtu wa kupiga naye kazi?
Makubaliano yanafanyika baada ya kila mmoja kiridhika na mwingine kwa kufahamu nyumbani na wazazi wa mwenziwe kama wapo, kisha sheria na taratibu nyingine kufuatwa.
Hili swala linawezekana?
ila siyo kilimo cha hekari kumi au ishirini(isiwe chini ya hekari 50), hapa nazungumzia shamba la ukweli maana hiyo ndiyo itakuwa ajira yangu.
Yaana kifupi naachana kabisa na mambao ya mwisho wa mwezi.
Huyo mtu yupo?
Mimi naweza ila hela yangu ndogo