Nimeamua kuachana na CHADEMA

Nimeamua kuachana na CHADEMA

Wangesema nisingeingia hasara ya kununua Lt 5 ya mafuta mgando,nisingenunua miwani ya kukinga macho yangu na mabomu ya machozi,nisingeamua alfajiri na baridi ya Arusha kukimbia 10 km ?.Ebo wengine hatupendi utani ukisema sisi tunatenda.
Ha ha ha ha!
 
..lengo la maandamano ni kufikisha ujumbe wa kupinga udikteta kwa wananchi.

..naamini ujumbe umefika pamoja na kwamba maandamano hayajafanyika.

..mikutano na maandamano yangefanyika bila shaka Polisi wangeingilia na kuumiza waandamanaji.

..uamuzi wa Kamati Kuu umewanyima Polisi nafasi ya kutekeleza uovu wao dhidi ya wanachama wa CDM.
Sizitaki mbichi hizi...
 
Nilishauona ule mwisho kabla ya mwanzo!! Ni falsafa!! Imeandaliwa! Ikasemwa!ikaeleweka! Kuna waliosubiri iwe Leo! Wengine kesho!! Hahahaaa too late!!kumbe ilishakamilika toka Jana!!

Mwenzako nimefura na mihasira imebidi nijikalie mahali nipooze roho na kichupa cha wine sina hamu,niko na wadau wamenishauri nijiandikishe Mount Meru Marathon 😕
 
Ujumbe wako hauna mashiko na maamuzi yangu.

Hauwezi kuwa na mashiko maana siwezi kukuandikia kukufurahisha zaidi ya kukutakia kila lakheri katika kutafuta furaha yako mpya period.
 
Hee Omo ya nini tena.
 
Chadema walikosa uugwaji mkono toka kwa wanaichi wa kawaida, sababu Magufuli anakubalika kwa watu wengi. Wakaona wataumbuka kwa zoezi lao kuto ungwa mkono
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo tarehe 31/08/2016 nimeamua kuachana na CHADEMA na kujishuhulisha na masuala ya michezo tu hasa mpira wa miguu.

Nilikuwa shabiki wa siasa bila kuunga mkono chama chochote cha siasa,kama mtanzania hata kama si mpenzi wa vyama bado nilikuwa na wajibu wa kuunga mkono jambo ninaloliona lina manufaaa kwa taifa.Tamko la viongozi wa CHADEMA la kututaka tuandamane nilikubaliana nalo kwa asilimia 100%, kwasababu madhumuni yake yalikuwa kupigania utawala wa sheria,kulinda uhuru wa kupasha habari,uhuru wa kusikia maoni kutoka vyama vyote si chama kimoja tu uku vingine vikizuiliwa hii ni hatari sana.

Viongozi wa CHADEMA walitangaza rasmi tarehe 01/09/2016 yangefanyika maandamano na mikutano nchi nzima.Makamanda walitumwa sehemu mbali mbali za jamhuri ya Tanganyika (Zanzibar ni nchi nyingine hainihusu) Ngongo na wapigania demokrasia hawakuhitaji kuhamasishwa na makamanda toka makao makuu tayari tulishafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia kilometa kumi kila siku asubuhi ili kuuweka mwili katika hali ya utayari kukabilia na nginja nginja ya Polisi.

Tulishanunua mafuta (sina uhakika kama yangesaidia) kwaajili ya kuilinda ngozi dhidi ya maji ya washawasha,tulisha nunua miwani isiyopitisha hewa kwaajili ya kujilinda na mabomu ya machozi (sina hakika kama zingesaidia) kwa ujumla maandali yalikuwa yamefikia 95% ghafla bini vuuu Kamanda anahairisha maandamano ?

Hii haikubaliki nasema haikubaliki kabisaa lazima viongozi watambue wajibu wao katika kila matamko yao si unatamka leo hivi kesho unatenda vingine.

Mwezi mmoa aliotoa kamanda wetu Mbowe hauna maana makamanda wameswekwa rumanda, wanachama na wapenzi wamejiandaa vya kutosha hatuna uhakika na hizo siku 30.
Lumumba kazini!
 
Kakudanganya nani unafikiri wenye nchi wangejua CHADEMA hawana support wangejishuhulisha namna hiyo.Kwanza hiyo Budget ya kuvunja UKUTA ukiambiwa unaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo bureeee.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo tarehe 31/08/2016 nimeamua kuachana na CHADEMA na kujishuhulisha na masuala ya michezo tu hasa mpira wa miguu.

Nilikuwa shabiki wa siasa bila kuunga mkono chama chochote cha siasa,kama mtanzania hata kama si mpenzi wa vyama bado nilikuwa na wajibu wa kuunga mkono jambo ninaloliona lina manufaaa kwa taifa.Tamko la viongozi wa CHADEMA la kututaka tuandamane nilikubaliana nalo kwa asilimia 100%, kwasababu madhumuni yake yalikuwa kupigania utawala wa sheria,kulinda uhuru wa kupasha habari,uhuru wa kusikia maoni kutoka vyama vyote si chama kimoja tu uku vingine vikizuiliwa hii ni hatari sana.

Viongozi wa CHADEMA walitangaza rasmi tarehe 01/09/2016 yangefanyika maandamano na mikutano nchi nzima.Makamanda walitumwa sehemu mbali mbali za jamhuri ya Tanganyika (Zanzibar ni nchi nyingine hainihusu) Ngongo na wapigania demokrasia hawakuhitaji kuhamasishwa na makamanda toka makao makuu tayari tulishafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia kilometa kumi kila siku asubuhi ili kuuweka mwili katika hali ya utayari kukabilia na nginja nginja ya Polisi.

Tulishanunua mafuta (sina uhakika kama yangesaidia) kwaajili ya kuilinda ngozi dhidi ya maji ya washawasha,tulisha nunua miwani isiyopitisha hewa kwaajili ya kujilinda na mabomu ya machozi (sina hakika kama zingesaidia) kwa ujumla maandali yalikuwa yamefikia 95% ghafla bini vuuu Kamanda anahairisha maandamano ?

Hii haikubaliki nasema haikubaliki kabisaa lazima viongozi watambue wajibu wao katika kila matamko yao si unatamka leo hivi kesho unatenda vingine.

Mwezi mmoa aliotoa kamanda wetu Mbowe hauna maana makamanda wameswekwa rumanda, wanachama na wapenzi wamejiandaa vya kutosha hatuna uhakika na hizo siku 30.

Umesahau jaji Mutungi aliwaita wenyeviti wa vyama vya siasa ili kuongea nao juu ya suala la UKUTA, na wenyeviti wa hivi vyama unawajua, au unajua wameongelea nini kweye huo mkutano wa siku mbili????
Mwezi mmoja si mwingi, ngoja tuone kama bado tutaendelea kukatazwa kukutana wakati chama cha magamba kinaendelea na siasa.
Unacheza na CDM wewe!
 
Ebu nijuze basi mkuu wangu labda kulikuwa na hoja za maana.
 
Mbowe kanisababishia Hasara ya 3.2M ya Vifaa tiba nilivyoweka kwny Pharmacy yangu kusubiri Sept 1
Mimi na cdm damu damu iwe kiangazi iwe masika, siwezi nunua kitu kwenye duka la mfuasi wa magamba hata kama ni dawa ya kuokoa uhai wangu.
 
Back
Top Bottom