Niliyoyaona jimboni Karatu

Niliyoyaona jimboni Karatu

safari ya kwenda loliondo ilinipa nafasi ya kufika jimboni Karatu na kujionea mambo mengi yaliyonivunja moyo na kunikatisha tamaa kabisa juu ya uwezo wa Dr Slaa! nilikutana na msururu wa kinamama wakiwa na ndoo wakienda sehemu za mbali kutafuta maji,pia kwa macho yangu niliweza kuona foleni ndefu sana za maji hii ilithibitisha kuwa kuna shida kubwa ya maji,pia niliweza kuona watoto wengi wa shule wakiwa hawana viatu miguuni,pia wananchi kwa ujumla walionekana wamekata tamaa ya maisha na nyuso zao zilionyesha hivyo! nikajiuliza hili si ndio jimbo la bwana slaa ambalo aliltumikia kwa miaka mingi,sasa kwanini alishindwa kutatua hizi kero za wananchi?? miaka yote alikuwa anafanya nini kama mbunge? kama jimbo dogo hili limemshinda je nchi angeiweza? nilijiuliza maswali mengi sana ambayo nilishindwa kuyapatia majibu kabisa
(Hii ni email niliyofowadiwa na rafiki yangu Mussa Mosha anayemiliki kampuni ya utalii pale Arusha na mfuasi mzuri wa chadema)

Ungefanya utafiti ujue hali ilivyokuwa kabla ya jimbo kuchukuliwa na CDM ndio ulinganishe. Siyo kusema tu wananchi wanashida , kwani ni majimbo mangapi yaliyo chini ya chama tawala yana shida nyingi zaidi ya hayo? Afadhali hata hiyo foleni ya maji ipo watapata muda wao ukifika.
 
: Majibu ya Ushuhuda jimboni karatu
Nimesoma ushuhuda wa mwanajamvi anayejiita KASHAGA kwamba Slaa hajafanya kitu Karatu hivyo hafai kuwa Rais kwasababu hakumaliza tatizo la maji karatu kwa miaka 15 aliyopewa.

Kwanza niseme Ushuhuda wako hapa Jamvini umeniwezesha nisiumize akili kujua kuwa una uwezo mdogo kutafakari mambo na unasumbuliwa na tatizo kubwa la Itikadi ya chama na chuki binafsi dhidi ya Dr. Slaa. Huwezi kusema umeshuhudia tatizo la maji Karatu ukiwa kwenye gari kwenda Loliondo kufuata dawa ya babu. Kwanza ulikuwa na matatizo ya afya wakati unafanya utafiti ukiwa kwenye gari, pili ulikuwa unawaza utapataje dawa ya Babu hasa ukizingatia foleni ya watu, TATU tatizo la maji karatu haikuwa ajenda yako kuitafiti umeiibua tu kwa mawazo yako finyu ukaona ni HOJA hapa, NNE hujamhoji hata mtu mmoja kupata maoni yao kujua hilo tatizo la lini?, TANO hujui historia ya jimbo la Karatu ndo maana ukiona watu wanafata foleni kupata maji unaona ajabu. Zamani hakukuwa na mabomba ya maji kupanga foleni kupata hayo maji zaidi ya msituni, leo umepita hapo kufuata dawa Loliondo umeona mabomba ya maji hiyo ni hatua. CCM imeongoza jimbo hilo tangu enzi na hata baada ya mwaka 1980 ilipogawanywa kutoka Mbulu hawakuweka bomba zaidi ya mabomba ya mjerumani, sasa Slaa kashirikiana na wananchi kwa miaka 15 kaweka mabomba kila kijiji na wananchi wanajisimamia wenyewe huoni ni hatua nzuri unakimbilia kukosoa. Haumtendei haki hata kidogo. Please badilika kimtizamo ndugu yangu. Kwa taarifa yako katika mwanzo wa uwakilishi wa Slaa hapo jimboni alipata sana shida kushirikisha wananchi kuleta maendeleo kwasababu CCM walivuruga kila alichotaka kufanya, mikutano ya hadhara na wananchi kujadili kero zao zilizuiwa kupitia vyombo vya dola, mabomba ya maji yalivyowekwa CCM walikata usiku, yote hiyo ni kutotaka juhudi za mbunge mpinzani isionekane ili warejeshe jimbo uchaguzi uliofuata. Walishindwa kwasababu wananchi wa Karatu tunamisimamo yetu, hatujui itikadi tunajua maslahi ya taifa letu. Fuatilia historia ya jimbo la MBULU tangu wakati wa Nyerere, hatutaki kitu kinaitwa maslahi ya chama au watu binafsi, tunajua demokrasia, Mwaka 1965 Nyerere alimleta Chief Sarwat kama mgombea wa TANU Mbulu wananchi wakamwambia huyo ni wako umetoka naye Dar es Salaam, sisi tunaye kijana wetu wa hapa tutamtuma Bungeni, wakamsimamisha Dodo.Hiyo ndo historia ya misimamo ya wananchi wa Karatu, Babati na Hanang' wakati huo hizo zikiwa tarafa za Wilaya ya Mbulu.

NOTE:Ungekuwa na mawazo hayo ya kuhukumu basi usingechagua CCM mwaka jana kwasababu JK na CCM hawakumaliza matatizo ya jamii kama maji na afya katika majimbo waliyopewa, lakini pia si hukumu halali kwasababu hata babu yetu marehemu Nyerere aliongoza taifa hili kwa miaka 24 na hakumaliza tatizo la umaskini. "Development is a Process"

Natumai kwa haya machache ndugu yangu KASHAGA utabadilika kimtizamo na utaacha kuhitimisha jambo kwa ushahidi mdogo.

Nawasilisha.​
 
Kama ni kweli dr slaa alishindwa kuongoza karatu basi mbunge aliya mteuwa kugombea kwa niaba yake asinge shinda.
 
ukweli siku zote unauma na unachoma,mi nilidhani mngejibu hoja kwa vielelezo lakini ni matusi tupu,mi nasema mtatukana matusi yooteila hamtanifunga mdomo nitaendelea kusema ukweli,Slaa karatu kaishindwa kabisa miaka aliyokaa ni mingi sana pale! mbona kwa Ndesa nimepasifia bila kinyongo,kwanini nisionyeshe ushabiki wangu kwa kupinga mambo aliyofanya ndesa?? lakini amefanya na ndio maana nampongeza,mbowe pale hai amejenga miradi mingi ya maji na kusaidia mashule mengi sana! sasa slaa amefanya nini karatu? ni kipi anachoweza kutembea kifua mbele kafanya yeye kama mbunge(uwezo binafsi) hali ya karatu ni mbaya sana tuache ushabiki

Jamani hivi kweli mmeamua ku-argue na mwanafunzi wa shule ya kata! Please JF members...!
 
h2.jpg h1.jpg handeni.jpg
hapo je ni karatu?:focus:....hapa ni hapo jirani kwa mzee kigoda-HANDENI
 
Toka lini ulimuona Slaa ana nia ya dhati ya kuwaletea watanzania mabadiliko? Bro huyo jamaa yako alipita mbali nadhani angepita kwao na Slaa mwenyewe nadhani angelia kiasi kwamba angeshindwa kusimulia. Nilivoona home kwao nilijiuliza kwa CV hii

1. PADRI WA KANISA LA KATOLIKI 1977-1978-1979-1980-1981-1982-1983-1984-1985-1986-1987-1988-1989-1990-1991
2. Mkurugenzi wa maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu). 1977-1979-1982-1985
3. Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
4. Mkurugenzi Mtendaji,chama cha wasioona Tanzania, 1992-1998
5.Mbunge wa Karatu 1995-2010
alishindwa vipi kupaweka sawa hata nyumbani kwao? kama mtu kampotezea mzee wake how comes awe na uchungu na wasiokuwa ndugu zake?

safari ya kwenda loliondo ilinipa nafasi ya kufika jimboni Karatu na kujionea mambo mengi yaliyonivunja moyo na kunikatisha tamaa kabisa juu ya uwezo wa Dr Slaa! nilikutana na msururu wa kinamama wakiwa na ndoo wakienda sehemu za mbali kutafuta maji,pia kwa macho yangu niliweza kuona foleni ndefu sana za maji hii ilithibitisha kuwa kuna shida kubwa ya maji,pia niliweza kuona watoto wengi wa shule wakiwa hawana viatu miguuni,pia wananchi kwa ujumla walionekana wamekata tamaa ya maisha na nyuso zao zilionyesha hivyo! nikajiuliza hili si ndio jimbo la bwana slaa ambalo aliltumikia kwa miaka mingi,sasa kwanini alishindwa kutatua hizi kero za wananchi?? miaka yote alikuwa anafanya nini kama mbunge? kama jimbo dogo hili limemshinda je nchi angeiweza? nilijiuliza maswali mengi sana ambayo nilishindwa kuyapatia majibu kabisa
(Hii ni email niliyofowadiwa na rafiki yangu Mussa Mosha anayemiliki kampuni ya utalii pale Arusha na mfuasi mzuri wa chadema)
Acha siasa maji taka wewe...JK ameiacha Chalinze bila hata sekondari 1 ukiiacha ile ambayo yeye alisoma middle school, ameacha Zahanati yenye hali mbaya wakati mahitaji ya mji wa Chalinze ni hospitali tena hospitali kubwa,maji yapo mjini tu,shule za msingi hazina madawati na wanafunzi wanashindana wingi wa funza miguuni kutokana na vumbi lililokithiri.....Anza na Jk kwanza kabla hujamshambulia Slaa
 
