Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Nimeamua kuachana rasmi na Vodacom

Eti nenda Polisi kaandikiwe loss report sijui wanafikiri tuna muda mchafu.Polisi mtu unakwenda kama kuna issue ngumu si mahali pa kwenda hovyo hovyo na vi issue vya kijinga.

Pole mi nilireneaw hivi karibuni laini yangu wakaniambia baada ya masaa arobaini na nane piga huduma kwa wateja nikapiga maswali ya huko ya kawaida sasa likaja umereneaw laini tarehe ngapi nikamwambia hiyo itakuwa ngumu kukumbuka manake hata karatasi niliyojaza nimeiacha palepale jibu likawa sitaweza kukuhudumia maswali mengine nimeyajibu sahihi hilo moja tu huduma hamna nilikwazika sana lakini tutafanyeje sasa MTEJA VODA KWAO NI MBWA TU!
 
teheteh Ngongo Una huishiwi vituko.............nakumbuka miaka ya nyuma Ulipoamua kuachana na Arsenal(kama sijakosea) ukaleta uzi na kichwa kama hiki..''Nimeamua kuachana rasmi KUISHABIKIA ...''

Sasa timu inapokulazimisha kwenda kusali kanisani unafikiri mchezo.

attachment.php
 
Haya makampuni binafsi na hata ya serikali, mengi yana watumishi wana viburi, dharau na majibu mabaya sana. Kama si kutumia hekima kwa wateka wengi, basi matusi hata kupigwa vingewaandama. Katika dunia ya sasa, mteja mbali na kuwa mfalme, ndio mpango mzima. Wanatakiwa kutukarimu kwa nguvu zao zote. Isiteshe wengi wamepata mafunzo ziada ya huduma bora kwa mteja, sijui tatizo lao nini???. Tubadilike jamani, tupende kusoma kujifunza human behaviors. Tutumie hizi smart phones zetu kuwa smart vichwani badala ya kuwa mbulula, itasaidia kuwajali wateja sana.
 
VODACOM huduma yao ya kununua umeme ina uwizi sana hadi sasa wameshanila karibia 20,000. Nawahama rasmi, ukiongeza internet wanavyopunja
 
Pole sana kaka! Karibu sana Airtel.Mapungufu yapo ila mambo ya kipuuzi kama hayo hakuna.
 
Voda huduma zao mbovu sana. Mi nilienda baada ya wao kufunga line yangu kwasababu sikuitumia kwa zaidi ya mwaka, nilienda ofisi zao za samora. Tulikuwa kama wanne tu kuhudumiwa ilikuwa kazi nilisimama zaidi ya dakika 45 halafu yule mama akaanza kuleta usumbufu wake, nikampa kitambulisho akasema sio nilichosajilia, sasa kama jina ni hilo hilo ila kitambulisho ni tofauti tatizo ni nini? Ila nilimwambia tu kuwa ana hiyari ya kunipa au la nivuke barabara niende Jmall nikaongeze line moja kati ya tigo au airtel. Akajishauriiii mwisho akanipa
 
Hawajakuuliza salio la M pesa?mi walinichosha nikaachana nao nikaingia kwa mtaa nikakwarua ya tigo na airtel sas iv nmeongeza halotel......voda wamebweteka..mabwenyenye
 
Kwa hapa bongo mitandao ya simu bado sana. Kwenye ishu ya internet ndo balaa kabisa. Ivi mm huwa najuliza kwa hii internet ya tigo ivi tigo wanaweza sema wana huduma ya internet kweli? Coz ukienda umbali wa mita 100 kutoka kwenye mnara unaosupply internet unakuta ki E hakipandishi wala kushusha internet km ulikuwa una surf ndo nitolee iyo. Yaan hovyo kabisa
 
Nimefurahia michango yenu sana. Kusema ukweli Nina addiction na Vodacom. Naifurahia sana internet yao sjawahi kupata shida nao ila vifurushi vya 12hrs vinaudhi. Pole ndugu kwa customer care mbovu ya ulipoenda. Karibu kwenda hqs huenda hapo ni VODA shop tu
 
Customer care wa Vodacom hasa pale mlimani city wanaringa sana, utasikia Mara kitambulisho kina picha ya zamani kalete barua ya serikali za mitaa, kwa ujumla wanatuchosha wateja
 
Ndio mkuu voda wanasumbua san mm nakumbika last year nilikuwa na shida hiyo hiyo lkn waliwrza kunisadia lakn ilikuwa mbide mpaka uwapigie had simu
 
Heshima sana wanajamvi,

Wiki mbili zilizopita simu yangu ilikwapuliwa na watoto wa mjini kwakuwa nilikuwa na safari nyingi nje ya mkoa sikupata nafasi ya kurenew line yangu.

