Heshima sana wanajamvi,
Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.
Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.
Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.