Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

🔥
 
Mkuu Mwami Atale Kwa msaada wa mtandao hayo maneno ni ya kiibreania maana yake ni "Umebarikiwa wewe, Bwana Mungu wetu, Mfalme wa ulimwengu."
  • Baruch ata– “Umebarikiwa wewe”
  • Adonai Elohim – “Bwana Mungu” (Adonai ni jina la heshima kwa Mungu, Elohim ni neno la kawaida kwa Mungu)
  • Melech haolam – “Mfalme wa ulimwengu”
Sijui kama ni tafsiri sahihi au la. Ila Inaonekana mzee wako alikuwa na elimu ya vitabu hasa zenye asili ya hapo mashariki ya kati.
 
Nguvu za kila kitu za binadam ni bora zaidi.
Naomba ufafanuzi zaidi.
Mwanzoni mwanzoni mwa uzi huu Arsis ulishawahi elezea kuhusu dunia kuwa zipo saba, Ya kwanza ndio tupo sisi binadamu ya pili wapo juju na majuju, ya tatu wapo majini, ya nne wapo wanyama wakubwa kama godzila na Mammoth ya tano wapo Ramadiyin.
Sasa naomba tuongee kuhusu dunia ya kwanza na ya tatu, Umesema nguvu za kila kitu za binadamu ni bora zaidi ya majini Je nguvu hizi ili tuweze kuziona au kuzihisi ubora wake kuna namna mwanadamu inabidi awe au kujiweka?

Swali la pili ni kuwa katika dunia tunayoishi wanadamu kuna maeneo ukienda utaambiwa ni makazi ya majini mfano baharini au maeneo yaliyotengwa kama misitu ,milima n.k sasa hapa utaona majini wapo katika dunia hiihii ila ni kwamba tu wengi wetu hatuwaoni, unavyosema wanaishi katika dunia ya tatu unamaanisha dunia ambayo ni physically au ni hiihii ila tu kuna pazia baina yetu na wao? kama ni dunia physically kama hii ya kwetu ina maana hawa waoishi na sisi huku wametoka huko kwao kuja huku kwetu ni ipi hukumu yao na je sisi binadamu tunaweza kutoka huku kwetu kwenda kwenye dunia yao.?
 
True. Alikuwa anatumia sana Zaburi 151 (kama sijakosea)
Kwenye Bible za kawaida Zaburi huishia aya 150, ila Kuna bible moja inafika mpk 151 hiyo ndo alikuwa akitumia kufanya maajabu.

Ni elim za kale kidogo,,,, miongon mwa Siri za Vatican ni mambo haya
 
Hivi inawezekana mwanaadam kuingia kwenye mlango wa kiroho wa mwanaadam mwenzake... (Kama wanavyofanya majinn)

Yani mfano Juma aingie kwenye ulimwengu wa Hamisi na kujua kinachoendelea huko, kukagua mazingira huko.... Kisha kutoka🤔

Hii kitu inawezekana, au ndo nishaanza kuweuka🤔🤔

Arsis
 
Kwa ufupi, dunia yao / zao ni physically lakini zipo kwenye "dimensions" tofauti. Kuna mipaka au niseme pazia baina ya dunia zote hizo. Tofauti yake ni kama vile unapoota (subconscious) unaweza ukaingia kwenye dunia au ulimwengu mwingine (dimension tofauti bila effort.
 
Asante hapo umezungumzia mtu kuingia kwa kuota vipi binadamu anaweza ingia physically kwenye dunia ya majini mfano kama vile ambavyo bakora alivyokuja katika dunia yetu physically kwa umbo la mtu kwenye kile kisa cha unguja cha yule daktari aliyekuwa anaumwa?
 
Kuna siku nilikaa riadhw siku 3 msikitin... (Huu msikiti ulikuwa hauna movement ya watu wengi n kama ulikuwa umetelekezwa, kwahyo mda mwingi pako kimya sana)

Siku ya pili kitu kama majira ya jion hivi katikati ya nyirad nikapitiwa na usingizi,,,, sasa ikawa n vision ✍️

Nikaona kwenye moja ya ukuta wa msikiti Kuna kitu kama mlango umefunguka (Kama zile movie za time travel, Yani mlango ambao unakupeleka ulimwengu mwingine.

halafu kule ndani Kulikuwa na watu wawili wamevaa kanzu, n kama gatekeeper wamesimama pembeni ya mlango mmoja huku mwingine kule.... n kama walikuwa wanasubiri niingie wafunge mlango

Jamaa alivyozungumza habari za Dimensions na muundo wake huwenda ni kweli ....
Hahaha nimekumbuka mbali kdg asee
(Japo vitu hivi vikikutokea usipokuwa na kiongoz unakuwa hujui maana yake.... )

