Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by ELNIN0, Mar 18, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  JF

  Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

  Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

  Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

  Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

  Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

  Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

  Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

  By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

  This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

  Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
   
 2. B

  Bobby JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,798
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  Hongera sana EL kwa uamuzi wa busara. Ila nadhani hapo kwenye bold kwangu mm ni pazuri mno kuwa kweli (too good to be true) please please naomba upadefend.
   
 3. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,197
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wazo zuri mkuu, big up! KILIMO KWANZA!

  Kijijin kwetu mababu wametuachia mashamba na sasa yamekua misitu. Ngoja nasi tuvute pumzi km vipi tujitose.
   
 4. C

  Cotan Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Elinino.Hongera sana kwa uamuzi huo mzee.kweli kilimo kinalipa ila kinataka uangalizi wa karibu sana.Lakini kwako naimani utafanikiwa kwa sababu huenda umejipanga vema toka muda mrefu.Basi kila la heri mzee.Unajua wa Tanzania wengi tunashindwa kunufanika na kilimo kwa sababu ya kutumia nyenzo duni pia ukosefu wa Utaalamu ktk kuendesha kilimo.
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Catan, wazo nilikuwa nalo na mwezi januari nikasafiri toka dar hadi kule nikanunua shamba lile just laki nne tu imagine na kuna camp pale ya wafanyakazi 3, casual labor tunapata huko huko sababu kwa sasa sina trekta - natumia jembe la ngombe.

  Ndiyo maana makadirio yangu nimesema yatakuwa around 5m tu. sababu labor ni cheap sana.
   
 6. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  big up my broda.safi sana.huo ndio mwendo mkuu!mungu akusaidie ufikie malengo yako.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Naomba kuwa mshirika kwenye mashamba yako ..I am serious Broda ...
   
 8. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hongera. Nadhani kila mtu inabidi atafute kitu mbadala cha kufanya na ulichofanya wewe ni kitu kizuri.
  Ila hujasema unalima zao gani. Mahindi au maharagwe? Au maua (labda ya mbegu, ndio unazalisha kwa magunia)?
   
 9. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Super profit! Kadrio la juu! Kwa uzoefu wangu there is always some miscellaneous costs and Yield loss! Lakini ukweli ni kwamba biashara inalipa! Kila kheri!
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sorry - ni mahindi mkuu. then baadaye nitafikiri kuweka maharage. ile sehemu ina rutuba sana hakuna haja ya kutumia mbolea ya aina yoyote.
   
 11. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,670
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 135
  I real appreciate your thoughts and actions
  Hongera sana kaka.
  Tupo nyuma yako kwa hili
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sawa kuna miscellaneous lakini kupita 5m target is vigumu - kwa mafano sasa hivi mpaka upandaji nitakuwa nimetumia 2m tu - palizi nitaweza kutumia 1m nyingine - uvunaji na kuhifadhi ni 3m approx
  hata ukisema nipate magunia 20 kwa heka still jumla itakuwa tatal gunia 1000 times 60,000 = 60m ( Kadirio la chini kabisa)
   
 13. N

  Ngala Senior Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umepata michango ya kukupa moyo mkuu lakini mi nakukumbusha kuwa l hekta =l00m by l00m na sio 70m by 70m. Pili umelenga umwagiliaji au rehema za Mungu kama ni umwagiliji nakupa hongera na kama ni mvua za Mungu basi usijipe matumaini kupitiliza usijeukasema pekee yako barabarani. Kumbuka nguvu ya soko inategemea mahitaji hilo nalo jiandae nalo. Kuna wadudu wanyama na ndege waharibifu nalo pia jiandae.yapo na mengine wanzangu watanisaidia kujazia vinginevyo nakupa HONGERA SANA wasomi wanatakiwa sasa mashambani kuibadili TIIZEEDII YETU
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  kwa kuanza ni mvua za rehema ya mwenyezi mungu - cha kuzingatia pale ni kupanda at a right time na mbegu ya muda mfupi. Wanyama, ndege na wadudu hapo hamna tatizo kabisa, hayo ndiyo mambo yaliyofanyiwa kazi wakati wa upembuzi yakinifu ( feasibility study) ambao ulifanyika kwa uangalifu mkubwa.

  Kwa sababu mtaji ni mdogo, suala la umwagiliaji litakuja baadaye sana - kwa sasa najikita kwenye kilimo cha nvua za mungu.

  pia nimejipanga kununua mahindi extra toka kwa wakulima wenzangu wadogo wadogo wakati wa msimu wa uvunaji- let say gunia zingine 1000, hapo naweza pata kwa bei nzuri - na nitauza hapa dar, hii itaniongezea mtaji wangu kukua zaidi.

  Kadri mtaji unavyokuwa ndiyo kadri nitakavyobadili mfuno wa ukulima wangu - kwa sasa nimeanza kwa hivi.

  I do agree with you kwamba challenges lazima ziwepo katika kila jambo unataka kufanya - i'm ready to face them.
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Thanks FristLady1 kwa moyo wako wa kutaka ushirika - kazi ni ngumu kidogo lazima u dedicate at least 4 days kila mwezi kwenda site kufanya physical monitoring. kule ni camp bado kwa hiyo utahitaji kwenda na Maji ya kunywa for those days, safari bed na vitu vingine personal.
  Chakula ni Local food, hakuna umeme, maji ya kuoga ni ya kisima (local), rafiki zako kwa those 4 days ni ndege - its real camping life - ni kama vile Maisha plus
   
 16. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 60
  Great idea mkubwa
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Mie nigependa kuwa jirani yako! tuweke two big estates unasemaje?
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  tuombe Mungu jina lako lisilete shari, ndugu
   
 19. T

  TANURU Senior Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe sana mkuu. Binafsi nahitaji kama ekari 200 kwa ajili ya kupanda miti ya mbao je naweza kupata?
   
 20. Renegade

  Renegade JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 4,208
  Likes Received: 1,564
  Trophy Points: 280
  I like that , All the best Bro.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...