Nimeamini mapenzi yanaua

Ulimfumania kwani mumeo?
Sio mume wangu ila mtu ambaye tushatambulishana pande zote na mpaka kwa wachungaji kanisani na mahari ilikuwa iletwe mwezi wa saba lakini katika yote bado sawa nakubali sistahili kujipa uhalali wa umiliki.
 
Kila kitu kinatokea kwa sababu na mshukuru Mungu kwa yote na songa mbele maana kuna maisha baada ya kutendwa
 
Hichi kimenitokea siku si nyingi yani nimemfumania live na hii si mara moja japo nishafumania mara nyingi lakini aliomba msamaha na maisha yakasonga. Lakini hii ya juzi kali badala ya kuomba msamaha kaishia kuniambia kama nimemchoka nimuache atapata wengine.

Dah eeh Mungu nisaidie nipite salama katika hili japo nishaamua ni no turning back tena ila maumivu nayopata ni Mungu tu anajua.But sitakuja kumuamini kiumbe anayeitwa mwanaume chini ya jua maana many of them wako na roho za kisatanic.
Pole dada kwa yaliyokukuta. Hiyo ni mitihani tu yakimaisha. Binafsi nilishapitia majarib kama ya kwako, niliumia sana mpaka leo majeraha hayaja pona.

Lakin pamoja na maumiv yote, siku chagua kuzin na kila dem anaekatiza pembeni yangu, sikuchagua kuwaona wanawake wote kuwa ni malaya.. kwamba sito waamini..

Bali nilirekebisha mapungufu yangu na kuwa makini ktk kutafuta mwenzi..
Ucjiapize kuwa hutakuja kumuamini mwanaume, maana kiapo kinaandikwa kwenye ulimwengu wa roho, ina maana hata siku akija yule ambae Mungu alipanga, uta mreject sababu ya mmoja alie kusaliti.

Kuwa makini dada, si wanaume wote wana roho mbaya, wapo wanaume faithful , linda moyo wako , ila mwombe Mungu akupe aliepanga.
 
Inawezekana but what I beleive ni kuwa kila jambo na wakati wake sitalia daima.
Rosalie Mungu alikuletea ujumbe tangia mwanzoni lakin hukutaka kusikiliza.
Ulivyo salitiwa mara ya kwanza ..pale pale ungemwacha. Hili la kujifanya unapenda moaka mtu ambae amekusaliti matokeo yake ndio haya.

Uliziona dalili lakin ukapuuzia, haya ndio matokeo yake.
 
Kwani hakuna wanawake wenye tabia hizo za kucheat? Iweje useme "wanaume most of them wana roho za kisatanic?"

Kabla ya kulaumu wanaume jaribu kujitafakari,nini kimepungua kwako mpaka huyo jamaa yako akucheat?

Tatizo ni nini mpaka akucheat? Kuna kitu anakosa kwako ndio maana kaenda kukitafuta kwa mwingine na ulitakiwa ulitambua hilo toka ulivyomkamata akikucheat mwanzoni kabisa.
Kiukweli kuna watu wengine ukimuuliza kwanini umemuacha yule utakuta hana sababu kabisa.
Ni tabia tu na maamuzi yake baasi
 
Tatizo lako ni kumuamini mtu baada ya kosa la kwanza, unapoumizwa kwenye mahusiano na mtu endapo ikatokea ukarudiana nae basi inabidi uwe makini saaaana. Usimpende kama ulimvyompenda mara ya kwanza, narudia tena kuwa makini saaaana urudianapo na mtu.
Always, nina theory moja kwamba mpenz wako aki ku cheat mara ya kwanza. Ukamsamehe, ukampenda tena. Atakucheat mara ya pili na ya tatu, ni suala la muda tu.
 
Wewe ndiye mwenye makosa ulitoa papachu pasipo hata kulazimishwa ukitegemea nini. Hicho ni kilio cha kujitakia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom