Kama mimi mtoto niliyezaliwa uswahilini na mjini kwa nini hivi vikundi vilikuwepo au kuwepo na leo panya roda watoto wa mbwa na n.k

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,723
Habari zenu na poleni wakazi wa dar kwa kusumbuliwa na vikundi hivi ambavyo vinasumbua sehemu ambazo kuna unafuu wa maisha.

Napo sema kuwa na unafuu wa maisha sio kwamba pesa hipo bali maisha ambayo sisi maskini tunaweza kumudu kama sukari ya miambili,miguu ya kuku,nyumba za kupanga bei rahisi,vibiashara vidogovidogo mama zetu wanaweza kufanya kama kuchoma vitumbua na n.k

Sehemu hizi ni kama manzese,mburahati,argentina,popo bawa,tandale,buza,mabagara na viunga vyake,keko,temeke maeneo tofauti,buguruni,kariakoo mchikichini,yombo na viunga vyake,mwananyamala,kinondoni bondeni,kawe na n.k

Haya maeneo hata ukiangalia takwimu ya polisi ya uhalifu na matukio kwenye kuandisha wanatoka wapi basi asilimia 89 yote inatoka huko kama nilivotaja.

maadili na ufatiliaji wa malezi hizi sehemu ni mdogo sana na ukichangiwa na makuzi anayokutana nayo mtoto kwenye jamii kuanzia shule ya msingi,sekondari mpaka mtaani.
yani mtoto wa uswahili kama ameweza kuvishinda hayo yote anakuwa mtu mzuri na muelewa kuliko yule ambaye kakulia sehemu za ushuwani. ndio maana unaona dimondi na wengine wengi mfano wa kuigwa.

Tuje kwenye maeneo yetu ambayo katika kulea ,kiufupi malezi ya uswahilini ni madogo labda mimi nitaweka kwa ufupi tu!.kutokana na ugumu wa maisha asilimia kubwa ya walezi ,wazazi mda mwingi wanatumia kutafuta riziki kwa ajili ya maisha na mda wa kuangalia mtoto hakuna.
na mfano mmoja wakati napanga buruguni malapa hapo baba mwenye nyumba ameachiwa mjukuu na mtoto wake lakini tokea kuandikishwa shule huyo mtoto mpaka anafika darasa saba kumbe ajawahi kufika shule na wala shule jina wala kumtambua!...

Malezi ya uswahili na maadili ni madogo sana pili kuogopana kwa sababu na wenyeji wanaoshikilia maeneo kama umepanga au mtaa ambao kutokana na elimu duni basi unaogopa kukemea ili wasije kukutenga au kufanya jambo baya.

Maadili ya uswahili kwa watoto wa kike ni janga kubwa na umaskini unaokabiri familia mfano uswahili kuna uhuru sana kama kila mtu anaweza kuja kwa mda wake na kuulizana au mzazi au mlezi anakuwa ananguvu ya kuuliza.
wazazi au walezi ufatiliaji wa watoto kama wanasoma,mwenendo wa tabia,marafiki,makundi hata kipato au kapata wapi kuuliza huwa ni ziro na wakipewa pesa kujua mwanae anafanya nini au shuguli fulani hakuna.

ndio maana unaona mzazi au mlezi akiambiwa mwanae ni mwizi ubisha sana mpaka kifo kitakapo mkuta huyo mtoto.

Swala la kipato kwa uswahilini ni finyu na ili kupelekea vijana wengi kuingia na tamaa ya kufanikiwa haraka kwa sababu ya mazingira waliopo kutokuwa navo.

Watoto wengi wanaozaliwa huku asilimia kubwa ni wale ambao vijana hawa jawa na umri wa kukomaa kuwa kama walezi,hao hao tena waliokuwa kwenye makundi,tamaa za mabinti bado wadogo na ugumu wa maisha.

Kama ustawi wa jamii itatambua hili basi wakiweza kuelimisha sana uswahilini na serikali kuweka jitihada kwa sehemu hizi kama kuboresha sera za vijana,ajira,fursa ziwe nyingi sehemu hizo ili kupunguza haya.


Hitimisho:
Kama kuna mtu askari magereza ambaye yupo segerea anaweza kutupa takwimu waliopo hapo ni wangapi wanatoka hizo sehemu !.

View attachment 2208702
 
Umasikini ndio tatizo.

Sema Wana wa uswahilini wana roho nzuri Sana ukilinganisha na waushuani.
Kama nikiambiwa nitoe zuri la maisha ya uswahilini ni roho nzuri ya ukarimu.
 
Umasikini ndio tatizo.

Sema Wana wa uswahilini wana roho nzuri Sana ukilinganisha na waushuani.
Kama nikiambiwa nitoe zuri la maisha ya uswahilini ni roho nzuri ya ukarimu.
Uswahilini watu hawana roho nzuri ila umaskini ndio mnawafanya watu wawe wapole
 
Ni mabeberu na watu wa Ulaya wenye mafikirio Dhalimu.

Hakuna kitu kitu kinachoitwa panya road roda wala rodi
Wacheni mbwembe zenu za kutusokomeleza maneno kejeli na kutulazimisha tuwe kama nyie na siasa zenu hasi.
Msitulazimishe tuwe na values zenu
 
Back
Top Bottom