kichwa cha habari hakiendani na ukichokiandika hapa mkuu! Kuna walakini wewe ni mmoja wa Wanalumumba! Ungeeleweka vizuri zaidi endapo kichwa cha habari kingesomeka hivi;Heshima kwenu wanajamvi,
Leo tarehe 31/08/2016 nimeamua kuachana na CHADEMA na kujishuhulisha na masuala ya michezo tu hasa mpira wa miguu.
Nilikuwa shabiki wa siasa bila kuunga mkono chama chochote cha siasa,kama mtanzania hata kama si mpenzi wa vyama bado nilikuwa na wajibu wa kuunga mkono jambo ninaloliona lina manufaaa kwa taifa.Tamko la viongozi wa CHADEMA la kututaka tuandamane nilikubaliana nalo kwa asilimia 100%, kwasababu madhumuni yake yalikuwa kupigania utawala wa sheria,kulinda uhuru wa kupasha habari,uhuru wa kusikia maoni kutoka vyama vyote si chama kimoja tu uku vingine vikizuiliwa hii ni hatari sana.
Viongozi wa CHADEMA walitangaza rasmi tarehe 01/09/2016 yangefanyika maandamano na mikutano nchi nzima.Makamanda walitumwa sehemu mbali mbali za jamhuri ya Tanganyika (Zanzibar ni nchi nyingine hainihusu) Ngongo na wapigania demokrasia hawakuhitaji kuhamasishwa na makamanda toka makao makuu tayari tulishafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia kilometa kumi kila siku asubuhi ili kuuweka mwili katika hali ya utayari kukabilia na nginja nginja ya Polisi.
Tulishanunua mafuta (sina uhakika kama yangesaidia) kwaajili ya kuilinda ngozi dhidi ya maji ya washawasha,tulisha nunua miwani isiyopitisha hewa kwaajili ya kujilinda na mabomu ya machozi (sina hakika kama zingesaidia) kwa ujumla maandali yalikuwa yamefikia 95% ghafla bini vuuu Kamanda anahairisha maandamano ?
Hii haikubaliki nasema haikubaliki kabisaa lazima viongozi watambue wajibu wao katika kila matamko yao si unatamka leo hivi kesho unatenda vingine.
Mwezi mmoa aliotoa kamanda wetu Mbowe hauna maana makamanda wameswekwa rumanda, wanachama na wapenzi wamejiandaa vya kutosha hatuna uhakika na hizo siku 30.
Ngbana bana mbona unapenda kususasusa na kuacha? Arsenal uliiacha, CHADEMA umeiacha kwa mwendo huu hata shemeji sijui kama hajaachwaManchester United FC
Mkuu Ngongo kilichotakiwa kufika kimefika mahala husika,ukiandika sawa!ukiimba sawa!ukilia sawa!ukiandamana sawa,kikubwa ni kufikisha ujumbe!! Na ujumbe umeshafika! Tuokoe gharama nyingine za fedha na damu,salute kwa UKUTA! Serikali nzima imejikuta ikijigonga na kuumia ukutani!! Asante Ukuta!Mwenzako nimefura na mihasira imebidi nijikalie mahali nipooze roho na kichupa cha wine sina hamu,niko na wadau wamenishauri nijiandikishe Mount Meru Marathon 😕
Ebu nijuze basi mkuu wangu labda kulikuwa na hoja za maana.
we dada umeongea ukweli watu wasiotaka kuusikia..Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
We kweli zuzu, tunataka utawala wa sheria we unamzungumzia slaa mwoga, yeye amechaguliwa toka wapi na anasimamia ilani ya chama kipi? Je CCM nayo italala hadi 2020? UKUTA bado nauona upo imara labda aje na tamko LA kuufuta kwani hata sisi (CCM) limetpoteza, tuna uchungu jumbo letu kwenda upinzani na tulikuwa na mkakati wa kulirudisha je hii ban ikiendelea hata serikali za mitaa tusubiri anguko kuu, thinks twice.Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
teh, ukuta umegeuka kifusiii, walishindwa kuhairisha week zilizopita wamesubiri masaa ndio wamekubali hawatowezaHahahaha yani kamanda aandamane peke yake?
hiki chama ni raha sana kwakweliNgbana bana mbona unapenda kususasusa na kuacha? Arsenal uliiacha, CHADEMA umeiacha kwa mwendo huu hata shemeji sijui kama hajaachwa
haahaa mkuu huyu ndio yule aliyenzisha thread kule jukwaa la sport akisema ameacha kuishabikia arsenalNgbana bana mbona unapenda kususasusa na kuacha? Arsenal uliiacha, CHADEMA umeiacha kwa mwendo huu hata shemeji sijui kama hajaachwa
Hizo ni tuhuma au hukumu ?Katika watu waongo na wanafiki humu JF ww upo kumi bora
Hahahh kumbe inawezekana.!Una andamana mbona wakati wakudai mkopo kuna mwanafunzi aliandamana mwenyewe mpaka ikulu.
Nadhani sasa watajifunza kuwa wana waheshimu hata wanao waona hawajasoma. Joyce kiria toka mwanzo aliwashauri kusitisha na akawambia hawatoweza lakini hawakutaka kusikia sasa angalia Lowasa na Mbowe wamekimbia na cement ya kujengea ukuta...teh, ukuta umegeuka kifusiii, walishindwa kuhairisha week zilizopita wamesubiri masaa ndio wamekubali hawatoweza![]()
![]()
![]()
hiki chama ni raha sana kwakweli
Si uliona tangazo la tenda gazetini, mchaakato wa kumpata mkandaradi uko mbioni.Hivi ujenzi wa uwanja wa ndege wa CHATO unaanza lini ?.