Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Niliyoyaona nilipokuwa Sero.
Ilikuwa siku ya Ijumaa ya juzi tarehe 02.11.2012 majira ya 13:10hrs nilipigiwa simu na afande mmoja kutoka central police ya Arusha, akiniomba nifike pale mara moja.
Nikachukua kitororo change speed mpaka Sentro, kufika tu nikampigia simu nimwulize yuko wapi .
akanijibu nipo huku nyuma upelelezi nikamfuata kule upelelezi
Nilipofika kule nilimkuta yupo na mdada moja (kumbe ni mke wa afande) ambaye kimsingi mi ndo nilimlalamikia kwa kunifanyia vurugu nyumbani kwangu usiku wa manane (majira ya saa saba na nusu) wa tarehe 21.07.2012, kwa kurusha mawe nk.
Afande yule akaniambia kuwa nina mashtaka, nimeshtakiwa na yule mdada kwa kosa la kuharibu mali.
Nikawaambia RB iko wapi . Wakanionyesha nikawauliza kuwa kwa hiyo mi ni mtuhumiwa? Wakanijibu ndiyo kuanzia muda ule nipo chini ya ulinzi ..
Pale pale nikapiga simu kwa jamaa zangu kwa ajili ya kuwekewa dhamana, ambapo haikupita dakika mbili watu kama ishirini hivi wakawa wamefika pale kwa ajili ya kuja kuniwekea dhamana.
Nikamwambia yule mpelelezi kuwa watu wa kuniwekea mdhamana wameshafika je, kuna sababu ya mimi kuwekwa ndani? Akaniita pembeni .. akaniambia ndg yangu nakufahamu sana, lakini wacha niwekwe ndani kwanza kwa sababu yule binti ameomba niwekwe ndani, na nisipowekwa ndani ataenda kwa RPC. Nikamwambia yule afande basi ngoja nimpigie RPC kwa sababu hata kesi ni ya uwongo akaniambia hapana nisimpigie twende ndani haraka kwa sababu hata rpc yupo kwenye msafara wa Rais.
Pamoja na kuwa na wadhamini pale nikapelekwa haraka haraka pale kaunta ya polisi, nikaambiwa vua viatu!! Mungi jamaniii, mara Mungi vua mkanda!!!!! Nikavua mkanda.. nikatoa pochi, nikatoa hela nilikuwa na Laki saba na nusu hivi .. walipoziona wakadhani nawakabidhi wao kumbe nikamwita jamaa yangu nikamkabidhi kila kitu pale hata viatu vyangu sikuwakabidhi. Kimsingi sikukabidhi chochote pale polisi. Vitu vyangu vyote nilivikabidhi kwa jamaa yangu.
Mlango wa sero ukafunguliwa . Nilipokelewa juu kwa juu na mahabusu . Sikujua kumbe kule ndani kuna viongozi wao, manake nilipokelewa na Mkuu wa wilaya, akani kabidhi kwa IGP wa sero kwa ajili ya kusachiwa, ambaye pia aliwaanda vijana kama wawili wa kukata wenge endapo ningekataa kusachiwa. Nikapiga pipooz ya nguvu wote wakaitikia poweeeer, zoezi la kunisachi likaahirishwa, badala yake nikapelekwa mahali wanapokaa waheshimiwa.
Sijakaa sawa nikamwona mzee moja hivi (mmiliki wa Angoni car hire), kama kawaida mkuu wa wilaya alimpokea na kumkabidhi kwa rpc kwa ajili ya kusachiwa, akaambiwa haaands up! Akakataa, ghafla akakatwa wenge, akakatwa lingine mzee akanyanyua mikono juu na kusachiwa.
Kule ndani nilikutana na watuhumiwa wa makosa mbalimbali;
Mmojawapo alikuwa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na moja, anatuhumiwa kwa kosa la mauaji. Nilimuliza ni kama kweli aliua, akasema ni kweli, walikuwa wanacheza, mwenzake alimkata mguu kwa sime (alinionyesha jeraha), naye akamkata mguuni pia kiasi cha kukata mshipa mkubwa. Nikamwuliza ana muda gani, akaniambia Loliondo alikaa wiki tatu, na huku ana miezi mitatu.
Mwingine nilimkuta yupo hoi hata kusimama hawezi, akaniambia amekaa mahabusu kwa wiki sita sasa. Nikamwuliza mbona ana majeraha makubwa usoni kwenye miguu na mikono, na kwa nini hata vidole vina majeraha makubwa? Akanijibu kuwa alipelekwa Guantanamo (the torture house), alipigwa sana, akapigwa shoti ya umeme, na hata amengolewa kucha zote za mkononi kwa koleo, pia amengolewa meno ya sebuleni mbili. Nikamuliza sababu ni nini, akanijibu kuwa nilikuwa nalazimishwa niitwe Juma badala ya jina langu halisi, anasema inasemekana kuna mtu moja anaitwa juma alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la armed robbery.
Mwingine niliyekutana naye anasema ye anaitwa Chepe, polisi wote wanamfahamu kwa kuwa yeye ni kibaka mzoefu. Anasema ameiba pesa nyingi sana. Nikamwuliza amezifanyia nini na kiwango kikubwa alichoweza kuiba ni ngapi, akajibu kuwa aliwahi kukwapua milioni 18 kwa mara moja, akafanyia starehe, amewahi kusafiri morogoro, mbeya, dar, mwanza, Nairobi, Mombasa nk. Kiwango kingine aliwahi kumkwapua mzungu begi lenye madola mengi hata hakuzihesabu, anasema alichofanya ni kumkabidhi bosi wake wa waizi akazichenji, alipozichenji akawa anafunga baa unga limited mpaka polisi wa unga limited walikuwa wanafunga kituo kwenda kunywa pombe.
Nilikaa pale, jamaa zangu kila wakitaka kunitoa wanaambiwa eti kesi haina mpelelezi, hadi wadhamini walipohoji polisi ni kesi ya namna gani mpaka nisidhaminiwe, kama ni murder waeleze.
Kumbe yule mdada alikuwa ametoa pesa ili nikae ndani mpaka jumatatu.
Akaja yule mpelelezi akiwa na jamaa yangu niliyemkabidhi pesa zangu ili niwagawie. Kwa msimamo na kwa kuwa nina hasira, nikamwambia mpelelezi kuwa naelewa mazingira ya mimi kuwekwa ndani pamoja na kujileta mwenyewe bila kukamatwa, najua walichofanya na yule mwanamke. Nikamwambia siko tayari kutoa hata mia, na nikamtahadharisha jamaa yangu kuwa ukiniambia umetoa kiasi Fulani ili nitoke narudi ndani mwenyewe kwa kuwa sina makosa, bali mnatumia nafasi ya kufahamiana. Nikawaambia lazima sitanyamaza hivi hivi.
Basi jamaa baada ya kusikia hivyo wakanitoa ndani bila hata hati ya dhamana, wakaniambia nirudi jumatatu.
Yule mwanamke aligaragara pale polisi baada ya kuona nimetolewa, anadai kwanini asilipwe pesa yake, lakini bado nilisimamia kuwa sijakataa kulipa pesa yake, bali nakataa kuharibu vitu vyake.
Back to the Isidingo why I was held under police custody:
Nakumbuka ilikuwa tarehe 18.07.2012 siku ya Jumatano mdada moja alinipigia simu majira ya saa 12 jioni, akiniulizia nipo wapi, nikamjibu nipo kwa ofisi, akaniambia ananihitaji pale City Garden ya Sanawari, nikamwambia nikipata muda nitaenda. Siku hiyo sikuenda, badala yake nilienda Lenana kupoteza muda. Akanitumia sms kunilaumu kwanini sikuenda.
Tarehe 19.07.2012 siku ya Alhamisi muda kama ule ule yule dada kanipigia simu, akaniomba nimkute City Garden ya Sanawari tena. Roho yangu ikaniambia wacha niende nikamsikilize.
Nikaenda pale, nikamkuta anakata kilaji, tukaanza mazungumzo, nikamsikiliza sana, alikuwa analalamika kwamba Mungi kama mtu anakupenda anataka aonyeshe kitu gani ili nimwelewe kuwa kweli ananipenda, nikamjibu kidiplomasia, japo nilikuwa nimepata historia yake ya huko nyuma kuwa haikupendeza mbele za jamii, nikamweka kwenye neutral ground asijue kama naelekea ama sielekei.
Ilipofika saa 2 za usiku nikamwambia mi naondoka, akaniomba nikamdrop nyumbani kwake ndo niende zangu home. Mungi na kiherehere na huruma yake akampakia mrembo mpaka home kwake, tulipofika akateremka, akaniambia nyumbani kwake siyo kituo cha polisi, akanilazimisha nikaribie hata kwa dakika moja. Ndani kwake kulikuwa na mdada mwingine, nikasema wacha nikaribie angalau kwa kwa muda. Nikaingia ndani nikakaa kwenye kiti. Baada ya muda yule dada mwingine alitoka sijui alikoenda.
Tulipobaki wawili yule mdada akakimbilia mlangoni akafunga mlango kwa ufunguo halafu akachomoa ufunguo. Nikamwuliza anafanya nini? Akajibu nyie wamangati mnajidai wajanja sana. Nikamwambia kwa nini? Akanijibu amehangaika sana kwa sms kwa ajili yangu, nimekuwa nikimtesa sana.
Nilifikiria kwa muda, nikisema nikionyesha hasira naweza kuletewa matatizo, anaweza hata kusema nimefunga mlango ili nikambake (wanawake wengine wanatumia jinsia yao kunyanyasa wanaume), na angesikilizwa.
