Nimeachana na mke wangu

Mwanamke ni watu watatu tofauti katika mwili mmoja!!
1: Akiwa hivi kawaida.
2: Akiwa mwezini.
3: Akiwa Mjamzito!

Jitahidi Sana kumuelewa mwenzio unayeishi nae!
 
unaonekana ww bado ni mtoto wanawake wakiwa na Mimba wana vitabia vya ajabu vinavyokuja automatic fikiria je kabla hajabeba Mimba alikua hivyo? je ukimuacha itamsaidia mtoto wako ajaye? uliza sisi tuliowahi kuambiwa tunanuka tukiingia ndani ya nyumba kuna kaharufu ka uvundo kanachafua nyumba tena hapo ni nyumba unayolipia kodi ww na kila kitu ni chako alaf cha ajab ukichelewa kurudi unaaambiwa upo kwa malaya wako!

Nilishawahi kufukungiwa nje kwakua tu sijanunua kitimoto cha kuchoma kama alivyotaka nlinunua rojo!

Nlisha wahi kuliliwa kwa kumnyanyasa eti simjali na nachelewa kurud nakaa na mlaya zangu

Biblia imendika ishini na wanawake kwa akili

Daah sasa nimekuelewa mkuu
 
Tunza mkeo
Hizo mambo ni shauri ya preg ni za muda! Huwezi muacha akiwa ktk hali hiyo!
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
Izo ni hali za mimba .kuwa mvumilivu akijifungua zitaisha pengine amekubebea dume ndomana mnakwazana
 
Asantee mkuu
Yeah nikweli mkuu nampenda wife ila acha iwe tu hayo maisha siwez moyo umeshagoma
Kuhusu shemeji haiwez kutokea mkuu

We ushapata mwanamke huko dodima huna lolote, hukutakiwa kumuacha bali ulitakiwa ukae na mbali kwa muda mifupu mimba yke imekuchukia.

Unakua km mgen wa mambo bwana, mimba kitu kingine. Hapo wala hajui analofanya, subiri ajifungue uone

Umeshindwa jiuliza why now....
Very disappointing

Wanaume mpeni somo huyu mtoto wa kiume. Kuna sababu za kuachana ila si hiii. Nenda kasome ht google hormonal changes during pregnancy.
 
Kama hakuwa hivyo kabla basi ni mimba inamsumbua. Ungesubiri kwanza ajifungue ndo ufanye maamuzi. Pole lakini...
 
Itakua ni huo ujauzito tu Mkuu Vipi Kabla hajabeba mimba pia alikua mgomvi???
 
Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili
Wewe na huyo dadaake mna umri gani?
Seems wote hamjui kuwa kwa baadhi ya wajawazito hiyo ni kawaida, so siyo kosa lake, na akijifungua atakuwa kawaida kama mwanzo
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
Pole sana mkuu ,

Nikuulize kwanza hiyo Hali ya ugomvi ilikuwepo kabla ya ujauzito au ni baada ya ujauzito ,

Kama ni baada ya ujauzito ,basi hayo yatakuwa yanasabibishwa na hiyo Hali ,
Wakiwa wajawazito hua wanakua na changamoto nyingi sana aisee Cha msingi subiri ajifungue mambo yatakuwa sawa mkuu
Nikushauri tu usichukue maamuzi magumu kipindi hiki subiri ajifungue
 
Yani mkuu ukikua mtu mzima ni pamoja na kukabiliana na mambo kama hayo. Tuwaone huruma wake zetu sometimes homoni zinawazidi akili zao za ku reasoning
 
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, mtoto wako anahitaji malezi yako sana mkiwa pamoja na mke wako.
 
fanya ufanyavyo mkuu, usimuache mkeo hasahasa kipindi ambacho ni mjamzito.

Inawezekana sijui sababu kubwa ya kwanini mnagombana sana, ila kipindi cha ujauzito ni kipindi cha uumbaji wa pili wa mtoto. huzuni yeyote au shurba yoyote inayompata mama mjamzito au anachopitia mtoto tumboni naye anahisi na anaumbika kutokana na mazingira ya nje.

Jifanye mpumbavu, for once. kuwa positive. muulize mama unataka nifanye nini au niweje na SIO umuulize kuna tatizo gani. jinsi unavyoliangalia tatizo ndio utajua hili linatatulika au halitatuliki.

Mi huwa naamini mpaka mmeoana, kuna mahali mnaafikiana. basi hapo ndo pawe nguzo ya maelewano yenu. this life is damn short. make it worthwhile.
 
Kuepuka shari huwa wanawapeleka makwao wakajifungulie huko.

Na huyo mkeo huenda kutokua ka kazi ya kufanya ndo kunampa hicho kisirani, anatamani mda wote apate kampani yako kitu ambacho ni kigumu kwako.

Na wewe tabia zako ni kama zake tu, huwezi kusuluhisha migogoro badala yake na wewe unapanick badala ya kumfanya atulie .
Na mwisho kabisa umeamua kususa kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Unamhukumu bure huyo mwanamke hana dhida akijifungua atakaa sawa tu mvumilie sana kipindi ana ujauzito, endapo utamtesa basi mtoto atakayezaliwa haya yanawezekana.
1. Atakuchukia sana wewe baba yake
2. Ana uwezo akawa shoga sababu ya huzuni za mama akiwa mjamzito

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom