Niliyoyaona kwenye Jukwaa la Siasa

Niliyoyaona kwenye Jukwaa la Siasa

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,347
Masiku yamepita na miezi imepita, nafsi ina sita lakini akili na moyo vinanisukuma kuandika jambo kuhusu niliyo yaona kwenye jukwaa la siasa humu JF na katika hili nafsi ikashinda, ila leo nikakumbuka kitu fulani kilicho nitokea baada ya kuhoji jambo fulani katika uzi fulani (Sikumbuki jina la uzi) nilijibiwa shombo, nikasema sitachangia kitu katika jukwaa hili sababu watu wamekaa kihamasa zile hamasa hasi, mihemko, ushabiki, chuki, na wanao hoji basi wanahoji kisengemneke.

Kwa ufupi niliyo yaona wengi wameyaona na wanaendelea kuyaona na wataendelea kuyaona, kwani yako wazi sana, ila haya yafuatayo watu wanatakiwa kuyajua na kinyume cha hayo ni uongo wa wazi.
  1. Siasa imegawanyika sehemu kuu mbili, inayofaa na isio faa. Lakini kabla sijagusia siasa inayo faa na isio faa, basi ni nini maana ya tamko Siasa ?
  • Siasa maana yake ni usimamizi wa jambo fulani kwa kufata utaratibu fulani.
  • Siasa iso faa hii kwa jina lingine huitwa siasa ya Kishetani humo inaingia Demokrasia na mfano wake. Siasa inayo faa inayo faa sitaigusia kwani ni kinyume cha ile isio faa.
Yafuatayo tunatakiwa kuyazingatia na kuyajua

  1. Ukiona mna kiongozi au mtawala muovu, asie muadilifu ujue na nyinyi raia mna tabia kama za kiongozi wenu. Huu ukweli haupingiki. Sasa kutatua hili inabidi kwanza nyinyi raia mbadilike.
  2. Kiongozi au mtawala hakosolewi kwenye majukwaa, yaani hadharani, kiongozi anakosolewa kwa siri tena na watu wenye maarifa mapana, wenye uchungu wa dhati na mustakabali wa taifa na watu wa taifa. Hapa najua mtasema mnafata demokrasia, huu ni mfumo wa kishetani mfumo usio faa kutawala watu, na hakuna uhuru usio na mipaka, huo tunaita utumwa wa kujitakia.
Maneno machache ni yale yenye faida na yenye kueleweka na haya ndio maneno bora.

Ahsanteni.
 
Wewe ndiye una tatizo kukimbia jukwaa sio solution ulitakiwa kupambana kwa hoja mwisho wa siku watu watajuwa pumba na mchele.
Unakubali kwamba kuna watu,hata uwaambie hii ni moja, wanabisha wanakwambia "Hii ni moja lakini sio moja kama niliyo izoea". Lakini hapo tunajua moja ni moja tu hata ikiwa imebinuka juu chini chini juu.

Sasa watu kama hawa kuwasimamishia hoja ni kupoteza muda.
 
Kwamba hatuna ruhusa ya kukosoa pale tunapoona mambo yanaenda tofauti hadi tuwangojee wakosoaji wanaokosoa kwa siri?
Hii ndio adabu, maana nitakuuliza wewe una kosoa kama nani ?

Tatizo ujuaji unakuwa mwingi, halafu mbele giza. Maana ya adabu ni kulifanya jambo kwa uzuri zaidi.
 
Kwani umelazimishwa uchangie kwenye hilo jukwaa la siasa? Mbona yapo majukwaa mengine!! Halafu wakati mwingine ujitahidi kuwa mvumilivu. Siyo kudeka deka tu na kulialia! SAWA SAWA?
Ndio maana nilipo ona hapanifai nikaamua kushika njia, ila nikaemq ipo siku tu nitafikisha huu ukweli.
 
Hapa ndio mahali sahihi,amekosoa demokrasia na suala la kumkosoa kiongozi mitandaoni,mambo haya kisiasa ni sawa lakini kidini sio sawa.

Mfano hata ule uzi wa kula tunda kimasihara kwa jukwaa ulipo ni sawa ila ukiletwa hapa ukaupinga kwa minajili ya dini ni sawa kwa sababu ni uovu.

So ametumia hekma hivyo atakaye kuja kumpinga asishangae kukutana na hoja za kidini.
Umesema kweli.
 
Hii ndio adabu, maana nitakuuliza wewe una kosoa kama nani ?

Tatizo ujuaji unakuwa mwingi, halafu mbele giza. Maana ya adabu ni kulifanya jambo kwa uzuri zaidi.
Hakika ndio maana jukwaa la siasa umekimbia
 
Ninachokiona kwako umekwama na hutaki kwenda na wakati !!. Kiongozi unapokubali kazi ya kuongoza watu (nchi), ukubali pia na kukosolewa. Na si kusifiwa tu hata pale unapoenda kinyume. Unaongoza watu siyo kondoo wa kuswaga. Kwa karne hii kiongozi lazima akosolewe

Kama kwenye halmashauri na bungeni, ambako ilitakiwa ukosoaji uwepo kikatiba na kwa utaratibu hakutakiwi ukosoaji bali kuunga juhudi, wananchi wafanye Je wanapokuwa na dukuduku na yanayoendelea ?!

Usiishi karne ya wafalme , hii ni ya viongozi. Na kiongozi ni kuonyesha njia siyo kutukuzwa [emoji120][emoji40]

Odhis *
 
Asante kwa kutahadharisha. Mwenye masikio amesikia. Ving'ang'anizi na wenye kudhani kumbe hawajui kuwa huwajui
 
Back
Top Bottom