Nimeachana na mke wangu

knows

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,403
2,006
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.
 
Piga mashine Bob....,pendelea kula Nyanya chungu mbichi saa Moja kabla ya show....au bamia mbichi kama utaweza na limau..... Utakuja nishukuru hapa,...Hicho ni kiherehere kinamsumbua...na kinatokana na wewe kutomfikisha kileleni.

Sema nini jombaaa.sio kesi...kama vipi we mwache wahuni tumshone tukuambukize mi yutiai sugu .....
Haina maana tena mkuu tushaachana
 
Back
Top Bottom