Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Mkuu Malila wala sijakusahau.

Nina kazi kuubwaa saaaana ya kuvuna, yaani mpaka nachnaganyikiwa. Inatia moyo mpaka basi. Wazee changamkieni dili. Mawazo nimeyatoa humu humu.

Elnino kaza buti mazee. You will never regret. Trust me

Ogal, its true i'm serious - unajua sisi tuliolima those days kwa shida tena jembe la mkono toka saa 12 alfajiri mpaka 12 jioni becomes simple, we just change tactics and its done, this time by using salary as Capital.

So far Wakuu nishamaliza kupanda heka zote, nimepalilia na sasa naomba mungu tu ashushe mvua kwa neema then we talk more on June wakati wa mavuno.

Sasa hivi najaribu kulima heka kama mbili hivi za maharage ya soya as a testing phase for tne next season - cheers!!
 
Hongera sana Mkuu..............
 
Ni-pm nikutajie,utacheka hadi uvunjike mbavu. Mkuu kilimo ni lazima tukifanye kama professionals wa kilimo hasa.
Nasikitika sana nilikutumia msg ila sijui kilitokea nini hapo katikati. Nilipoona kimya (hunijibu) nikaamua kupitia sent msgs na kugundua msg yako haipo.

Samahani sana mkuu ila nakutumia sasa hivi.
 
Nasikitika sana nilikutumia msg ila sijui kilitokea nini hapo katikati. Nilipoona kimya(hunijibu) nikaamua kupitia sent msgs na kugundua msg yako haipo.
Samahani sana mkuu ila nakutumia sasa hivi.
Poa mimi naisubiri hiyo msg.
 
Kila nikisoma thread hii nakumbuka jinsi nikivyosomeshwa na fedha ya kahawa, na sasa kahawa haipo kama zamani na umaskini umeshika kasi. Ila nimegundua ukiweka bidii na utaalamu kilimo kinaweza kulipa.

Nawashukuru wote wanaotoa mchango. Leo nimecheka na kufurahi sana baada ya kukutana na mabrazameni wa dar wakienda kutembelea mashamba yao huko bagamoyo vijijini.nimefurahi kwa sababu naona watu wameamua kuwekeza kwenye kilimo.

Ngoja niungane na elnino, malila etc kuhimiza wengine kujikita kilimoni.

Ila naona itabidi tujikite kilimo cha kisasa badala ya kutegemea mvua. Aidha ni vema unapoanza kuwekeza kwenye kilimo ukafikiria jinsi ya kupata masoko.

Mimi sasa hivi nimeanza kufikiria kilimo cha VITUNGUU MAJI, VITUNGUU SAUMU na passion fruits. wapi kilimo hiki kinafanyika?
 
Kila nikisoma thread hii nakumbuka jinsi nikivyosomeshwa na fedha ya kahawa, na sasa kahawa haipo kama zamani na umaskini umeshika kasi. Ila nimegundua ukiweka bidii na utaalamu kilimo kinaweza kulipa
Nawashukuru wote wanaotoa mchango.

Leo nimecheka na kufurahi sana baada ya kukutana na mabrazameni wa dar wakienda kutembelea mashamba yao huko bagamoyo vijijini.nimefurahi kwa sababu naona watu wameamua kuwekeza kwenye kilimo.

Ngoja niungane na elnino, malila etc kuhimiza wengine kujikita kilimoni.

Ila naona itabidi tujikite kilimo cha kisasa badala ya kutegemea mvua. Aidha ni vema unapoanza kuwekeza kwenye kilimo ukafikiria jinsi ya kupata masoko.

Mimi sasa hivi nimeanza kufikiria kilimo cha VITUNGUU MAJI, VITUNGUU SAUMU na passion fruits. wapi kilimo hiki kinafanyika?

Kilimo cha vitunguu maji nenda Ruaha Mbuyuni-kilolo,au bonde la Kibakwe Mpwawa,au Kipatimu. Huko kitunguu kinakubali na maeneo bado yapo kiasi. Passion fruits ni po pote pale,ila ukiweza katafute zile mbegu za passion pale Iringa sokoni,zile passion ukipanda zinaishi miaka mingi sana na zinazaa sana. Zina rangi kama blue kwa mbali hivi.

Wenyewe wanasema walileta wajerumani zamani sana.
 
Elnino, Malila na wengine,

Nina washikaji hapa Poland wanatafuta zao la Vitunguu Swaumu. Ila hapa kuna masharti kidogo kwani itakuwa import ndani ya European Union. Kwa hiyo wao wanatafuta vitunguu swaumu vyeupe na vyekundu na viwe na Diamter (kipenyo??) cha 55mm-65mm. Kama kuna mtu atakuwa tayari kulima basi mara akizalisha basi tuwasiliane na watakuja na kununua kiasi chochote atakachokuwa amezalisha (ila kumbuka masharti hapo juu). Wako tayari kununua hata makonteina 20 kwa mwezi. Hivyo wakulima kazi kwenu kwa watakao kuwa tayari kuzalisha kiasi cha walau Konteina moja.

Kwa wakulima wa mazao mengine, kama unazalisha zao fulani kwa wingi, basi tuwasiliane ili kuangalia kama jamaa watakuwa tayari kulitafutia soko na baadaye kuja kununua na kuuza. Hii inaweza kuwa mboga, matunda, viungo nk.
Jamaa wanasema kwa yeyote atakayekuwa anauza, basi watanunua hapohapo (pesa zote kupitia bank, hawataki kutembea na cash). Ila tuwasiliane mapema ili kwa zao unalotaka kuuza, wapate sample kama kilo tatu kwa kila zao. Wataenda nalo ili kupima (urasimu wa EU) na kibali kikitoka basi jamaa watakuja na kuanza kununua. Kama ni zao ambalo lilishapata tayari kibali EU, basi itakuwa ni rahisi zaidi.

Vitunguu Swaumu changamkieni wakulima, soko zuri lipo. Tuwasiliane kwa PM au sambali@afryka.org.
 
Ahsante sambali kwa taarifa nzuri.Mbogamboga je wananunua? mimi nalima mchicha kwa wingi ila soko ndio tatizo.
 
Wakuu mmeniencourage sana sana. Na mimi nipo mbioni kuanza, nitaleta matokeo ya maendeleo ili kuwatia moyo na wengine.
 
Kila mdanganyika akiwa na ari hii ya kilimo kwanza kweli tutaupiga umaskini teke! Naona na masoko ya nje pia yanapatikana hapahapa JF, sasa naanza kutafuta shamba rasmi ikiwezekana mashamba na mwakani nami naanza kuvuna nitapata ushauri wa kilimo bora toka kwa Elnino, masoko huko poland yani naamini oneday nami nakua kamilionea na sio wa kifisadi ati!
 
Elnino, Malila na wengine,

Nina washikaji hapa Poland wanatafuta zao la Vitunguu Swaumu. Ila hapa kuna masharti kidogo kwani itakuwa import ndani ya European Union. Kwa hiyo wao wanatafuta vitunguu swaumu vyeupe na vyekundu na viwe na Diamter (kipenyo??) cha 55mm-65mm. Kama kuna mtu atakuwa tayari kulima basi mara akizalisha basi tuwasiliane na watakuja na kununua kiasi chochote atakachokuwa amezalisha (ila kumbuka masharti hapo juu). Wako tayari kununua hata makonteina 20 kwa mwezi. Hivyo wakulima kazi kwenu kwa watakao kuwa tayari kuzalisha kiasi cha walau Konteina moja.

Kwa wakulima wa mazao mengine, kama unazalisha zao fulani kwa wingi, basi tuwasiliane ili kuangalia kama jamaa watakuwa tayari kulitafutia soko na baadaye kuja kununua na kuuza. Hii inaweza kuwa mboga, matunda, viungo nk.
Jamaa wanasema kwa yeyote atakayekuwa anauza, basi watanunua hapohapo (pesa zote kupitia bank, hawataki kutembea na cash). Ila tuwasiliane mapema ili kwa zao unalotaka kuuza, wapate sample kama kilo tatu kwa kila zao. Wataenda nalo ili kupima (urasimu wa EU) na kibali kikitoka basi jamaa watakuja na kuanza kununua. Kama ni zao ambalo lilishapata tayari kibali EU, basi itakuwa ni rahisi zaidi.

Vitunguu Swaumu changamkieni wakulima, soko zuri lipo. Tuwasiliane kwa PM au sambali@afryka.org.
Safi sana,ila ssambali, watu kumi tukikutumia kila 3 hizo ni kila 30,hapo si umepata kamtaji tosha kakuanza biashara ktk ebay ;) natania tu ingekuwa bora utoe more data,ya aina ya vitunguu swaumu wanavyotaka,au weka linki tuone sample then tuanze kilimo cha kufa na kupona for vitunguu export,je unaweza kutuambia wateja wanavitumia ktk kitu gani?

Hii itasaidia ktk kufanya biz projections na kutathmini bei.
 
