Lazia Sultan
Senior Member
- Jun 4, 2020
- 120
- 328
Ni kusini mwa Tanzania nimetembelea Mtwara, kama Msomi wa kati niliyeamua kujiajiri kutoka nyanda za juu kusini nimeamua kujiajiri nipo kusini ambako mjini Masasi kuna Tandale Kama ile ya Dar.
Huku Kuna stori nyingi
wanakusini ni watu wa kubadilika kulingana na matukio, habari yao kuu ni zao la korosho na ufuta. Story ambayo kwao imekuwa Kama gumzo kwa miaka ya karibuni. Ila biashara zinasonga sana na kupo vizuri.
Kuna mama mmoja maarufu Tandale ya Masasi mnunuzi wa nyanya huwa tunapiga story sana na nilijaribu kumhoji kuhusu elimu japo nilikuwa najaribu nimpime tu, akanijibu huku watu wamesoma lakini "wanajisikia sana" yaani wana majivuno.
Kuna sekondari kongwe Kama Ndanda, Masasi girls, Chidya, Ndwika girls... lakini sasa hivi hazivumi. Kumbe mama Anne Makinda kasoma Masasi Girls na Mkapa Ndanda. Sikujua kabla. Akasema Watoto wetu wanasoma huko, walimu wenye degree wanahamishwa kupelekwa shule za msingi wanabakizwa wenye diploma wafundishe sekondari. "Viongozi wetu wamerogwa"
Kiukweli nikaamua kumrudisha huyo mama kwenye biashara zetu za sokoni, ingawa mzigo nilishamaliza Hayo ya elimu nikaona si size yake. Tukaendelea na story nyingine.
Nipo njiani narudi kuchukua mzigo mwingine nipeleke tena kusini.
Aisee Vijana tupambane huko kwenye ajira tuwaachie wenyewe. Kujiajiri Kuna mengi mazuri. Sikujua kuwa wanafunzi wa sekondari wanasoma tuition kwa mwl wa shule ya msingi huko Mtwara.
Ati kuna Degree na Masters zinafundisha msingi huku Diploma zipo High Schools.
Wasaidieni wale watu jamani, sikujua kwanini kusini kunadharaulika kumbe ni mambo Kama yale. Hadi muuza nyanya anawapuuza. Si kweli jamani khaaa!!