Nimeachana na mke wangu

Nimeachana na mke wangu

Wewe na huyo dadaake mna umri gani?
Seems wote hamjui kuwa kwa baadhi ya wajawazito hiyo ni kawaida, so siyo kosa lake, na akijifungua atakuwa kawaida kama mwanzo

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Pole sana mkuu ,

Nikuulize kwanza hiyo Hali ya ugomvi ilikuwepo kabla ya ujauzito au ni baada ya ujauzito ,

Kama ni baada ya ujauzito ,basi hayo yatakuwa yanasabibishwa na hiyo Hali ,
Wakiwa wajawazito hua wanakua na changamoto nyingi sana aisee Cha msingi subiri ajifungue mambo yatakuwa sawa mkuu
Nikushauri tu usichukue maamuzi magumu kipindi hiki subiri ajifungue

Sawa mkuu nimekuelewa nntafanyia kazi hilo
 
Yani mkuu ukikua mtu mzima ni pamoja na kukabiliana na mambo kama hayo. Tuwaone huruma wake zetu sometimes homoni zinawazidi akili zao za ku reasoning

Nikweli mkuu upo sahihi
 
fanya ufanyavyo mkuu, usimuache mkeo hasahasa kipindi ambacho ni mjamzito. inawezekana sijui sababu kubwa ya kwanini mnagombana sana, ila kipindi cha ujauzito ni kipindi cha uumbaji wa pili wa mtoto. huzuni yeyote au shurba yoyote inayompata mama mjamzito au anachopitia mtoto tumboni naye anahisi na anaumbika kutokana na mazingira ya nje. jifanye mpumbavu, for once. kuwa positive. muulize mama unataka nifanye nini au niweje na SIO umuulize kuna tatizo gani. jinsi unavyoliangalia tatizo ndio utajua hili linatatulika au halitatuliki.
mi huwa naamini mpaka mmeoana, kuna mahali mnaafikiana. basi hapo ndo pawe nguzo ya maelewano yenu. this life is damn short. make it worthwhile.

Nimekuelewa mkuu shukrani sana
 
Kuepuka shari huwa wanawapeleka makwao wakajifungulie huko.

Na huyo mkeo huenda kutokua ka kazi ya kufanya ndo kunampa hicho kisirani, anatamani mda wote apate kampani yako kitu ambacho ni kigumu kwako.

Na wewe tabia zako ni kama zake tu, huwezi kusuluhisha migogoro badala yake na wewe unapanick badala ya kumfanya atulie .
Na mwisho kabisa umeamua kususa kabisa.

Daah sawa mkuu
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.

Mke kama huyo una mpuuza, ndoa itakuwa changa, vumilia akianza majukumu ya mtoto atatulia.

Hivi mtu akikupigia simu kwenye kikao, uka text upo busy, akileta ugomvi wa text unaumia wapi? Kwani kaja kwenye kikao?

Huyo anajua tu uzaifu wako na anakuonea, akijifungua atatulia, sikiliza waliokutangulia, acha kutangaza matangazo ya kuacha mke.
 
Basi usimuache mkeo kwani kinachomfanya awe hivyo ni wivu tu na hiyo mimba inampa kisirani kwani anahisi kwamba wakati yupo kwenye situation hiyo pengine wewe upo na side chicks na hivyo upo mbali ndo kabisa unampa wakati mgumu maana kila muda anakuwazia wewe tu.... Usimuache mwanamke kwa sababu mnagombana tena kwa sababu za wivu tu, bali muache kama ni muasherati.... Kuwa proud na wivu anaokuonea mkeo maana siku wivu ukimuondoka hutompata tena.

Sawa mkuu ubarikiwe sana nimekuelewa kiongoz
 
....Mbona Umeamua Vizuri TU? Ushauri Gani na wa Nini Tena Unataka?
Ulioa upate Mtu wa kukuliwaza Ukiwa na Mawazo.
Sasa inapotokea uliemchagua ndio anakusababishia Mawazo zaidi, wa nini Tena huyo?
Ndio maana nikasema Umeamua Vizuri kujtenga mbali naye. Move on. Utaumia kiasi lakini Utazoea TU.... Na utakuwa na AMANI...!

Sawa Mkewangu shukrani
 
Aisee mkuu usichukulie hasira sana juu ya Jambo hili.

Tuliza Ball tu, Mambo yatajipa na kurudi kama ilivyo awali pindi akijifungua.
 
Pole Mkuu!!!
Kama fujo zote zimekuja baada ya kuwa mjamzito, ndiyo chanzo cha magomvi yote unayoyaona na si vinginevyo... Na kinyume chake ndiyo ukweli...

"Uzoefu ni mwalimu mzuri"...
 
USIMWACHE HATA KIDOGO !!

Wewe bado hujapata maarifa ya kuishi na mwanamke. Ukiona mwanamke ni mja mzito halafu ana ugomvi hivyo, jua tu ni HIYO MIMBA INAMSUMBUA !! Hujuilizi ni kwa nini baadhi ya wanawake waja wazito wana hamu kubwa kula udongo? Lakini akishajifungua hamu inaisha !!

Wacha nikwambie. Huyu wa kwako sio anakuchukia. Ni hiyo mimba tu ! Kuna mwingine akiwa mja mzito ANAKUPENDA KUPITA KIASI - yaani inafikia hataki utoke uende kazini!! Anakuwa KERO ! Lakini mwanaume mwenye akili unamchukilia tu kama mtoto uliyemnyima pipi halafu anakuwa na hasira mbaya hadi eti kutaka kukupiga!!

Nakushauri tena !! Usimwache. Ugomvi wake kwako unasababishwa na ukweli kwamba ANAKUPENDA SANA !! Anaona WIVU MKALI kwa vile anajua ni mja mzito na huwezi "kupiga mechi ya kiuhakika na yeye", hivyo anaamini kama uko mbali lazima unabanjua "samsing" ya pembeni !!

Zaidi ya hapo, wewe mwenyewe unampenda sana mkeo!!I MIMI SIKUJUI lakini DONT EVER MAKE THE MISTAKE OF LEAVING HER !!

Wanawake wote ni "kiungulia" tu. Kamwe hutakaa umpate ambaye hana mambo ya ajabu. Ukimwacha huyu unaweza ukampata unayedhani ni mpole kumbe ni malaya wa kutupwa! Au mwingine anataka umnunulie kila nguo inayokuja mpya, kila kitenge, kila kanga, na ukimwambia pesa hakuna anakununia na hata kufikia kukunyima "haki yako"

Mwingine atakugombanisha na ndugu na marafiki na hata wafanyakazi wenzako au wateja.

BAKI NA HUYO ! Waswahili husema:-
"Awali ni awali tu hata ikiwa ngada" (karata)

Shukrani mkuu nimekuelewa ubarikiwe sana wacha niongee nae nimuwekesawa maisha yaendelee
 
Sikatai ups and downs zipo kwenye ndoa lakini baada ya kuwa mjamzito ugomvi umezidi kuliko kawaida
Hiyo ni hali ya ujauzito tu uwe mwelewa, labda kama ulikua na plan zako tu za kumtelekeza.
 
ni mimba tu inamsumbua. vumilia, akijifungua utaona ajabu. utapata penzi la uhakika na hatotaka mtoto akae mbali nae. acha utoto, vumilia tu
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
Acha iwe hivyo
 
Umechemka sana.
Hiyo issue ilikuwa ndogo sana. Rudi kwa mkewe acha utoto.
 
Kusema kweli hili mi binafsi japo wanawake wenzangu watanipopoa ila tuseme tu ukweli.
Mbonq kama mimba zinatofautiana kulingana na status ya mtu????? Maana kuna watu wa matabaka flani wakiwaga na mimba hujui Wadada wa kazi, mtu ambae bwana kaikataa mimba au hana hela unakua zako normal tu!
Ila hawa zake za wenyewe hawa eeeeweh!!!! Ni hatari niko hapa na mke wa mtu naishi nae ananinyanyasa kama hakai kwangu kwanza unamfulia, anajifanya akivaa nguo dakika 0 imechafuka, mara unanuka mara niketee sijui upupu gani!!! Hapo hajaanza kulalamika oooh mimba kazi ooooh mimba fyoko yani mambo ya hovyo tu

Kusema kweli mi Mleta mada namuelewa sana! Hapa msijifanye mnajua sana kuishi na mimba ila hawa so called Wifes wenye mimba wanakera mno MNOOOOO! hata mimi ningeondoka manake maisha yenyewe ya saivi ni mimba tosha bado na mmama wa mtu akuvuruge aaah
Braza ajichimbie uko akijifungua akamwone amuulize kaacha utoto ?? Kama kaaacha waendelee na maisha.

Plz Tuonane PM Miss
 
Back
Top Bottom