Nimeachana nae pasipo kumwumiza

Nimeachana nae pasipo kumwumiza

Mlanje

Senior Member
Joined
May 16, 2013
Posts
141
Reaction score
77
Ndugu wana jamii natumaini mnaendelea vyema. Mimi ni mwanaume niliyetokea kupendwa sana na wanawake wawili ila mmoja sikuwa nampenda sana ingawa yeye alinipenda mno.

Kutokana na hilo nilimkatalia kwa nyakati tofauti kufanya mapenzi kabla sijaoa na alikuwa tayari kusubiri. Hivi karibuni alianza kunitambulisha kwa rafiki zake na ofisini kwao na alionyesha upendo wa hali ya juu kiasi cha kulia sana nisipopokea simu yake hasa usiku.

Ila nilijihadhari kumwambia kuwa simhitaji maana angeumia sana hivyo niliamua kumwomba Mungu ampe mtu atakaye mpenda na mimi nipate yule nitakaye mpenda. Siku moja baada ya maombi yule dada aliacha kabisa kupokea simu zangu na nimemtafuta mara nyingi hapokei wala kujibu meseji zangu hivyo yeye ameamini kuniacha ila kimsingi mimi ndio nimemwacha.

Pia sasa hivi nimeamua kuendelea na huyu mwingine ambaye pia ananipenda sana. Ushauri kwa vijana wenzangu tusifanye zinaa ni dhambi na pia utaumia zaidi ukiachana na mtu ambaye umefanya nae ngono maana nafsi yako inakuwa imeungana nae.

Hata huyu wa sasa sifanyi nae ngono mpaka nioe na hata akitaka kuniacha siwezi kuumia sana maana sijaunganishwa nae tumia maombi kumwacha mtu. Pia Mungu awasaidie kushinda zinaa na kupata wake na waume wema barikiweni sana pia samahani kwa maandishi mengi.
 
haleluya muujiza umetendeka, japo katika uhalisij ni ngumu kuamini
 
Uyo wa sasa haufanyi nae ngono wajanja wanakusaidia....

Ila sio mbaya kuchapiwa cr ya ndan
 
Mi nadhani wewe ndio uliachwa. Maana kwa mtazamo wangu kwa kuwa ulikuwa hujampenda, kitendo cha kutokukupigia kwako kingekuwa faraja na usingehangaika kumpigia kila mara. Kuwa mkweli,
 
Mi nadhani wewe ndio uliachwa. Maana kwa mtazamo wangu kwa kuwa ulikuwa hujampenda, kitendo cha kutokukupigia kwako kingekuwa faraja na usingehangaika kumpigia kila mara. Kuwa mkweli,
Hapana kumpigia simaanishi namhitaji kimapenzi nilitaka kujiridhisha tu kama kweli ameamua kwa sasa mimi nina mtu mwingine
 
Ni kweli siwezi kufanya mzaha kwa Mungu hata mimi kwa kweli nimeshangaa sana


.kipi kigumu kuamini hapo? Kuwa mtu hawezi kuishi bila kujihusisha na ngono??
 
Safi sana bro. Sema watu ni kuendekeza ngono tu. Mbona kipindi cha nyuma watu ilikuwa hakuna ruhusa kula tunda kabla ya ndoa na iliwezekana? Ukidhamiria inawezekana sema sasa watu wanajifanya wako westernized!!!!! Dhambi na westernization mhhhhh!!!
 
Inawezekana? Just kuomba?

Imani yangu changa sana
 
Back
Top Bottom