VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Ninazo habari nyingi nyeti za kimatokeo. Lakini, naheshimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hivyo kuiachia kazi yake hiyo ya kikatiba na kisheria. Kazi ya kutangaza matokeo. Kwa sura niionayo, CCM iko njiani kuondoka madarakani.
Madaraka hunoga pale ambapo kuna udhibiti wa kutosha wa mihimili miwili ya dola: Serikali na Bunge. Pia, madaraka hunoga pale ambapo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani zinatawaliwa na chama kimoja: CCM. Mwaka huu jambo hilo haliwezekani.
Tayari,kuna Manispaa, Miji, na Miji Midogo imeshaangukia mikononi mwa wapinzani. Inakuwa chini ya utawala wa vyama vya upinzani. CCM inapoteza ladha ya kuitawala Tanzania kwa mapana yake. yaweza kupata hili na lile lakini itakosa yale.
Mwaka huu nimeamini na kujionea jinsi chama kinavyozaliwa,kukua na kuelekea kufa. Nayasema haya kwa uchungu mkubwa ingawa ndio ukweli wenyewe. Nasema tena kuwa CCM inapoteza kwa kasi itiayo wasiwasi utawala wake hapa Tanzania.
Kama chama, tutafurahia kitakachopatikana lakini tutapaswa kujitazama upya na kujirekebisha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam