Nimeamini sisi UKAWA ni wasaka tonge tu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
Habari zenu wanajamii,

Kiukweli mimi nimekuwa nafuatilia sana utendaji wa Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe magufuli, kiukweli anayotekeleza ni kama alikuwemo kweme moyo wangu, anatekeleza yale yote ya ukawa kama ukawa ilikusudia kuyafanya endapo ingechaguliwa.

Cha kushangaza na kinachonikera ni vile baadhi ya viongozi wa ukawa wanavyoponda uwajibikaji huu, inaniuma sana ninapoona kiongozi wa ukawa anasimama hadharani na kupinga utumbuaji, sasa najiuliza hivi ukawa hii inamaana kweli?

Kwanini inapinga? Kwani upinzani ni kupinga maendeleo?. Rais alipomtumbua aliyekuwa mkuu wa mkoa, ndugu -Sumaye, Lowassa n.k walipinga na kusema kwanini wasipewe nafasi wachunguzwe?

Pia juzi Kabwe katumbuliwa napo wamelalamika, sasa je, hivi hawa watu wanataka Rais afanye nini? hawaoni kuwa huo utendaji wa mazoea na uzembe na tume za uchunguzi ndizo zilizotufiksha hapa?

Inanikera sana kwakweli, hata humu, wanaharakati wa mitandao ya kijamii kama Yericko Nyerere naye anaposti hoja za kupingana na utumbuaji, hivi ukawa ingefanikiwa kuingia ikulu kumbe wangefanyaje? Kama mambo yenyewe ndo hivi bora kusiwe na upinzani maana tunachanganyana tu.

Kwa kweli nampongeza sana sana rais huyu mheshimiwa John Pombe Magufuli; na kwa unafiki unaooneshwa na ukawa ni dhahiri hawastahili hata kupewa nchi kwa dakika moja ni wanafiki na wasaka tonge tu.
 
Mh. Magu mjanja sana nafasi za ukuu wa wilaya na nyinginezo za uteuz ameziminya kwanza ili mjikombe weeee mpaka mkimaliza ndo atawachuja. So Ukawa saiv wategemee matusi na kejeli, sababu akili ya mtanzania iko tumboni.
 
wewe si ukawa, usilete unafiki, msaka tonge ni wewe na ccm yako, unajidai kujifanya ukawa....ukawa hatuikubali serikali iliyoko madarakani iliyoingia kusiko halali, hivyo juhud za huyo mfalme unayemtaja hazituhusu..
Kwahiyo wewe unamtambua LOWASSA au? unadhani kwa style hii lowassa angefanya nini, Tusilete ushabiki wa mpira kwenye maisha ya watu, hadi sasa wafanyakazi hewa elfu 7600. bado unapinga unataka ufanyiwe nini? Huyo KABWE kaharibu mbeya akaondolewa, akaharibu MWANZA napo akaondolewa na kuletwa DAR, huku nako kaharibu,,.sasa anatumbuliwa UNALALAMIKA, hivi nchi hii kwani hakuna wengine wa kuwatumikia wanachi? Ukipinga utumbuaji huu basi wewe hujawahi pata huduma katika ofisi za umma ukaona madudu yao.
 
PAMOJA NA MAZURI YA RAISI WETU MPENDWA LAKINI......

KWA NINI WAJIFUNGIE GIZANI?

WAKINA MZEE TOLA MTAKULA MAKONOKONO UCHOYO MBAYA.
 
Hahaha,waskaa Tonge
Ila sema wengi wa mambo haya Wapo Dar,mikoani waliisha sahau wanapiga kazi tu
Maana after 5 yrs wengi humu wazee,so lazima ukubali tu usipokubali tafuta nchi ya kwenda kuishi.
Ukijua neno UPINZANI basi hata hupati shida,maana mpinzani hata ukimuambia baba yake mwanaume atasema hapana,hahaha UKAWA ni sheeda
 
Habari zenu wanajamii;
kiukweli mimi nimekuwa nafatilia sana utendaji wa Rais wetu mpendwa Dr. JOHN POMBE MAGUFULI, kiukweli anayotekeleza ni kama alikuwemo kweme moyo wangu, anatekeleza yale yote ukawa kama ukawa ili kusudia kuyafanya endapo ingechaguliwa, cha kushangaza na Kinachonikera ni vile baadhi ya viongozi wa UKAWA wanavyoponda uwajibikaji huu, Inaniuma sana ninapoona kiongozi wa Ukawa anasimama hadharani na kupinga UTUMBUAJI, sasa najiuliza hivi ukawa hii inamaana kweli? kwanini inapinga? kwani upinzani ni kupinga maendeleo?. Rais alipomtumbua aliyekuwa mkuu wa mkoa, ndugu -SUMAYE,LOWASSA n.k walipinga na kusema kwanini wasipewe nafasi wachunguzwe, pia juzi KABWE katumbuliwa napo wamelalamika, sasa je, hivi hawa watu wanataka RAIS afanye nini?Hawaoni kuwa huo utendaji wa mazoea na uzembe na tume za uchunguzi ndizo zilizotufiksha hapa? inanikera sana kwakweli, hata humu, wanaharakati wa mitandao ya kijamii kama YERICKO NYERERE naye anaposti hoja za kupingana na UTUMBUAJI, hivi ukawa ingefanikiwa kuingia IKULU kumbe wangefanyaje? kama mambo yenyewe ndo hivi bora kusiwe na upinzani maana Tunachanganyana tu.
kwakweli nampongeza sana sana Rais huyu mheshimiwa JOHN POMBE MAGUFULI; na kwa unafiki unaooneshwa na UKAWA ni dhahili hawasitahili hata kupewa nchi kwa dakika moja ni WANAFIKI NA WASAKA TONGE TU.
Uko kama mimi hata ukicheki thread zangu sikuwahi kumfagilia Magufuli uchaguzi uliopita lkn kwa namna anavyochukia rushwa imenipasa niweke pembeni ushabiki wa kisiasa. Naanza kuwaogopa UKAWA.
 