Toka lini ulimuona Slaa ana nia ya dhati ya kuwaletea watanzania mabadiliko? Bro huyo jamaa yako alipita mbali nadhani angepita kwao na Slaa mwenyewe nadhani angelia kiasi kwamba angeshindwa kusimulia. Nilivoona home kwao nilijiuliza kwa CV hii

1. PADRI WA KANISA LA KATOLIKI 1977-1978-1979-1980-1981-1982-1983-1984-1985-1986-1987-1988-1989-1990-1991
2. Mkurugenzi wa maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu). 1977-1979-1982-1985
3. Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
4. Mkurugenzi Mtendaji,chama cha wasioona Tanzania, 1992-1998
5.Mbunge wa Karatu 1995-2010
alishindwa vipi kupaweka sawa hata nyumbani kwao? kama mtu kampotezea mzee wake how comes awe na uchungu na wasiokuwa ndugu zake?

Musimuandame sana Dr wa ukweli wajameni,, alihitaji kugawa muda vilevile wa kunyatia wake za watu. Ndiyo viongozi wetu hao.
 
Jamani hivi kweli mmeamua ku-argue na mwanafunzi wa shule ya kata! Please JF members...!

Wewe umeelewa au hujaelewa alichokiandika Kashaga? Ameamua tu kutumia herufi ndogo,, hatupo kwenye mtihani wa kuandika insha hapa mpaka ufuate kila rule, kwani wewe mwalimu wa Kiswahili? wa Sekondari gani? Haya na miye nakosea maKuSUdi sasa.. umefurahi? Wewe jibu hoja, acha blah blah.

Mwenzio DCONSCIOUS hapo juu kaandika hivi:

"Kama ni kweli dr slaa alishindwa kuongoza karatu basi mbunge aliya mteuwa kugombea kwa niaba yake asinge shinda".

Sasa kama kweli tupo hapa kuhakiki kila herufi au neno wanaloandika wengine, je hayo makosa yote yaliyokolezwa rangi hukuyaona kwake? Umeyaona kwa Kashaga tu? Wakati unaona ya Kashaga ulitumia macho yapi tofauti na ulipokuwa unasoma post ya DCONSCIOUS? Ajabu kabisa. Au kwa sababu huyo mwingine kaongea positively kuhusu Slaa? Dr. Slaa ni nani asikosolewe? mbona una mahaba ya kumpenda vibaya wewe? Hebu tujifunze kuwa fair na si kuangalia "vijimakosa" vya wengine tu.
 
JK akiwa Mbunge wa Chalinze aliweza kuwapelekea maji salama na ya uhakika wananchi wa jimbo lake.
Unavijua vijiji vya Chalinze wewe? Na unajua ni vingapi vinapata hayo maji? unajua ni vijiji vingapi wanashare maji ya kunywa na mifugo? KWA TAARIFA YAKO NI 30% ya wanajimbo la Chalinze wanaoyapata hayo maji
 
Toka lini ulimuona Slaa ana nia ya dhati ya kuwaletea watanzania mabadiliko? Bro huyo jamaa yako alipita mbali nadhani angepita kwao na Slaa mwenyewe nadhani angelia kiasi kwamba angeshindwa kusimulia. Nilivoona home kwao nilijiuliza kwa CV hii

1. PADRI WA KANISA LA KATOLIKI 1977-1978-1979-1980-1981-1982-1983-1984-1985-1986-1987-1988-1989-1990-1991
2. Mkurugenzi wa maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu). 1977-1979-1982-1985
3. Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
4. Mkurugenzi Mtendaji,chama cha wasioona Tanzania, 1992-1998
5.Mbunge wa Karatu 1995-2010
alishindwa vipi kupaweka sawa hata nyumbani kwao? kama mtu kampotezea mzee wake how comes awe na uchungu na wasiokuwa ndugu zake?

