Masiku yamepita na miezi imepita, nafsi ina sita lakini akili na moyo vinanisukuma kuandika jambo kuhusu niliyo yaona kwenye jukwaa la siasa humu JF na katika hili nafsi ikashinda, ila leo nikakumbuka kitu fulani kilicho nitokea baada ya kuhoji jambo fulani katika uzi fulani (Sikumbuki jina la uzi) nilijibiwa shombo, nikasema sitachangia kitu katika jukwaa hili sababu watu wamekaa kihamasa zile hamasa hasi, mihemko, ushabiki, chuki, na wanao hoji basi wanahoji
kisengemneke.
Kwa ufupi niliyo yaona wengi wameyaona na wanaendelea kuyaona na wataendelea kuyaona, kwani yako wazi sana, ila haya yafuatayo watu wanatakiwa kuyajua na kinyume cha hayo ni uongo wa wazi.
- Siasa imegawanyika sehemu kuu mbili, inayofaa na isio faa. Lakini kabla sijagusia siasa inayo faa na isio faa, basi ni nini maana ya tamko Siasa ?
- Siasa maana yake ni usimamizi wa jambo fulani kwa kufata utaratibu fulani.
- Siasa iso faa hii kwa jina lingine huitwa siasa ya Kishetani humo inaingia Demokrasia na mfano wake. Siasa inayo faa inayo faa sitaigusia kwani ni kinyume cha ile isio faa.
Yafuatayo tunatakiwa kuyazingatia na kuyajua
- Ukiona mna kiongozi au mtawala muovu, asie muadilifu ujue na nyinyi raia mna tabia kama za kiongozi wenu. Huu ukweli haupingiki. Sasa kutatua hili inabidi kwanza nyinyi raia mbadilike.
- Kiongozi au mtawala hakosolewi kwenye majukwaa, yaani hadharani, kiongozi anakosolewa kwa siri tena na watu wenye maarifa mapana, wenye uchungu wa dhati na mustakabali wa taifa na watu wa taifa. Hapa najua mtasema mnafata demokrasia, huu ni mfumo wa kishetani mfumo usio faa kutawala watu, na hakuna uhuru usio na mipaka, huo tunaita utumwa wa kujitakia.
Maneno machache ni yale yenye faida na yenye kueleweka na haya ndio maneno bora.
Ahsanteni.