Nimeamini sisi UKAWA ni wasaka tonge tu

Nimeamini sisi UKAWA ni wasaka tonge tu

mbona na sisi tuliwafukuza Zito, Prof Mkumbo, Mwigamba, Said Arfi, yule aliyekua mbunge wa Bariadi, bila kuwaonea haya na wala kuwapa muda wa kujitetea? tusiangalie wengine tu, we must do mambo yote ambayo tusingetegemea wenzetu watufanyie
 
emu waambie maana hum ndan. ukiifagilia serikali unaonekana unataka kacheo kumbe walaa¡ aise kufulia kisiasa noma sana muulizen lowasa anavoteseka
 
Ukawa hawana mpya, wamegeuka watetezi wa majizi na matumizi ya hovyohovyo bila kujali maisha ya wanyonge.
Lowas alisema rafiki zake wafanya biashara wanaonewa kwa kulazimishwa kulipa kodi hata kama hawajikii kulipa. nchi hii.....halaf huyu ndie tulikuwa tunataka tumsukumie ikulu.!!!!!
 
Ukawa nimewatupa.. Nimekuja kugundua ni wapuuzi fulani hivi wasiojielewa.. Lakini rule yangu ni ile ile.. Rais CCM Mbunge Ukawa
 
Hali imekuwa ngumu Thamani ya shilingi Kwa dola bado inazidi kupishana , hakuna unafuu wowote , sera ya Majipu inatumbua vijipu Uchungu pekee , Bandari ya Dsm imekimbiwa na wateja kutokana na Ofisi zao kukaa zig zaga hawana mpangilio maalum Kama Bandari za Mombasa na Msumbiji , ATC wapo hoi kuna Watumishi wanalipwa mishahara bila kufanya kazi , Safari za nje zipo kimya kimya japo wanatudanganya kuwa zimefutwa kuna mengi yanafanyika nyuma ya pazia huenda nchi ikawa na hali ngumu zaidi kuliko Sasa .
nadhani umepata wenda wazimu. bandari ya dsm imekimbiwa au wamekimbia wenyewe. wale wafanya biashara bao walikuwa wakikwepa kodi na wwnye makontena hewa. biashara si mchezo ukizoea kukwepa kodi mfumo ukitengamaa kidogo na kuanza kubana ukwepaji huo lazima wengine wakimbie. mbona inaekeweka na kila mtu. usituambie eti ofisi zimekaa vibaya zigzag kwani kabla ya ujio aa Magufuli ofisi zilikaa vizuri hazikukaa zigzag?? angalia kamanda usije ukatumbuliwa na wewe kwa kutueleza uongo hapa
 
Habari zenu wanajamii,

Kiukweli mimi nimekuwa nafuatilia sana utendaji wa Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe magufuli, kiukweli anayotekeleza ni kama alikuwemo kweme moyo wangu, anatekeleza yale yote ya ukawa kama ukawa ilikusudia kuyafanya endapo ingechaguliwa.

Cha kushangaza na kinachonikera ni vile baadhi ya viongozi wa ukawa wanavyoponda uwajibikaji huu, inaniuma sana ninapoona kiongozi wa ukawa anasimama hadharani na kupinga utumbuaji, sasa najiuliza hivi ukawa hii inamaana kweli?

Kwanini inapinga? Kwani upinzani ni kupinga maendeleo?. Rais alipomtumbua aliyekuwa mkuu wa mkoa, ndugu -Sumaye, Lowassa n.k walipinga na kusema kwanini wasipewe nafasi wachunguzwe?

Pia juzi Kabwe katumbuliwa napo wamelalamika, sasa je, hivi hawa watu wanataka Rais afanye nini? hawaoni kuwa huo utendaji wa mazoea na uzembe na tume za uchunguzi ndizo zilizotufiksha hapa?

Inanikera sana kwakweli, hata humu, wanaharakati wa mitandao ya kijamii kama Yericko Nyerere naye anaposti hoja za kupingana na utumbuaji, hivi ukawa ingefanikiwa kuingia ikulu kumbe wangefanyaje? Kama mambo yenyewe ndo hivi bora kusiwe na upinzani maana tunachanganyana tu.

Kwa kweli nampongeza sana sana rais huyu mheshimiwa John Pombe Magufuli; na kwa unafiki unaooneshwa na ukawa ni dhahiri hawastahili hata kupewa nchi kwa dakika moja ni wanafiki na wasaka tonge tu.
Elimu yako? Halafu inatosha tu wewe kuwa wewe badala ya kutumia nguvu kujinasibisha na UKAWA.
 
Wewe unachojua ni kuzungukia kwa Lugumi, escrow, mabehewa mabovu, kivuko feki, Chenji ya Rada na ya Bunge la katiba , bomba la Gesi , vibali vya sukari kutafuna pesa kisha umejitoa Fahamu na kuona huko ccm hakuna Dhambi ?
Mkuu ulichokiandika kina fanana kabisa na Id yako,Funza..mara nyingi huwa wanapatikana chooni,kwa hiyo inaonyesha jinsi akili yako ilivyo athiriwa na kinyesi..We ulijitoa ufahamu kwakumpokea mtu aliyemtuhumu ni fisadi kwa miaka nane kupitia mikutano na vijarida vyenu vya mwanahalisi, mawio na Tanzania daima..halafu ghafra akawa malaika.
 
