Nimeamini mapenzi yanaua

Hatuna tofauti we umeacha mahali ila nami ilikuwa ni mtu ambaye tushatambulishana pande zote na kama mipango ingekwenda sawa ilikuwa tufunge ndoa mwishoni mwa mwaka huu but kisicho ridhiki hakiliki.

Nimekuzidi hahaha mpaka unatoa mahari unajua process zote tayari ama.
Ila nini jikaze mama.

karibu tuuguzane kwa maneno tu.
 
Hongera kwa kuamua maamuzi mazuri japo ni magumu! Usirudi nyuma ni marufuku kuirudia Jana yenye maumivu jikaze utaifikia kesho kutwa yenye nafuu japo ni mbali mno,mshirikishe M/Mungu Fanya ibada zaidi na muombe M/Mungu akujaalie moyo wa Imani
 
Tatizo lako ni kumuamini mtu baada ya kosa la kwanza, unapoumizwa kwenye mahusiano na mtu endapo ikatokea ukarudiana nae basi inabidi uwe makini saaaana. Usimpende kama ulimvyompenda mara ya kwanza, narudia tena kuwa makini saaaana urudianapo na mtu.
 
Inawezekana kweli ila ni bora angeniambia mapema kuliko mda alionipotezea na aibu alonitia kama alijua hilo alinipeleka kwa wazazi wake kufanya nini alikuja na kwa wazazi wangu kufanya nini.
Mkuu kuna wakati unaweza kumpeleka mwanamke kwenu kisa wazazi kama sio wazazi huyo mpenzi wako anataka ajulikane kwa ndugu zangu na hii hutokea kipindi mwanamke anatamani kuwa kwenye ndoa na mwanaume anatafuta pa kumpumzikia

Hutakiwi kukata tamaa kama ulipo fikia leo

Huwa tunasema nilipo kosea ndio nilipo jua njia vizuri na kujua kutumia niliyo jifunza

Hapo unatakiwa uchukue utulivu wa kutosha

Na hili chukulia kama changamoto ya kawaida

Kuna watu wanatolewa mahari na tarehe ya ndoa inapangwa na mambo yanaenda sivyo ndivyo

Hapo shukuru mungu kakunusuru na mengi mbele ya safari
 
Hongera kwa kuamua maamuzi mazuri japo ni magumu! Usirudi nyuma ni marufuku kuirudia Jana yenye maumivu jikaze utaifikia kesho kutwa yenye nafuu japo ni mbali mno,mshirikishe M/Mungu Fanya ibada zaidi na muombe M/Mungu akujaalie moyo wa Imani
Ahsante my dear.
 
Sikuja hapa kutafuta mwanaume ila kupunguza maumivu yangu.Na ndo mana hata PM yangu nimefunga sababu nililihisi hili maana wengine katika maumivu ya wengine huwa mnaona ndo sehemu ya kuongezea maumivu.
Basi nikutake radhi bibie..
 
ahsante nami naamini hilo pia kuna mengi naepushwa japo moyo ni mgumu kukubali.
 
Tatizo lako ni kumuamini mtu baada ya kosa la kwanza, unapoumizwa kwenye mahusiano na mtu endapo ikatokea ukarudiana nae basi inabidi uwe makini saaaana. Usimpende kama ulimvyompenda mara ya kwanza, narudia tena kuwa makini saaaana urudianapo na mtu.
Ahsante nami naamini hilo ndo kosa kuu nililofanya kuna wakati inafika mpaka nalaani siku niliyokutana naye.
 
Pole,pia usisahau wapo me waliojiapiza kuwa hawatowaamini viumbe aina ya ke.
 
Wamekufa wengi tu.....Romeo and Juliet
 
ahsante nami naamini hilo pia kuna mengi naepushwa japo moyo ni mgumu kukubali.
Kubali kuumia Mara moja ili mbele uwe na maisha ya furaha

Binadamu tunapitia mengi yapo ya kuumiza yapo ya kufurahisha pia

Mwanaume mmoja hawezi kubeba dhamana ya wanaume wote

Mwanamke mmoja hawezi kubeba dhamana ya wanawake wote

Baaada ya akili yako kutulia utampa mtu utake sema ulikuwa wapi

Kukubali kushindwa sio dhambi

Dhambi ni kung'ang'ania usivyo viweza
 
hayo yote umeyataka kwanini? ukafumanie?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…