Hapa Leo ndo nagundua kwamba Ile ilikuwa Dunia ya viumbe wengine.. ila kipindi hcho sikujua lolote🥺
 
Umefanya nikumbuke kitu hapa, Ujue biblia hii ya kawaida kuna vitabu havipo ndio wanaita ''Deuterocanonical'' inajumuisha vitabu kama Tobiti,Yudithi, Baruku, Wamakabayo wa kwanza na wapili na hiyo zaburi ya 151, vitabu hivi inadaiwa vipo katika biblia ile ya kiebrania ya kale ila vilikujwa kuondolewa katika hii biblia ya sasa kwa kudaiwa kuwa ni vitabu vya heshima na si vya mamlaka ya kiroho.
Sasa siku moja nikasema ngoja ni vitatute nisome nikaanza na hiki cha Tobiti alooh! nikakuta neno 'jini' limetumika waziwazi tena imetajwa kabisa 'jini mahaba' nikajisema hivi vitabu vingekuwepo kwenye hii biblia ya sasa kusingekuwa na huu mvutano wa waislamu na wakristo kuwa jini mbaya ndio wao huita pepo ni lexicon tofauti tu kama ambavyo Arsis anapenda kuita.
Ajabu zaidi katika kitabu hichi ilielezwa jinsi ambavyo malaika RAFAEL alimsaidia TOBIA mtoto wa TOBITI kumtoa jini huyo mahaba ambaye alikuwa anamsumbua sara kiasi sara akashindwa kuolewa, wanaume saba tofauti walileta posa lakini wote waliuliwa na huyu jini aliyeitwa 'Asmodeus' Sasa ndio Tobia na yeye akatakiwa amuoe huyu sara ikabidi huyu malaika RAFAEL amsaidie tobia kumuondoa huyo jini mahaba kwa kutumia moyo na maini ya samaki akamuambia tobia ayakaushe alafu achome nyambani kwa sara huyo jini atakimbia na kweli jini huyu alikimbia .
Nilichokuja kugundua ni kuwa hii dawa ya moyo na maini ya samaki inatumika mpaka sasa nadhani ndio hii inaitwa 'miati saila' hutumika kufukuzia majini wabaya kwa wanaosoma ruqya watakuwa wanajua zaidi kwenye kitabu kile cha ruqya mwishoni dawa hii imeandikwa pia kama njia ya kufukuza majini wachafu.
Kweli Elimu imefichwa sana.
 
Hapa ndio unakuja kuona umuhimu wa kuwa na mtu wa kukuongoza au kukupa ABC za mambo ya kiroho watu wengi sana wanapewa ujumbe kiroho kwa njia ya ndoto au maono ila kwakutokujua au kuelewa ujumbe waopewa wanajikuta wanashindwa kutatua changamoto zao, Kumbe njia ya kutatua matatizo yako unaambiwa kila siku ila ndio hivyo unakuwa huelewi.
Mwenyezimungu atujalie ufahamu juu ya jumbe tunazopokea kutoka dimension nyingine.
 
Sasa tutafanyaje ndugu na unajua wenye elim ya Hakika sikuhz n wachache na hata ukikutana nao n wachoyo hawezi kukupa ujuzi wenye manufaa!!

Ila pia ukiwa hauna mwalimu mda mwingine n nzuri maana elim yako inakuwa haina mipaka...... (Japo kwenye foundation lazima awepo mwalimu ila ukishapata basics n vyema ukajitafuta pekeako!!)

Mfano mtu ambaye alikuwa ndio kama mwalimu kwangu, aliyenipa basics, kwasasa nimemuacha mbali sana........ sababu yeye aliendelea kusomewa kitabu ila mm nilichagua kupita njia yenye miba nikaacha universe (spiritual realm) inifunze direct!!!

Ulimwengu wa kiroho hamna siku elim yake utaimaliza.... pia ukipendwa sana unapewa mpk elim kama zawadi.

Binaadam wengi wanamaradhi ya nafsi,,, wababaishaji ndio maana unaona elim ya Hakika inazidi kupotea siku hadi siku, sababu walojaaliwa kupewa hawafundishi wenzao
 
Hapo jambo kubwa linalotukwamisha katika mambo ya kiroho ni hilo la maradhi ya nafsi.
Nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha ibn Arab ''Journey to the lord of power" alielezea hatua za ukuaji wa kiroho mpaka kumfikia Muumba akianza na Kujitenga(Khalwa) alafu Toba na Kujitakasa N.k alieleza hatua kama saba hivi sasa moja katika changamoto inakuja hapa, kadri mwanadamu atakavyokuwa anapiga hatua basi hufunuliwa siri za ulimwengu kama madini, mimea ,wanyama n.k na mwisho huondolewa pazia(Veil) kati ya yanayoonekana kwa dhahiri na yaliyojificha sasa ukiwa katika hiyo safari kuna maadui wa ndani ya nafsi yako wasioonekana ambao wataanza ku-interupt safari yako maadui hao ni
  • Ubinafsi (Self-Centerdness)
  • Kiburi (Arrogance)
  • Majivuno (Boastfulness)
  • Uchoyo (Greed)
  • Tamaa (Desire,Lust)
  • Hasira (Anger)
  • Chuki (Hatred)
  • Uongo (Lying)
  • Udanganyifu (Deception)
  • Fitna (Slander)
  • Kusingizia(False accusation)
  • Husda (Envy) na Kujipendelea (Ego favoritism)
Haya ndio mtu inabidi apambane nayo kuyashinda akiyashinda basi haya hugeuka kinyume chake ndio pale utakuta mchamungu badala ya kuwa na ubinafsi yeye anakuwa na Huruma(Empathy), badala ya kuwa na Kiburi yeye anakuwa na unyenyekevu (Modesty),badala ya kuwa mchoyo yeye anakuwa mkarimu (Generosity) n.k
 
We unakitu Hakika.... Allah akuongoze kwenye njia alowapitisha waja wake wema!!

Kuna kitu umegusa hapo.... ngoja nikupe kisa chake tena huenda ukapata kitu

Kipindi nafika Zawiyan, siku ya pili yake kabla hata sijaanza kufanyishwa taratibu yoyote...... waalimu wangu walimfata yule mwalimu wangu wa kibinaadam wakamwambia hivi
"Mtibu kwanza maradhi ya nafsi kabla ya chochote..... wakampa na nyirad anipe.
(Hii ukiitaka ntakupa!!)

Amini kwamba vita ya nafsi n ngumu kuliko unavyodhan... hapa ndipo Kuna Mungu, hapa ndipo uchamungu ulipo, Siri zote za kitwariqa zipo hapa✍️
 
Tafadhali mimi ninaomba hizo nyiradi mkuu
 
Mkuu unaweza kufafanua kuhusu mizimu?maana inanisumbua kwelikweli
 
Mkuu unaweza kufafanua kuhusu mizimu?maana inanisumbua kwelikweli
Kwa uelewa wangu kias.... Mizimu ni kikundi cha majini wenye mafungamano na jamii flani.

Mizimu huwa na mafungamano yasiyo ya kidini na jamii husika, Imani za kale ndio zilitoa nafasi au katiba au formula ya jamii kuishi na mizimu kwenye maisha ya kila siku...... lakini kutokana na mambo kubadirika jamii nyingi sikuhz zimepoteza elim ya Hakika kutokana na ujio wa dini, usasa n.k
Hvyo watu wakatelekeza huo ubia uliopo enzi na enzi bila kujua kila ushirika huwa na mikataba!!

Watu wengi sana wanateseka na hili swala na wamekubali kwa kuhofia mizimu n ushetani... taratibu zao haziendani na Dunia ya Leo, taratibu zao haziendani na mambo ya kidini n.k
Kwahyo mizimu inapitia changamoto ya kukataliwa kila Leo na watu wao... hvyo ndo ugomvi unaanza hapo, na mwanaadam ili uweze kumcontrol ili akubali jambo lako kwa ridhaa yake lazima umshike kwenye furaha yake na uchumi wake
(Ndo utaona watu wengi wengi wenye ugomvi na asili zao huwa na hali ngumu kimaisha, magonjwa n.k)

Mizimu n asili yako... hawa hawahitaji kitu chochote kutoka kwako zaidi ya kutaka kukutumia kuwasaidia ndugu zako!!
Hili ndio kundi ambalo huwa wanataka kuona umefanikiwa bila mashart yoyote, wenyewe wanachotaka n wapate makazi tu!!

Nimetoa maelezo ya faida zao sabb n upande ambao huwa wengi hawaugusi.... wanaeneza mabaya tu!!

Note: Hawa jamaa sio mashetani na wala sio Babu zako waliokufa zamani!!

Dini kageuka n adui mkubwa sana wa hawa jamaa, sabb wadau wa dini kutokuwa na elim na ulimwengu wa kiroho mafundisho Yao yamekuwa n opposite na uharisia..... wao kazi Yao n kutafsiri maandishi✍️

Kitu kimoja watu wasichokijua n kuwa mizimu inaweza kubadirika baadhi ya taratibu zake kutokana na mtu au wakati!!
Nimeeleza kwa ujumla ili upate picha kubwa
 
Namna gan naweza kupata pia hata kdg ya elimu hizi mlizo nazo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…