Habari zenu wanajamii;
kiukweli mimi nimekuwa nafatilia sana utendaji wa Rais wetu mpendwa Dr. JOHN POMBE MAGUFULI, kiukweli anayotekeleza ni kama alikuwemo kweme moyo wangu, anatekeleza yale yote ukawa kama ukawa ili kusudia kuyafanya endapo ingechaguliwa, cha kushangaza na Kinachonikera ni vile baadhi ya viongozi wa UKAWA wanavyoponda uwajibikaji huu, Inaniuma sana ninapoona kiongozi wa Ukawa anasimama hadharani na kupinga UTUMBUAJI, sasa najiuliza hivi ukawa hii inamaana kweli? kwanini inapinga? kwani upinzani ni kupinga maendeleo?. Rais alipomtumbua aliyekuwa mkuu wa mkoa, ndugu -SUMAYE,LOWASSA n.k walipinga na kusema kwanini wasipewe nafasi wachunguzwe, pia juzi KABWE katumbuliwa napo wamelalamika, sasa je, hivi hawa watu wanataka RAIS afanye nini?Hawaoni kuwa huo utendaji wa mazoea na uzembe na tume za uchunguzi ndizo zilizotufiksha hapa? inanikera sana kwakweli, hata humu, wanaharakati wa mitandao ya kijamii kama YERICKO NYERERE naye anaposti hoja za kupingana na UTUMBUAJI, hivi ukawa ingefanikiwa kuingia IKULU kumbe wangefanyaje? kama mambo yenyewe ndo hivi bora kusiwe na upinzani maana Tunachanganyana tu.
kwakweli nampongeza sana sana Rais huyu mheshimiwa JOHN POMBE MAGUFULI; na kwa unafiki unaooneshwa na UKAWA ni dhahili hawasitahili hata kupewa nchi kwa dakika moja ni WANAFIKI NA WASAKA TONGE TU.

pombe tuliyokunywa inalewesha balaa mpishi sijui kachanganya na nini? hadi milango ya majumbani tunapotea ikiisha kesho asubuhi tunaenda kutafuta chai ngoma sukari supu na bia hatuwezi mana pesa hakuna wacha tuendelee kunywa kimpumu na komani.
 
wewe si ukawa, usilete unafiki, msaka tonge ni wewe na ccm yako, unajidai kujifanya ukawa....ukawa hatuikubali serikali iliyoko madarakani iliyoingia kusiko halali, hivyo juhud za huyo mfalme unayemtaja hazituhusu..
sasa kama haiwahusu msitoe hayo matamko yenu juu ya utendaji wala kitu chochote kinachotendwa na serikali hii ya jpm mkae kimya,na hata ikiwezekana mtoke bungeni kila siku msiingie kabisa maana mnachojadili ni cha serikali ya JPM
 
Mheshimiwa akifanya mazuri atapewa sifa zake na anapokengeuka vilevile anaelezwa tu..Na hivyo ndivyo mambo yatakavyoenda ishu si kumwondoa Kabwe ishu ni kamuondoaje, Na kwani akifuata utaratiibu wa kisheria lengo lake lisingefikiwa?
 
Utaratibu wa kisheria unaoujua wewe ni upi? Kisa kasema Mtatiro ndiyo umekuwa Utaratibu wa kisheria? Miaka mingi mmelalamika serikali ya ccm ni legelege inakomaa tena mnasema!!!!! Nchi ni yetu tulikokuwa tumefikia na anachofanya JPM ni sahihi kabisa. Na elewa pesa iliyokuwa ikiibiwa ni yako wewe mtanzania pasipo kuchagua chama.
Kuna watumishi wanapokea mishahara hewa ya watu 10. Bila aibu wanatutukana mitaani kumbe ni wezi. Wengine sasa wamepalalaizi na wamelazwa hosp. Hao nao bado una huruma nao. Fuatilia maafisa elimu kitengo cha TSD uwezo wao kimapato na mishahara yao kama vinaendana. Wana wtumishi hewa kibao. Wakitumbuliwa hadharani nao mnalalamika!!! Mbona wao mambo yao walikuwa wakiyafanya hadharani?
TUUNGANE KUIJENGA NCHI YETU
 
Kwa uwezo huo wa kufikiri huwezi kupata hata nafasi ya utendaji wa mtaa, achilia mbali ukuu wa wilaya.
 
Mh. Magu mjanja sana nafasi za ukuu wa wilaya na nyinginezo za uteuz ameziminya kwanza ili mjikombe weeee mpaka mkimaliza ndo atawachuja. So Ukawa saiv wategemee matusi na kejeli, sababu akili ya mtanzania iko tumboni.
Mkuu hivi wewe unadhani magufuli ni mjinga kama Lowasa? Jpm hufanya mambo yake kisayansi wala siyo kijinga kama nyie.
 
We jamaa wewe hujielewi hivi we unahisi kutumbua majipu tu ndio tumpe sifa hapa kazi bado hajaanza
 
Back
Top Bottom