Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Ndugu pole sana yamenikuta hata mm niliazia voda shop k/ manyanya wakazingua ivyoivyo nikasema ngoja niende mlimani huko ndio nilikitana na viroja maswali yote nikapatia cha ajabu akanimbia hujapiga simu muda mrefu kama miezi miwili ila mpesa unatumia marakwa mara sawa akasema sasa andika barua upeleke kwa meneja nikamwambia Dada kwani naomba kazi kwenu nikachana karatasi uyo nikatembea zangu wanazingua mbaya foleni kibao
 
voda ni kizamani sana,na wana ---- wao mmoja mweupe hivi anajifanya kizungu kingi nae anamajivuno kwa mb wanazotuibia,siipendi kampuni hii
 
Mkuu mimi niliwatupia fomu yao pale mlimani city, Kwa jambo hilihili na nikaachana na line yao mpaka leo, kisa eti namba mbili hazikufanana,.

Pole mkuu hawa wameshiba sasa wametutapikia ,mim nilipoteaza ,sasa nikawa mdogo kwa kuwa kwenye sim kulikuwa na sh kama 800000 hivi nilpo ipata tu nikaipaki hadi leo
 
Mimi nilishafunga ndoa na Voda na sito waacha
 
Tatizo hii mitandao ya simu sio reliable kabisa.

Unaweza kuhamia Airtel halafu ukafika huko wakaanza kukuzingua kama Vodacom.

Nilikuwa mteja wa tigo toka wakati inaitwa buzz ni bomba, niliwasababishia usumbufu mkubwa sana wale waliokuwa na simu yangu.

Nimeamua kutohama tu japo internet ni kichomi siku hizi.
 
Tatizo ni kuwa na regulator legelege.

BTW Voda wanafanya marudisho ya pesa ooops peremende alizokuwa anagawa Jambazi Sugu.
 
Vodacom mkoa wa Mbeya network yao imekuwa Bomu! Ukipiga simu kwa mtu inaanza kukata pesa hata bila kuita na mtandao wao unasumbua balaah
 
Nilikosea kutuma m pesa kuwapigia voda nikaulizwa passport,tena dada kashupalia hiyo tumebishana nusu saa ambapo alitakiwa ablock pesa,mpaka zikachukuliwa tena na wakala wa voda,nikaambiiwa nitarudishiwa akiweka hela,mpaka leo mwaka sasa nimedhulumiwa
 
Mimi tangu waondoe hyo Uhuru bundle, nimewaweka kando. Nipo na tiGO now Freebasics.
Sasa sijui mjanja nani lile buku nilokuwa narecharge daily sasa hawalambi tena.
Loss report ya polisi sio mbaya maana inakulinda na wewe. Ila all in all Vodacom lazima wabadilike maana hamna namna nyingine sasa! Nyuma kidogo nilikosea kutuma hela nikawaomba wanirudishie hela yangu... hadi kesho sijapata nawavumilia tuu ila nawategea!! Kuniondolea unlimited ya 1000 kwa siku nimewamaindi sana asee!!! Manyanyaso yanazidi kuwa mengi asee!! Wapi halotel!!!!!!!!!!!!!!
 
Voda ni majanga jamani, siitaki kuiona wala kuisikia kero zake zooote nazifahamu fika
 
Umekutana na mpuuzi sana. Mi nlikua sijatumua line ya tigo mwaka mzima na nlikua sikumbuki namba hata moja ya mwisho wala tigo pesa ila kitambulisho kiko sawa wakarenew hapo hapo. Na airtel nliibiwa simu hata hawakuhitaji huo upuuzi mwingi hvy. How does a person remember all that shit? Umechelewa kugundua kwamba voda ni wajinga. Mi siku hizi voda simu inakaa home. Naitumia kama mtu ananitumia pesa na hana mtandao mwingine

Kwa mtiririko wa uzi huu nadhani Voda, watajirekebisha.
 
Kwanza wamekua wezi sana siku hizi, nimejiunga na kifurushi jana usiku alaf sijapiga hata simu moja, eti leo naamka asubuhi nakutana na sms kuwa kifurushi changu kimeisha na wakati hakijakaa hata masaa 12 tu
 
Si kwamba ni utaratibu wa TCRA? Maana wizi wa kutumia simu umekithiri sana.

Pia ni muhimu ukaripoti polisi upotevu wa simcard yako, maana inaweza kutumika vibaya halafu ikakuletea shida nyingine tena. Loss report ya polisi inakusaidia wewe endapo simu yako au simcard/namba yako ikijatumika kwenye uhalifu.

Lakini kwa vyovyote vile urasimu unakera sana.

Nilishaibiwa cmu nikaenda police nipate lost report nikaelezwa niende kwenye voda kisha nirudi polisi kwakweli ni shida na usumbufu itafutwe njia nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom