Nimeachana na mke wangu

Nimeachana na mke wangu

Hizo mimba ni kisingizio tu hamna kitu hapo, yaanii mimba haiwezi sababisha mtunga mimba akachukiwa, unaweza Kuta hata mimba sio ya jamaa

Mmh
 
Icho n kipindi cha mpito.... Wengi tumeyapitia hayo.... jitahidi kua Mwanaume Acha uvulana.... mpe nafasi kubwa ya yeye kuongea anataka uweje, kuliko wewe unavotaka aweje...... Inasumbua lkn inavumilika.... Zaid Hongera sana kutokuficha swala lako, Kama hakuna kingine ulichoficha juu ya Chanzo cha mgogoro.... Hope mgogoro wenu umekwisha kupitia ushauri uliopewa ktk hili jukwaa... kila la kheri

Sawa mkuu
 
Mke kama huyo una mpuuza, ndoa itakuwa changa, vumilia akianza majukumu ya mtoto atatulia.

Hivi mtu akikupigia simu kwenye kikao, uka text upo busy, akileta ugomvi wa text unaumia wapi? Kwani kaja kwenye kikao?

Huyo anajua tu uzaifu wako na anakuonea, akijifungua atatulia, sikiliza waliokutangulia, acha kutangaza matangazo ya kuacha mke.

Sawa mkuu
 
Sawa mkuu

Hemu usimtelekeze mtoto wa watu, nenda naye taratibu mpaka ajifungue, mtakuwa sawa, tumepita unapopita na tuli fanya makosa, hemu jishushe na mbebe binti yetu kwenye hili.
 
Pole Mkuu!!!
Kama fujo zote zimekuja baada ya kuwa mjamzito, ndiyo chanzo cha magomvi yote unayoyaona na si vinginevyo... Na kinyume chake ndiyo ukweli...

"Uzoefu ni mwalimu mzuri"...

Asantee mkuu
Shukrani sana mkuu
 
Hiyo ni hali ya ujauzito tu uwe mwelewa, labda kama ulikua na plan zako tu za kumtelekeza.

Hapana sijawah kufikilia kumterekeza mkewangu
 
Hemu usimtelekeze mtoto wa watu, nenda naye taratibu mpaka ajifungue, mtakuwa sawa, tumepita unapopita na tuli fanya makosa, hemu jishushe na mbebe binti yetu kwenye hili.

Sijamtelekeza mkuu kama ningemtelekeza bas nisinge endelea kumjali mkewangu
 
Wanawake wakiwa kwenye kipindi cha ujauzito wanasumbua sana uamuzi wako ni mzuri wengine huwa wanawarudishaga nyumbani kwao mpaka watakapo jifungua.
 
Sijamtelekeza mkuu kama ningemtelekeza bas nisinge endelea kumjali mkewangu

Kumjali sio kumpa Dada yake hela, Kumjali ni kuchukuliana na Hali yake na kuwa karibu na yeye
 
Umefanya maamuzi ya kiume,lakini!, inaonekana una tabia za kike,huo muda wa kujibishana na mwanamke unapata wap?,si umuache aongeee akichoka atanyamaza
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
Wakati mwingine kama huo ugomvi umeanza baada ya kupata ujauzito basi ujue kuwa sababu ya chuki hiyo kwako ni ujauzito wake

Huwa inatokea hasa mtoto anapokuwa wa kiume hutokea mama kumchukia mume na changamoto zinazofanana
Hivyo kumuacha akiwa na ujauzito wako kwa sasa sio sahihi.
 
Back
Top Bottom