Nimeamua kujilipua. Nimeanza upya

Nimeamua kujilipua. Nimeanza upya

Hongera bwana sio kila mafanikio mje kusema hapa mtawauwa bure watoto wa watu .

Mfano mimi jana tu nimelala na mademu wawili wa kwenda ila sijasema kwa watu nimevunga nafrahia moyoni kimya kimya hivyo ni rahisi badaye kupata demu mwingine kirahisi
ID fake zinatusaidia sometimes. Japo kuna baadhi tunajuana huku
 
Wanajamii mko fresh eee...

Ebwana haya maisha ni noma sana, mambo yanachanganya na mengine yanachosha moyo.
Baada ya kujitafuta sana kwa miaka mitano kwenye harakati mbalimbali, hatimaye leo nmeamua kubadili mwelekeo wa mambo.

Nilianza na kupanga chumba kimoja, baada ya mwaka nikaona nina uwezo wa kumudu nafasi kubwa zaidi... nikahamia chumba na sebule. Harakati hazikupoa, nikaona nioe.

Huko nikaishia kupigwa za uso na nikamfukuza mke. Maisha yakawa bomba sana kwa kiasi chake. Nikafanikiwa kununua viwanja vitatu, boda 2 na kuongeza msuli wa kazi.

Mwezi wa pili nilikaa nikaitafakari kazi + mazingira ninayoishi nikajiona ni kama mda wote sikuwa kwenye mstari ninaoutaka.

Niliamua kuuza kila kitu, viwanja vyote, boda zote na mzigo wa kazi nilokuwa naifanya hadi kila kitu cha ndani.

Nilikamata milioni 16 huku nikiwa sina hata pa kulala, japo chumba nilibaki nacho. Nilisepa nikaenda mkoa ambao sikuwahi hata kuufikiria, nikasoma upepo nikaona kuna fursa.
Nilinunua mashine 2 za kukamua alizeti pamoja na mashine 1 ya kuparata mkonge then nikaingia sokoni.

Niliajiri vijana 9 nikaanza kukimbizana na fungu la kupata au kukosa.

Kwa sasa maisha yameanza na ukurasa mpya. Hadi sasa nimesev milioni 7 tu kwa miez 2.... japo ka moyo kanadunda kwa maamuzi nilochukua.

Ila fresh... nimejilipua.
Umefanya kitu kikubwa usikate Tamaa endelea kupambana Allah atakufanyia wepesi utakua mtu mwenye uwezo mkubwa baadae 🔥🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom