Huyo Kiongozi anayetakiwa kukosolewa kwa siri ni Baba Paroko, Baba Askofu, Baba Mchungaji, ni wale Mitume wetu na Manabii, Masheikh na Maimamu, au ni viongozi gani hasa?!
Kiongozi yoyote hata baba mwenye ngumba ni kiongozi katika nyumba yake, hutakiwi kumkosoa hadharani, kwanza si adabu pili, kiubidamu ni vigumu sana mwanadamu kuvumilia fadheha. Hapa inabidi tuwe wa kweli, hata wewe kama unafikri kwa uzuri, kukosolewa kwenye faragha huwa kunaleta uzito kuliko hadharani, ukizingatia maslahi na madhara, njia ya kukosolewa kwenye faragha huwa ni bora na ina natija sana kuliko njia hii ya pili.
Au unamaanisha kama vile Jiwe anavyowajaza watu ujinga kwamba corona haingii misikitini na makanisani basi ndo aandikiwe barua ya siri, aambiwe "baba, nahisi kama umeteleza hivi, lakini sawa tu baba..."
Nimesema huko juu, ukiona mna kiongozi muovu mjue na nyinyi raia ni waouvu kama yeye au zaidi yake.
Duniani kumepita visit ngozi wagumu wa mioyo mpaka leo ardhi inashuhudia hilo, tatizo njia mnazotumia si sahihi. Haya maneno yalishaandikwa na walio faulu katika utawala, na kalamu zimenyanyuka na wino umekauka kitambo sana. Wapo viongozi wao kuuwa mtu hadharani ilikuwa sio tatizo, lakini wapo watu waliwafungia safari na kuwapa nasaha, hutakiwi kuogopa wa kumuogopa kiongozi kama wewe ni muhusika na una vigezo vya kuweza kumpa nasaha kiongozi, una mpaka, akikubali hilo ndio zuri na bora zaidi, akikataa weww wajibu wako umeondoka.
Uzuri haki na ukweli huu haubadiliki na utabakia hapa hapa, walaumu watakao laumu.
Dah, kumbe ndo maana watu walikulipua huko siasani, manake ndo nachopendea siasani hicho... huna uwezo wa kuhimili vitasa, bora ubaki kusoma tu, na ikibidi usiingie kabisa kwenye jukwaa lenyewe!
Kulipuliwa sio hoja hoja wamenilipua kwa nini, kuna watu aina nne katika maarifa na kujua mambo, ila mule siasani, kuna watu wanajidai wanajua na hawajui kama hawajui, watu wa hivi ni WAPUMBAVU na mpumbavu huwa aana puuzwa.
Angali hivi kuna tatizo kubwa kuliko la mtu kujiona anajua halafu hajui kama hajui, aisee bora uwe chizi kabisa.