Safi sana,ila ssambali, watu kumi tukikutumia kila 3 hizo ni kila 30,hapo si umepata kamtaji tosha kakuanza biashara ktk ebay ;) natania tu. Ingekuwa bora utoe more data,ya aina ya vitunguu swaumu wanavyotaka,au weka linki tuone sample then tuanze kilimo cha kufa na kupona for vitunguu export,je unaweza kutuambia wateja wanavitumia ktk kitu gani? Hii itasaidia ktk kufanya biz projections na kutathmini bei.

Sammbali hebu jaribu kutoa ufafanuzi wa maswali uliyoulizwa hapo juu. Elnino upo unaendeleaje na kilimo hapo turiani?
 
Wakuu,

Nimepokea PM nyingi wadau wanauliza maendeleo ya project yangu. Nilitegemea kwenda last weekend ili nije kuwapatie full updates pamoja na picha, lakini nvua zinanyesha sana kiasi njia hazipitiki kirahisi.

But so far so good tumeshamaliza kupalilia yamestawi vizuri - range urefu yapo kwenye kiuno cha mtu mzima. ndiyo tunaomba mwenyezi mungu andondoshe mvua tu hizi za masika ili at the end of the season tuone tumesimama wapi.
 
Ahsante sambali kwa taarifa nzuri.Mbogamboga je wananunua? mimi nalima mchicha kwa wingi ila soko ndio tatizo.

Mkuu Dafia,

Kuhusu mboga hizo ntaomba usubri kwanza hadi waje Tanzania. Kuna mpango wakija Tanzania basi waamue wenyewe na kuongea na jamaa wa mashirika ya ndege maana huwezi kusafirisha mchicha kwa Meli. Pia kibaya ni kuwa Poland hakuna Waswahili wengi wala mchicha. Na hawa unaweza kukuta hata Mchicha hawaufahamu maana wao ukiwaambia Spinachi basi wanafikiri hizi Kabeji za Kichina.

Ila kwa vitunguu swaumu ni biashara ambayo tayari wanaifanya na wana masoko yao tayari wanauza. Nikishakubaliana nao kufahamu lini watakuja (kama watakuja) basi ntakujulisha mapema ili tuje tuonane na wao waanze kuutafutia soko nchi kama uholanzi au UK ambako kuna waswahili wengi sana.
 
Kanyigio,
Mkuu wangu nilikuwa nimeandika hapo. Wao wanataka viwe vyekundu au vyeupe na Diameter yake iwe na 55mm-65mm.
Labda tu cha zaidi ni kuwa mwangalifu na mbolea unazoweka maana huweza kuharibu kabisa ubora wake (wataalamu wa kilimo saidieni). Mengine sidhani kama yapo ambayo utataka zaidi nikuwekee maelezo. Kama rangi huelewi basi nakuwekea hapa chini picha ya vitunguu swaumu wanavyosema Vyekundu na vile vyeupe.
Pia angalia ukurasa huu utaona VYEKUNDU (ukweli viko kama Violet colour) na VYEUPE vinavyopishana.
2 Sisters Garlic

Sammbali hebu jaribu kutoa ufafanuzi wa maswali uliyoulizwa hapo juu.
Elnino upo unaendeleaje na kilimo hapo turiani?

Majibu nimekuwekea juu. Kama ni wingi wa vitunguu vya kutuma hali iko hivi: Kama mtakuwa wengi na tukawasiliana basi kwa Tanzania nzima zinahitajika hizo kilo tatu. Labda kuwe na tofauti sana kati ya vitunguu swaumu vya sehemu moja na nyingine. Wakishatolea kibali kimoja basi itatosha. Nikipata hizo kilo tatu basi ntaandika hapa ili wengine wafahamu kuwa kibali kikitoka basi inabaki kuuza tu bila kuleta sample. Ila ntataka sana Wakulima moja kwa moja kwani hawa jamaa wa EU huwa wanakwenda kuangalia hivyo vitunguu vimetoka wapi. Ukisema Tanzania Ruaha au sijui Manyara, jamaa wanatia timu kuangalia kama kweli kuna mashamba pale.

safi sana,ila ssambali, watu kumi tukikutumia kila 3 hizo ni kila 30, hapo si umepata kamtaji tosha kakuanza biashara ktk ebay ;) natania tu ingekuwa bora utoe more data, ya aina ya vitunguu swaumu wanavyotaka,au weka linki tuone sample then tuanze kilimo cha kufa na kupona for vitunguu export. Je, unaweza kutuambia wateja wanavitumia ktk kitu gani? Hii itasaidia ktk kufanya biz projections na kutathmini bei.

Chesnok-Red-Garlic-blog2.JPG
zupa+mlody+czosnek3.jpg
red%20garlic.jpg
 
Back
Top Bottom