Leo nikaamua kwenda ofisi za Voda Uhuru road kwanza nikakutana na foleni kubwa kiofisi kidogo hewa gongana nikataka kuondoka lakini nikaona isiwe taabu ngoja nikomae.Kwanza nikapewa fomu nikatakiwa kujaza simu tano za mwisho,m pesa tano za mwisho,sijui kifurushi cha internet......Mara kitambulisho nikamaliza kupeleka fomu kwa mdada mwenye maringo ya kijinga kaona ajira ya Voda mali sana imemwezesha kupaka wanja na kubadili vigauni vya mtumba kabonyeza bonye computer kanirejeshea fomu namba za watu wa mwisho kuongea nao tatu sio sahihi nikamwambia kwakuwa mbili ni sahihi na simu iliibwa wiki mbili zilizopita si rahisi kukumbuka zote.Kachukua fomu kaandika loss report nenda polisi wakakujazie ebo nikamwambia nani kakwambia nina muda mchafu kwani Voda ipo yenyewe kwa taarifa yako nina line nyingine za mitandao 3 hizi si zama za TTCL na ukiritimba za enzi za Mwl nikachana fomu nikaitupia kwenye dustbin nikamwambia Vadacom kwaheri.

Masharti ya kupata line mpya iwapo simu imepotea/imeibwa yamekaa kizamani sana kama taarifa zangu zipo sahihi eg kitambulisho nilichosajilia simu,majina na nk yapo sawa kwanini wanaleta urasimu wa kuangaisha wateja.

Mkuu mimi niliwatupia fomu yao pale mlimani city, Kwa jambo hilihili na nikaachana na line yao mpaka leo, kisa eti namba mbili hazikufanana,.
 
Si kwamba ni utaratibu wa TCRA? Maana wizi wa kutumia simu umekithiri sana.

Pia ni muhimu ukaripoti polisi upotevu wa simcard yako, maana inaweza kutumika vibaya halafu ikakuletea shida nyingine tena. Loss report ya polisi inakusaidia wewe endapo simu yako au simcard/namba yako ikijatumika kwenye uhalifu.

Lakini kwa vyovyote vile urasimu unakera sana.

Mkuu hujapoteza SIM card ya voda labda ndo maana, nilikutana na dada mmoja wa Voda pale mlimani city, alivyokuwa ananijibu kwa nyodo na maringo ile form ya ku renew SIM card , nilimwachia mezani nikaondoka jumla ikawa ndo mwisho wangu na voda.
 
Mkuu hujapoteza SIM card ya voda labda ndo maana, nilikutana na dada mmoja wa Voda pale mlimani city, alivyokuwa ananijibu kwa nyodo na maringo ile form ya ku renew SIM card , nilimwachia mezani nikaondoka jumla ikawa ndo mwisho wangu na voda.
Ni kweli mkuu sijawahi kupoteza simcard yoyote. Ila naelewa tatizo la customer service kwa nchi yetu hii.....sio Voda tu, hata ukienda kwenye mabenki, petrol station na pengine hata bar. Ni shida sana. Nitashanga sana kama tigo na airtel wapo tofauti katika hilo. Niliwahi kupiga customer service ya tigo sina hamu mpaka leo. Hata Voda pia ni shida.
 
Kwa sasa kama hujafanya simswap maana yake ni kuwa ile line yako iliyoibwa inaweza kutumika na mtu aliyeiiba. Pengine utaratibu wa Voda sio mzuri, lakini kwa ujumla wake matukio mengi ya wizi katika simu (mobile money) mara nyingi yanahusisha simswap.

Kwa kutoripoti polisi, hiyo ni hatari (risk) kwako. Hata kama hutaki kupata line yako ya zamani lakini kuripoti polisi kuwa imeibwa ni kinga muhimu.

Well, pengine sio jambo kubwa kivile!

Sasa cha ajabu, baadae ya kushindwa ku renew SIM card yangu ya voda Kwa ajili ya urasimu wao, baada ya muda ile Namba yangu wakauza Kwa mtu mwingine, na anaitumia mpaka sasa. Imeniuma sana sitaki hata kuwasikia hawa watu.
 
Back
Top Bottom