Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Heshima sana wanajamvi,

Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.

Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.

Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.
mkuu unahama vodacom uhamie wapi? tigo? airtel , zantel, smart, au halotel?
kwa taarifa yako tu, kama umeona huo ni usumbufu hadi ukaondoka voda, huduma kwenye hii mitandao mingine ni za kusuasua sana
alafu kwa ninavyokuona wewe ni mswahili na mtu wa lawama sana, hapo umepoteza line ukakaa wiki 2 bila ku renew ukasahau namba wewe unakutana na dada ambaye anafuata masharti ya kazi yake unamlaumu?
na vodacom hayo masharti waliyowekwa ndiyo yaliyowekea na tcra na yanatakiwa yafuatwe na kila mtandao, voda hawana njaa sana na wateja nenda labda halotel au tigo huko ambao una renew line kwa taarifa fake kiasi kwamba unaweza ku renew hata line isiyo yako ukafanya nayo utapeli
acha kumtusi dada wa watu makosa unayo wewe
 
Mkuu hiki ulichoandika hapa sidhani kama kuna usahihi sana. For starters natumia airtel na voda na bila ubishi airtel wana vifurushi matata sana.angalia vyote vya data na kupiga simu. Kuhusu ufeki… makampuni yenye matawi zaidi ya nchi nane afrika kweli yakiwa feki basi serikali imeamua yawe feki (ingawa sioni popote huo ufeki wao kihuduma)
 
Kati ya mitandao wezi ni vodacom ukiweka buku ukinunua mb,za jero ile itakayobaki inaliwa ju,kwa ju!
 
Si kwamba ni utaratibu wa TCRA? Maana wizi wa kutumia simu umekithiri sana.

Pia ni muhimu ukaripoti polisi upotevu wa simcard yako, maana inaweza kutumika vibaya halafu ikakuletea shida nyingine tena. Loss report ya polisi inakusaidia wewe endapo simu yako au simcard/namba yako ikijatumika kwenye uhalifu.

Lakini kwa vyovyote vile urasimu unakera sana.
Mkuu umenena vilivyo. Wizi wa mitandao umekithiri kwa kiwango cha juu sana. Swali kwa mlalmikaji, je utajisikiaje siku unaenda voda baada ya kuona sim kadi yako haifanyi kazi ghafla? Na ukaambiwa kuna mtu kafojisha kitambulisho kaweka majina yako na picha yake na kwenye fomu hakuweza kujibu Yale maswali (hajajaza). Na unaangalia kwenye a/c ya M-PESA unaambiwa hela yote imetolewa na unaenda kucheki benki unaona zaidi ya mil.10 imeibiwa. Nataka nimuulize mlete mada ata react vipi kwa hawa wenye mtandao?
Muda mwingine procedure zikiwa ngumu labda zinaweza kusaidia kulinda hizi akaunti zetu za mitandao ya simu na sim banking.
 
Mkuu hiki ulichoandika hapa sidhani kama kuna usahihi sana. For starters natumia airtel na voda na bila ubishi airtel wana vifurushi matata sana.angalia vyote vya data na kupiga simu. Kuhusu ufeki… makampuni yenye matawi zaidi ya nchi nane afrika kweli yakiwa feki basi serikali imeamua yawe feki (ingawa sioni popote huo ufeki wao kihuduma)
voda wapo vizuri kuizidi airtel, kulinganisha ubora usiangalie vifurushi tuu, voda ni wazuri zaidi kwa kua wametanda tanzania nzima, internet yao hata ukienda kijijini unaipata vizuri, huduma za m pesa pia zipo kila mahali kila kijiji tz, na huwa hawasuisui kukatika kwa mawasiliano kama hawa wengine
kuhusu swala la ufeki nilikua namaanisha kuna mitandao mingine unaweza ukaenda uka renew line {isiyo yako} kwa kua hawazingatii sana details nyingi kama voda, unaweza ukajua namba chache tu za huyo mtu mwenye line na kitambulisho chako feki then unapata line ya mtu, (wengine hawaulizii hata kitambulisho!) hapa mimi sizungumzii matawi mengine africa nazungumzia matawi yaliyopo tz kwa kua watoa huduma kwa wateja hawapo sawa kwa nchi zote
 
Heshima sana wanajamvi,

Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.

Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.

Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.
Mkuu mimi umenitonesha donda langu ni karibu mwezi wa pili sasa line yao nimeweka kabatini tena ina kiasi flani cha Pesa inaniuma sana.

Line yangu Ilipotea Mimi Niko mukoani tena vijijini nikaungaunga nauli nikaenda mjini na kitambulisho changu nikaulizwa maswali mengi.
Nikafanikiwa kurudisha line yangu wakaniambia Huduma ya mpesa itarudi baada ya Massa 24 nimesubiri haya masaa24 hadi Leo bado nikiwauliza wananitaka nirudi tena mjini nikatoe maelezo.
Sasa line nimehamishia kabatini nauli ya kurudi kwenye maduka yao yaliyoko mjini sina.
 
kwa voda ukitaka huduma poa nenda pale tandika, kuna braza flan yank ni muelewa sana,, voda hata wa mliman pale kuna wahudum wapumbav sana?
 
mkuu unahama vodacom uhamie wapi? tigo? airtel , zantel, smart, au halotel?
kwa taarifa yako tu, kama umeona huo ni usumbufu hadi ukaondoka voda, huduma kwenye hii mitandao mingine ni za kusuasua sana
alafu kwa ninavyokuona wewe ni mswahili na mtu wa lawama sana, hapo umepoteza line ukakaa wiki 2 bila ku renew ukasahau namba wewe unakutana na dada ambaye anafuata masharti ya kazi yake unamlaumu?
na vodacom hayo masharti waliyowekwa ndiyo yaliyowekea na tcra na yanatakiwa yafuatwe na kila mtandao, voda hawana njaa sana na wateja nenda labda halotel au tigo huko ambao una renew line kwa taarifa fake kiasi kwamba unaweza ku renew hata line isiyo yako ukafanya nayo utapeli
acha kumtusi dada wa watu makosa unayo wewe

Mkuu real G toroka uje Airtel Muzee Tsh 35,000/= Mwezi mzima unatwanga mitandao yote dakika 700 sms 6000 300 MB huko Voda ushuzi mtu wala sitakiwa kuwasikia.
 
Back
Top Bottom