Nikawa mpole, nikaanza kumbembeleza afungue mlango, akawa analazimisha tubanjue. Hatukukaa muda akaja kwenye kochi nililokuwa nimekaa, akainama kwenye magoti yangu anafungua zipu. Nikasimama halafu nikamrusha kwenye kiti alichokuwa amekaa. Akaanza kulalamika kuwa namwonea, mimi nikajitetea kuwa tokea asubuhi nilikuwa ofisini hata kula sijala, hivyo nisingeweza kufanya chochote. Sasa kulikuwa na chipsi mezani, akaniambia nikale zile chipsi, mi nikamwambia silagi chipsi.
Baada ya muda kidogo nikasimama, nikaanza kumbembeleza anifungulie, akasema hafungui.
Basi ikabidi nianze kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kumpa matumaini, tulikuwa tumesimama wote, nikaanza kumpapasa, mara napitisha mdomo shingoni mwake, mara nafanya hivi na vile, nikamwahidi kuwa leo ni Alhamisi, kesho ni Ijumaa, nitajiandaa siku ya Jumamosi lazima nizifunge kwake ili nimtimizie ahadi yake.
Tukakubaliana, akanifungulia mlango nikaondoka.
Siku ya ijumaa ikapita hatukuwasiliana.
Siku ya jumamosi akanitumia sms vipi mbona kimya? Nikamjibu sijambo mambo vipi? Akanijibu mabaya, nikamwuliza kwa nini, akajibu njaa. Nikamjibu kama ni njaa ni sawa kwasababu hata mie nina njaa. Baada ya muda akanitumia sms tena akiuliza inakuwaje leo manake nilimwahidi Jumamosi, sikumjibu. Akanitumia sms nyingine tena anaulizia kama nitaenda sikumjibu.
Baadaye saa tisa akanitumia sms ananiambia kuwa amenitumia sms mbili kuwa leo nilimwahidi nitaenda kwake sijamjibu. Nikamjibu kuwa siko tayari kufungiwa ndani ya nyumba, mwanamke huyoooooooo aka react. Kwa hasira akaanza kulalamika kwanini nashikilia wakati tulishamalizana na akanifungulia mlango. Akasema basi yaishe, nikamjibu sawa yaishe.
Saa 12 jioni akanipigia simu kuwa niko wapi, mi nikamjibu kuwa nipo lenana. Akaniambia anakuja, nikamwambia sawa, lakini mi naondoka labda atabaki na mzee. Akaniambia mzee hana hadhi ya kukaa na yeye, akaanza kulalamika kwa hasira. Kama dakika tano hivi akaja mpaka lenana.
Alifika akiwa na hasira kwanini sikuenda nyumbani kwake wakati nilimwahidi, nikamwambia kutiana siyo lazima, halafu kwanini analazimisha ana matatizo gani, akanyanyua chupa ya bia akataka kunipiga nikanyanganya, halafu nikamkata wenge kama mbili hivi akapepesuka, wadau walimshika pale, manake alikuwa anaonekana amelewa.
Mi nikaondoka pale, akaanza kuwapigia polisi ili nikamatwe, lakini polisi walipofika wakaambiwa yeye ndiyo mwenye makosa, lakini wakamwacha kwa sababu anajulikana.
Majira ya saa 7 usiku akafika nyumbani kwangu anarusha mawe, mara anagonga mlango kwa mawe, ananilazimisha nitoke niende naye kwake kwasababu nilimwahidi, nikatoka nje nikampiga mateke na makofi, nikamnyanganya kiberiti na kisu alichokuwa amekificha. Nikamtuma mtu mpaka polisi nikampakia kwenye difenda mpaka polisi. Tulipofika nikafungua jalada ya kuja kunivamia nyumbani na kutishia kuchoma nyumba. Wakati wanataka kumweka ndani roho iliniuma, nikaomba nimdhamini mwenyewe asiwekwe ndani.
Akaruhusiwa kuondoka, kesho yake akaripoti polisi kama kawaida, na faili lilikabidhiwa kwa afande mmoja kwa upelelezi, akanieleza story zake, kumbe amezaa na afande mwenzake, akaniambia hakuna haja ya kupeleka kesi mahakamani, bali tufikie muafaka. Mi nilimweleza kuwa binafsi sipendi kumshtaki kwa sababu upeo wake ni mdogo, na mimi siko tayari kufanya mapenzi kwa nguvu. Tukaiacha pending hadi leo hii.
Sasa alipofikia mahali haoni mafanikio kwangu, akaanza kuungana na jamaa yake pale polisi kwa kuunda kesi kuwa nilimharibia mlango wake na kochi, gharama yake ni sh. Elfu 60, akisema kuwa nimemharibia vitu vyake hataki kutengeneza. Nikamjibu kuwa sijakataa kutengeneza vitu vyake, bali nakataa kuviharibu vitu vyake.
Nimeamini sero siyo wote wanaoenda wenye makosa, bali wengine kwa uonevu.
Nilikaa kama masaa manne ndani lakini niliona kama wiki.
Nawasilisha