Hebu tupeni sababu za kufukuzwa Kanisani kwa kiongozi huyu, hapa inaonyesha ametumikia sana Kanisa.
 
Toka lini ulimuona Slaa ana nia ya dhati ya kuwaletea watanzania mabadiliko? Bro huyo jamaa yako alipita mbali nadhani angepita kwao na Slaa mwenyewe nadhani angelia kiasi kwamba angeshindwa kusimulia. Nilivoona home kwao nilijiuliza kwa CV hii

1. PADRI WA KANISA LA KATOLIKI 1977-1978-1979-1980-1981-1982-1983-1984-1985-1986-1987-1988-1989-1990-1991
2. Mkurugenzi wa maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu). 1977-1979-1982-1985
3. Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
4. Mkurugenzi Mtendaji,chama cha wasioona Tanzania, 1992-1998
5.Mbunge wa Karatu 1995-2010
alishindwa vipi kupaweka sawa hata nyumbani kwao? kama mtu kampotezea mzee wake how comes awe na uchungu na wasiokuwa ndugu zake?

Alaaah...!!! Kumbe ameishawahi kuwa Padri? Kwenye siasa anatafuta nini alichokikosa Madhabahuni? Hapa kuna kitu. Hebu tuambieni, ni kitu gani kilimtoa ktk utumishi wa Bwana?
 
Unavijua vijiji vya Chalinze wewe? Na unajua ni vingapi vinapata hayo maji? unajua ni vijiji vingapi wanashare maji ya kunywa na mifugo? KWA TAARIFA YAKO NI 30% ya wanajimbo la Chalinze wanaoyapata hayo maji

Kama kawaida yenu, uongo ndio jadi yenu. Nilikuwa nawasubiri kwa hamu kubwa sana niwaumbue ktk hili. Kabla sijakudhalilisha hadharani NATAKA utuambie hiyo asilimia 30 ni sawa na vijiji vingapi, na vipo wapi? Nataka kukomesha uongo wenu humu JF na Taifa kwa ujumla.
 
Unavijua vijiji vya Chalinze wewe? Na unajua ni vingapi vinapata hayo maji? unajua ni vijiji vingapi wanashare maji ya kunywa na mifugo? KWA TAARIFA YAKO NI 30% ya wanajimbo la Chalinze wanaoyapata hayo maji

Kwa taarifa yako mimi nimefanya kazi ktk mradi ule wa maji. Unachosema ni uongo wa hali juu na una lengo la kutaka kupotosha wananchi. Nipe idadi ya vijiji hivyo vinavyokuwa covered kwa asilimia 30 uliyoitaja. Hapa kwangu ni pazuri sana, nataka kuonyesha uongo wenu na tabia ya kukurupuka ktk mambo muhimu.
 
Napata tabu kidogo siamini Kama jimbo la Chalinze lina matatizo sawa na ya karatu inabidi tuanze hapo halafu ndio. Tuje Ikulu mara ingine Kama hili limeonekana karatu tujiulize je propaganda? Au kuna ukweli hasira na kuropoka haviwezi kuleta tija kwa taifa letu. Walioko karatu hebu tuhabatishe ni Kweli Dr Slaa hakufanya chickpea? Mbona alichaguliwa mara 2 tena?
 
huyu kashaga anajulikana.......Muongo mkubwa na mchochezi,,,,hajafika hata loliondo!

muulizeni kwa nini hawakunadamana juzi kama vijana wapenda aman?

We koma, Kashaga sio kijana, ni Steven Wassira Tyson... Waziri wa Public Relation...
 
Jk hana uwezo wa kuwa deal mafisadi, dr slaa anawachana laivu kwa najina, kiongozi shupavu na asiye na uoga.
 
We koma, Kashaga sio kijana, ni Steven Wassira Tyson... Waziri wa Public Relation...

Kashaga hakusema kama alikwenda Karatu. Yeye amesema kuwa kaletewa taarifa ile na rafiki yake anayeishi Arusha. Mbona munakuwa watu wa kukurupuka kama Dr. Slaa? Sasa munaanza kunitia mashaka juu ya uwezo wenu wa kuelewa na kuchambua mambo, inawezekana hapa tunajadili hoja hii na watu wanaojifunza na sio watu wanaoelewa
 
Back
Top Bottom