Wana jukwaa,

Naomba kuhoji hapa, hivi ni kweli hawa nduguzangu wa cdm hawaoni harakati na mipango mingi na mizuri inayofanywa na Dr Magufuli na Serikali yake???

Nilitegemea walau msemaji na bavicha kujitokeza hadharani na kumsifu pamoja na kumpa moyo katika harakati zake za kuipeleka Tanzania mbele hasa katika mapinduzi ya viwanda na kutokomeza rushwa pia kuleta usawa nchini. Ila wamekaa kimya tuu.......Hili halijanipendeza binafsi.

Ndugu yenu,

Mandla.
 
Mambo gani mazuri mpaka sasa ? au kufukuza na kusimamisha watu ?
 
Wana jukwaa,

Naomba kuhoji hapa, hivi ni kweli hawa nduguzangu wa cdm hawaoni harakati na mipango mingi na mizuri inayofanywa na Dr Magufuli na Serikali yake???

Nilitegemea walau msemaji na bavicha kujitokeza hadharani na kumsifu pamoja na kumpa moyo katika harakati zake za kuipeleka Tanzania mbele hasa katika mapinduzi ya viwanda na kutokomeza rushwa pia kuleta usawa nchini. Ila wamekaa kimya tuu.......Hili halijanipendeza binafsi.

Ndugu yenu,

Mandla.


Kwani wewe huoni mazuri meengi yanayosemwa na CHADEMA, au ndio ule mfumo pendwa was makofi kwa kila kitu.
 
Ndg rushwa n sawa na majipu n sawa kutumbuliwa lkn tang mwezi wa 1 hadi sasa maisha n magumu umasikini umeongezeka kwa wananchi na hudum za jamii km afya imekuwa ngumu sana hakuna dawa wala vifaa tiba kwa sasa mahospitalin heri hata awal, Dr JPM aangalie maisha ya wananchi wake kuliko kuwa na kipato kikubwa kinchi lkn wananchi hawanufaiki na kipato hicho, mleta mada changamoto kwako tangu kuingia ww umenufaika kwa magapi?
 
ucha kulia na bado wanajipanga ndani ya wiki lijalo wanaanza kuzunguka tz nzima kuelezea mapungufu ya jpm wenu. toka aingie maisha yamekuwa magumu kupindukia hasahasa kwa wale wa vipato vya chini ndo usiseme.
 
Umefanya busara kutengeneza hiki kibanda vijana wa lumumba wapate pa kujificha maana huko jukwaani kuna jua la hatari.
Anyway, mazuri tumeyaona kama swala la vilaza.
 
hawaoni hao
Hebu nionyeshe hata alilolifanya kwaajili ya taifa hasa kwa mm mtanzania wa chini kabisa yaani kama sukari nanunua sh 6000, hajali wananchi wake anawaita vilaza maisha mitaani ni magumu sasa kwahayo machache sioni la kumsifu zaidi ya kupenda kuonekana kwenye media
 
Nafikiri asiyetambua mazuri ya serikali ya Magufuli atakuwa "kilaza,lofa na mpumbavu". Kimsingi yapo mambo mengi mazuri yaliyofanywa na mheshimiwa tangu aingie Ikulu ya magogoni.

Jambo la kwanza aliloanza nalo ni lile la kuzuia Uhuru wa habari kwa kukataza matangazo ya moja kwa moja ya bunge,tangazo lililotolewa na waziri wake " kilaza" wa Habari.Asichukie nikimwita kilaza kwa Maana kwa mujibu wa Mh.Rais, kilaza ndiyo utambulisho mpya wa Taifa letu kwa wale wote waliopata dv 4 kidato cha nne.

Baada ya kupiga marufuku bunge live zilikuja sarakasi za kupambana na wakwepa kodi ambao kimsingi walikuwa wanafanya vitendo hivyo kwa msaada wa maafisa wa serikali yenyewe ya ccm.Alipoteuwa baraza lake tulishuhudia vikumbo vya ziara za kustukiza za mawaziri wake na fukuzafukuza ya wale wote walioonekana wanafaa kuwa kafara ili serikali yake "I make headlines" za vyombo vya habari nchini.

Likaja suala tete la vipimo vya kiasi cha mafuta kinachoingia nchini(flow meter),hapa ndipo tulipoanza kushuhudia double standard za kiongozi wetu hasa pale alipomfukuza msimamizi wa mita,lakini akamuacha waziri mwenye dhamana aliyekuwa anaongoza utendaji wa meter hiyo kwa SMS.

Kufumba na kufumbua Mh.alilishtua Taifa kwa kusema akiwa Chato kuwa kuna meli kadhaa ziliingia nchini kimyakimya na kushusha shehena ya mizigo na kutokomea kusikojulikana bila kulipa kodi.Tukajiuliza kama meli zenye shehena ya bidhaa zinaingia nchini na kushusha bidhaa kisha kutokomea kusikojulikana huku Taifa letu linamiliki Mitambo ghali kabisa ya Rada tuliyopigwa cha juu na joka la makengeza,usalama wetu kama taifa ukoje?

