Nimeamua kuachana na CHADEMA

Nimeamua kuachana na CHADEMA

Kamanda Ngongo hasira hasara.

Chama cha siasa ni mbinu. UKUTA umefanikiwa kwa 80%. Wote tumeona reaction ya serikali na vyombo vya dola; hii inaonyesha nguvu ya CHADEMA Tanzania. Hata hivyo operesheni UKUTA haijafutwa bali imesogezwa mbele kwa ushauri wa viongozi wa dini.
Aluta continua!

Mkuu unakijua kile kilima cha ESAMI mwenzako kila siku saa 11 napandisha round za kutosha mwili uko fit kweli kweli unadai haki yake sasa sijui nikajiandikishe Mount Meru Marathon ?.
 
umefanya uamuzi sahihi kwa muda na wakati sahihi...... chadema wanaendesha mambo kiujanjaujanja hususani toka Dr.Slaa aachie ngazi kwa umangimeza wa mbowe!!!! pale hamna chama bali limebakia jina tu............ leo wanasema hili kiesho wanasema lingine..... hakika ukuta umesamaratika.... watakuja na hoja nyingine nyepesi mnooo...... trust me
 
Umechelewa kushtuka bora ujiunge na Desi upande mbegu kuliko ulipokuwa
 
Ngongo una NASABA na leProfesseri lipumba!

kuna kipindi kama sikosei uliwahi kuhama Arsenal ukahamia man utd! KWA KIFUPI WW NI POPO SHWAIN
 
Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
tunatumia historia kurekebisha mapungufu ya yaliyopita na kujenga mema ya kesho sio kwa kuleta porojo! Dr slaa kukumbukwa atakumbukwa tu kwani ni principle awe ametenda mema au mabaya
 
Ngongo una NASABA na leProfesseri lipumba!

kuna kipindi kama sikosei uliwahi kuhama Arsenal ukahamia man utd! KWA KIFUPI WW NI POPO SHWAIN

Uliamini kweli nilikuwa mpenzi wa Arsenal ?.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo tarehe 31/08/2016 nimeamua kuachana na CHADEMA na kujishuhulisha na masuala ya michezo tu hasa mpira wa miguu.

Nilikuwa shabiki wa siasa bila kuunga mkono chama chochote cha siasa,kama mtanzania hata kama si mpenzi wa vyama bado nilikuwa na wajibu wa kuunga mkono jambo ninaloliona lina manufaaa kwa taifa.Tamko la viongozi wa CHADEMA la kututaka tuandamane nilikubaliana nalo kwa asilimia 100%, kwasababu madhumuni yake yalikuwa kupigania utawala wa sheria,kulinda uhuru wa kupasha habari,uhuru wa kusikia maoni kutoka vyama vyote si chama kimoja tu uku vingine vikizuiliwa hii ni hatari sana.

Viongozi wa CHADEMA walitangaza rasmi tarehe 01/09/2016 yangefanyika maandamano na mikutano nchi nzima.Makamanda walitumwa sehemu mbali mbali za jamhuri ya Tanganyika (Zanzibar ni nchi nyingine hainihusu) Ngongo na wapigania demokrasia hawakuhitaji kuhamasishwa na makamanda toka makao makuu tayari tulishafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia kilometa kumi kila siku asubuhi ili kuuweka mwili katika hali ya utayari kukabilia na nginja nginja ya Polisi.

Tulishanunua mafuta (sina uhakika kama yangesaidia) kwaajili ya kuilinda ngozi dhidi ya maji ya washawasha,tulisha nunua miwani isiyopitisha hewa kwaajili ya kujilinda na mabomu ya machozi (sina hakika kama zingesaidia) kwa ujumla maandali yalikuwa yamefikia 95% ghafla bini vuuu Kamanda anahairisha maandamano ?

Hii haikubaliki nasema haikubaliki kabisaa lazima viongozi watambue wajibu wao katika kila matamko yao si unatamka leo hivi kesho unatenda vingine.

Mwezi mmoa aliotoa kamanda wetu Mbowe hauna maana makamanda wameswekwa rumanda, wanachama na wapenzi wamejiandaa vya kutosha hatuna uhakika na hizo siku 30.
Mkuu mbona umechelewa sana kutoa maamuzi.
Wengi walishajua hilo mapema tena miaka mingi tu iliypita.

