We jiulize kwa kutumia mifano hii.
1.a) Kwanini ukitaka kufanya harusi watu wana changia sana?
b)Kwanini ukitokea msiba,hata utake kwenda kuzikwa INDIA watu wata changa na utaenda.
2. a) Kwanini ukitaka kwenda shule ukaomba mchango hakuna wa kukupa?
b)Kwanini ukiwa unaumwa,hata daktari hakutibu pasipo kutoa hela kwanza,wala ndugu hawatoi hela,lakini ukifa hata daktari anaweza kukusafirisha hadi kwenu ukazikwe?
Harusi ni sehemu za kudanganyana kwamba tuna pendana,ila ukweli wake utaupata kwenye mazishi,HATUPENDANI.
Wengi wanaokimbia kama wewe ni wale ambao wameoa karibuni, wanaona mzigo kulipa fadhila!!! Mtu ambaye anatarajia kuoa/kuolewa, na atategemea kuchangiwa, hawezi kuweka kando hili suala la michango. Inauma but unakuwa huna jinsi...ndiyo jumuiya yetu na jamii yetu, ndiyo maisha tuliyoyachagua.
Ni jambo bora - japo ungechangia harusi fulani ya ndugu yangu kwa mara ya mwisho.
Du!Kujitoa ni ngumu sana,mimi naugulia ndani kwa ndani maana kwa maisha yetu ya kitanzania kujitoa kwenye mambo kama hayo inaweza tokea siku ukakodi watu wa kumzika ndugu yako au hata mke na watoto,jambo hili lina impact kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.
hiyo michango huwa inaniuma roho sana huwa naipotezea tu.unakuta kila mwezi unachangia du ,yakwangu sikuomba mtu mchango ili nisijelipa fadhila sikutaka kabisa,
my wedding was planned 1moth only with my poket only sikuwa na wapambe,sijui watoto blabla ndugu wakalazimisha wakaambia jichangeni wenyewe sichangii chochoteSitegemei kufanya harusi kubwa,itakua ndogo na waalikwa wachache tu.
Naamini hiyo ni budget nitakayo iweza.
Ha ha,jana nimeenda kikao flani nikasema hiki ni cha mwisho.
Eti wao single elf60,double laki1,hutaki unaacha.
hapo kuna kadi kama 5 hivi unatakiwa kuchangia,....yaani hii michango michango tu
ya mwezi huu ningeweza nunua gunia 2 za mchele,mahindi mengi tu kwa ajili ya ugali
nikasahau njaa.
MBAYA ZAIDI SINYWI POMBE,NA SODA SINYWI ZAIDI YA 2,AGGGGGHRRRRR hasara tupu
Basi wenzio watakukamata kwenye matatizo,walimwengu ni ngumu sana kuwakwepa.Kwenye mazishi na matatizo sawa,ila hizi kufuru zingine SITAKIIIII.
Ninajua nitakavyo wakwepa