Nimeachana na mke wangu

Nimeachana na mke wangu

Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi,

Shukrani wakuu.
Pole sana wanawake wengine ni zigo la m.avi au gunia la chunvi. Tunaoa ili tuishi kwa amani sio magonvi. Hatua nzuri umechukua
 
Mimba imekua kama sehemu ya kujiendekezea ili kutimiza mambo ambayo wazazi hawajakufanyia kwenu eti homoni

Homoni gani bwanaa homoni zina react mwilini sio zinatuma udongo sijui pweza...
Mimba imekua kama sehemu ya kujiendekezea ili kutimiza mambo ambayo wazazi hawajakufanyia kwenu eti homoni

Homoni gani bwanaa homoni zina react mwilini sio zinatuma udongo sijui pweza...
Ngoja waje watakuambia hujawah pata mimba
 
Icho n kipindi cha mpito.... Wengi tumeyapitia hayo.... jitahidi kua Mwanaume Acha uvulana.... mpe nafasi kubwa ya yeye kuongea anataka uweje, kuliko wewe unavotaka aweje. Inasumbua lkn inavumilika.

Zaidi Hongera sana kutokuficha swala lako, Kama hakuna kingine ulichoficha juu ya Chanzo cha mgogoro. Hope mgogoro wenu umekwisha kupitia ushauri uliopewa ktk hili jukwaa, kila la kheri
 
Epuka kufanya maamuzi ukiwa na hasira wengi hujutia sana hilo

Tafuta watu wazima kama wazazi au viongozi wa kidini mkae na mkeo msuluhishe hilo tatizo achana na huyo dada mtu

Jaribu kuongea na wakuu wako kazini ikiwezekana wakupe likizo fupi waambie hali halisi kwamba lengo lako ni kunusuru ndoa yako.

Cha muhimu pambana kuinusuru ndoa yako. Huyo dogo atakayezaliwa anahitaji sana malezi na upendo wa baba na mama yake

Daah sawa mkuu nimekuelewa shukrani
 
Basi kama ni hivyo unatakiwa upime, kama ugomvi wenu wakati hajabeba mimba ulikuwa wa kawaida badi mvumilie tu atarudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kujifungua!

Sawa mkuu
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
Una umri gani?,si umesema mkeo ni mjamzito?,wenye ujauzito ndio changamoto zao,akihljifungua atatulia
 
Kijana kaa chini na watu wazima watakuelekeza haya mambo. Najua unapitia changamoto ambazo hujawahi kufikiri kukutana nazo. Enzi za zamani kuepusha haya mwanamke akipata ujauzito alikuwa anapelekwa kwa wazazi wake kuepusha shari kama hizi.

Ujauzito ni kipengele ndugu yangu kuwa mdogo na mvumilie mkeo katika shida aliyonayo. Ukisema unamwacha unakosea sana kwani kipindi hiki ndio ulitakiwa uonyeshe kujali sana na kuwa karibu nae

Tatizo wanaume hatuandaliwi katika maisha ya ndoa na changamoto zake. Siku ya kuona unatoa tu mahari na kwenda kuchukua mke imeisha hiyo. Hufundishwi jinsi ya kuishi na mwanamke, kuishi na mke mwenye ujauzito, hata mtoto akizaliwa hatujui tufanyeje. Mambo haya yalikuwa yanafundishwa jandoni

Mke huyo bado hamjaachana sema tu wewe na utoto wako umeamua kususa kitu ambacho kinadhalilisha sana uanaume wako kwa kumkimbia mke kipindi ambacho ni mjamzito na anataraji kukuletea kiumbe. Ni baba wa aina gani ndugu yangu

Nimesikitishwa sana na hii mada ila ndio hivyo tunafundishana kupitia ujinga wa wengine. Nachoweza ku-conlude ni kwamba Taifa lina watu wa ovyo sana

Sawa mkuu nimekuelewa shukrani
 
Wengi watasema ni hangover ya mimba lakini umewah jiuliza house girl akipata mimba huo mvurugiko mbona huwa haupo? Mdogo wangu akipata mimba akiwa kwangu Wala sikugundua na alijitahidi kufichaa hakuna kuchagua chakula au kudeka kama hivyo, nikagundua kumbe wanafanyaga makusudi kupima upepo, kuanza hapo nikasema make wangu haji kuniletea hivyo vitimbwili, akijizima data inakula kwake

 
Mwanamke ni watu watatu tofauti katika mwili mmoja!!
1: Akiwa hivi kawaida.
2: Akiwa mwezini.
3: Akiwa Mjamzito!

Jitahidi Sana kumuelewa mwenzio unayeishi nae!

Sawa mkuu
 
We ushapata mwanamke huko dodima..huna lolote.....hukutakiwa kumuacha bali ulitakiwa ukae na mbali kwa muda..mifupu mimba yke imekuchukia....
Unakua km mgen wa mambo bwana..mimba kitu kingine....
Hapo wala hajui analofanya..subiri ajifungue uone

Umeshindwa jiuliza why now....
Very disappointing

Wanaume mpeni somo huyu mtoto wa kiume...
Kuna sababu za kuachana ila si hiii

Nenda kasome ht google hormonal changes during pregnancy...

Sawa Mkewangu shukrani
 
Kama hakuwa hivyo kabla basi ni mimba inamsumbua. Ungesubiri kwanza ajifungue ndo ufanye maamuzi. Pole lakini...

Sawa madam sio mbaya lakin everything it’s gonne be okay
 
Back
Top Bottom