Pengine sasa pamoja na wengine waliobaki mtajitambua kuwa chuki zenu kwa CCM haina maana mapenzi kwa CHADEMA.
Mbadala wa CCM hapa nchini haupo!!
 
Eeeeeh na bado

Muwafatao na maamuzi yenu poleni

Bora mfikirie kujiongeza kimaisha, mnapoteza muda bure na pesa kisa mmmmmmh virojo
 
Kamanda Ngongo hasira hasara.

Chama cha siasa ni mbinu. UKUTA umefanikiwa kwa 80%. Wote tumeona reaction ya serikali na vyombo vya dola; hii inaonyesha nguvu ya CHADEMA Tanzania. Hata hivyo operesheni UKUTA haijafutwa bali imesogezwa mbele kwa ushauri wa viongozi wa dini.
Aluta continua!
We naye mahaba yako kwa Lowassa yamekuzidi hadi umekuwa kama zu.zu tu!!! Umeipimaje hiyo 80%? Weka checklist ya objectives za UKUTA uanze kuanalyze mafanikio ya kila objective.

Nnavyojua objective kuu ilikuwa kupinga udikteta, je udikteta umeisha? Bado upo, kama ulikuwepo kweli!

Specific objectives zilihusisha Uhuru wa vyombo vya habari, bunge live and there is absolutely no change!!

Mmefanikiwa nini hadi useme 80%?? Rudi kwenye akili yako timamu! Mtu mwenyewe mamluki huko cdm umekuja na mafuriko ya lowassa, kesho ukingua wanakutimua na matusi juu kama mbwa!
 
Nimekwambia sina chama ila naunga mkono mambo ya maana yawe yamefanywa na chama chochote.Mfano niliunga mkono wazo la serekali ya CCM ya kufufua shirika letu la ndege,majuzi wameleta ndege mpya si mtumba toka Canada.Naunga mkono uhakiki wa wafanyakazi hewa,naunga mkono suala la kumaliza uhaba wa madawati,naunga mkono ujenzi wa reli Dar to Rwanda & Burundi lakini napinga ujenzi wa uwanja wa ndege CHATO,napinga matamshi ya Makonda wakati wa kuaga miili ya askari waliouwawa (ningekuwa mimi ni Rais ningetengua uteuzi wake mara moja)Nalaani matumizi mabovu ya jeshi la polisi hasa katika masuala ya kisiasa upooo ndugu yangu.
Swali jepesi:
Kama wewe unaunga mkono mambo ya maana na si chama, kwa nini leo umetangaza "kuachana na chadema"? Umesahau kwamba chadema ni chama? Hapa namaanisha kwamba kama ulikuwa unaunga mkono UKUTA kwa sababu uliona ni jambo la maana, kwa nini uachane na chadema? Keshokutwa wakiibuka na jambo jingine la maana utafanyaje?
 
Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
Siyo CDM tu wameachana na maandamano hata uvccm nao wameghairi
 
Mkuu mbona umechelewa sana kutoa maamuzi.
Wengi walishajua hilo mapema tena miaka mingi tu iliypita.

Pengine sasa pamoja na wengine waliobaki mtajitambua kuwa chuki zenu kwa CCM haina maana mapenzi kwa CHADEMA.
Mbadala wa CCM hapa nchini haupo!!

Hivi ujenzi wa uwanja wa ndege wa CHATO unaanza lini ?.
 
Swali jepesi:
Kama wewe unaunga mkono mambo ya maana na si chama, kwa nini leo umetangaza "kuachana na chadema"? Umesahau kwamba chadema ni chama? Hapa namaanisha kwamba kama ulikuwa unaunga mkono UKUTA kwa sababu uliona ni jambo la maana, kwa nini uachane na chadema? Keshokutwa wakiibuka na jambo jingine la maana utafanyaje?

Kwasababu hawasimamii wanachosema.
 
Sasa kama hukuwa na chama inakuwaje inaachana na CHADEMA?
Pia umenishtua nilidhani umeachana na mkeo/mmeo nilitaka kujua no kwa sababu gani,kumbe chama NOP achana nacho and MYOB.
 
Back
Top Bottom