Hazijapita siku nyingi,likaja sakata la LUGUMI linalogusa familia za vigogo.Hapa tulibahatika kama Taifa kuzifahamu rangi halisi za " Ngariba wetu wa majipu" Namna alivyolishughulikia sakata hili tuligundua kuwa "Ngariba wetu" hatumbui majipu,bali anadili na upele tu ambao unaweza kuondolewa hata kwa kutumia medicated soap kama vile Rungu,Family na nyinginezo.

Ukawa mchana,Ukawa usiku,kiki zilipoanza kupungua,mkubwa akaibuka na bei elekezi ya sukari na kupiga marufuku uagizaji wa sukari toka nje,thubutuuu!!! Sukari liligeuka kaa la moto,hakuna cha bei elekezi wala nini badala yake iligeuka kuwa bidhaa ya anasa kiasi cha kuwafanya hadi baadhi ya watu kusahau hata radha ya sukari.Ili kujinusuru katika aibu ya sukari,zikaanza sarakasi za kuvamia maghala ya wafanyabiashara wetu na kuwasingizia wameficha sukari na serikali sikivu sana ya vilaza wa ccm ikawaaminisha vilaza wa Taifa hili kuwa itataifisha sukari yote na kuigawa bure,masikini ya Mungu...... kwa aibu huku mikono ikiwa nyuma,tukasikia ..... ikiungama hadharani kuwa sukari yote iliyokamatwa kwenye maghala inamilikiwa kihalali hivyo hakuna cha bure,kauli iliyokamilisha maandiko yasemayo"asiyefanya kazi na asile",waliokuwa wamejipanga kupata vya bure wakaumbuka kimtindo.

Kufumba na kufumbua,"The big boss" wa mambo ya ulinzi kwa maelekezo maalumu,aliingia bungeni akiwa amepiga "kitwanga" kadhaa,kisha akashukiwa kama mwewe na kutolewa kafara eti alilewa,wenye akili tulibaini mchezo huo tukakaa kimya.Sasa hivi munene yuko huru na kashfa ya LUGUMI

Punde si punde,Mh.Rais kwa mbwembwe akawagrade watu wake kwa kuwapa madaraja ya vilaza na vipanga na mjadala wa ukilaza bado unaendelea hasa baada ya watoto vilaza wa masikini wa Taifa hili kufukuzwa chuoni kama vibaka,huku kilaza wake akiachwa aendelee na masomo yake pamoja na ukilaza alionao.

Kwa haya machache,Tumepiga hatua kubwa kama Taifa kuelekea Tanzania ya viwanda huku tukishindwa kuzalisha sukari ambayo malighafi yake ni miwa inayolimwa nchini.Kama tatizo letu ni vipaumbele,kwa nini tusiiombe serikali yetu sikivu ya vilaza wa chama cha vilaza waibadili ahadi yao ya kuleta Kilimo cha umwagiliaji wa ubuyu kule Singida,badala yake wamwagilie miwa ilimwe kwa wingi tupate sukari ya kutosha?

CCM hoyeeeeee!!!!!! Kidumu chama cha Mapinduzi,
Mapinduziiiiii..........Daima.Jehcher hoyeeeeeeee.
 
Wana jukwaa,

Naomba kuhoji hapa, hivi ni kweli hawa nduguzangu wa cdm hawaoni harakati na mipango mingi na mizuri inayofanywa na Dr Magufuli na Serikali yake???

Nilitegemea walau msemaji na bavicha kujitokeza hadharani na kumsifu pamoja na kumpa moyo katika harakati zake za kuipeleka Tanzania mbele hasa katika mapinduzi ya viwanda na kutokomeza rushwa pia kuleta usawa nchini. Ila wamekaa kimya tuu.......Hili halijanipendeza binafsi.

Ndugu yenu,

Mandla.
unapenda asifiwe?enhe?
 
Wana jukwaa,

Naomba kuhoji hapa, hivi ni kweli hawa nduguzangu wa cdm hawaoni harakati na mipango mingi na mizuri inayofanywa na Dr Magufuli na Serikali yake???

Nilitegemea walau msemaji na bavicha kujitokeza hadharani na kumsifu pamoja na kumpa moyo katika harakati zake za kuipeleka Tanzania mbele hasa katika mapinduzi ya viwanda na kutokomeza rushwa pia kuleta usawa nchini. Ila wamekaa kimya tuu.......Hili halijanipendeza binafsi.

Ndugu yenu,

Mandla.

Majukumu na Kazi za Upinzani ni nini?
Upinzani ni Kukosoa, Kikubwa hapa ni "Bila Upinzani Imara, Tanzania tusahau Maendeleo Thabiti". Tusiwabeze Upinzani kwa Kiwango Kikubwa. Wana Mchango mkubwa kwenye Ustawi wa Nchi na Taifa.
 
Back
Top Bottom