Niliyoyaona jimboni Karatu

Niliyoyaona jimboni Karatu

Kwa taarifa yako mimi nimefanya kazi ktk mradi ule wa maji. Unachosema ni uongo wa hali juu na una lengo la kutaka kupotosha wananchi. Nipe idadi ya vijiji hivyo vinavyokuwa covered kwa asilimia 30 uliyoitaja. Hapa kwangu ni pazuri sana, nataka kuonyesha uongo wenu na tabia ya kukurupuka ktk mambo muhimu.
Mkuu nasubiri kwa hamu ajibu kuhusu hiyo 30% maana hawa watu wanawapotosha sana wananchi na siye tulio nje ya nchi,, unaweza mtu ukadhani kweli kumbe ni uzushi mtupu.
 
Jenerali
Umeandika kwa kirefu lakini unapoteza mantiki pale unapokwepa hoja ni muhimu vikatolewa vithibitsho kuwa Dr slaa amefanya vizuri Maana wapo watu humu tayari wataanza kuamini si kiongozi mzuri hasa ninapoona wengine humu wanatoa maneno yenye jazba tuwaombe wana karatu watupe utendaji Wa Dr Slaa ili kufuta hoja hii na kuiweka kwenye kapu la propaganda
Tuwe Makini kutetea tukipendacho

: Majibu ya Ushuhuda jimboni karatu
Nimesoma ushuhuda wa mwanajamvi anayejiita KASHAGA kwamba Slaa hajafanya kitu Karatu hivyo hafai kuwa Rais kwasababu hakumaliza tatizo la maji karatu kwa miaka 15 aliyopewa.

Kwanza niseme Ushuhuda wako hapa Jamvini umeniwezesha nisiumize akili kujua kuwa una uwezo mdogo kutafakari mambo na unasumbuliwa na tatizo kubwa la Itikadi ya chama na chuki binafsi dhidi ya Dr. Slaa. Huwezi kusema umeshuhudia tatizo la maji Karatu ukiwa kwenye gari kwenda Loliondo kufuata dawa ya babu. Kwanza ulikuwa na matatizo ya afya wakati unafanya utafiti ukiwa kwenye gari, pili ulikuwa unawaza utapataje dawa ya Babu hasa ukizingatia foleni ya watu, TATU tatizo la maji karatu haikuwa ajenda yako kuitafiti umeiibua tu kwa mawazo yako finyu ukaona ni HOJA hapa, NNE hujamhoji hata mtu mmoja kupata maoni yao kujua hilo tatizo la lini?, TANO hujui historia ya jimbo la Karatu ndo maana ukiona watu wanafata foleni kupata maji unaona ajabu. Zamani hakukuwa na mabomba ya maji kupanga foleni kupata hayo maji zaidi ya msituni, leo umepita hapo kufuata dawa Loliondo umeona mabomba ya maji hiyo ni hatua. CCM imeongoza jimbo hilo tangu enzi na hata baada ya mwaka 1980 ilipogawanywa kutoka Mbulu hawakuweka bomba zaidi ya mabomba ya mjerumani, sasa Slaa kashirikiana na wananchi kwa miaka 15 kaweka mabomba kila kijiji na wananchi wanajisimamia wenyewe huoni ni hatua nzuri unakimbilia kukosoa. Haumtendei haki hata kidogo. Please badilika kimtizamo ndugu yangu. Kwa taarifa yako katika mwanzo wa uwakilishi wa Slaa hapo jimboni alipata sana shida kushirikisha wananchi kuleta maendeleo kwasababu CCM walivuruga kila alichotaka kufanya, mikutano ya hadhara na wananchi kujadili kero zao zilizuiwa kupitia vyombo vya dola, mabomba ya maji yalivyowekwa CCM walikata usiku, yote hiyo ni kutotaka juhudi za mbunge mpinzani isionekane ili warejeshe jimbo uchaguzi uliofuata. Walishindwa kwasababu wananchi wa Karatu tunamisimamo yetu, hatujui itikadi tunajua maslahi ya taifa letu. Fuatilia historia ya jimbo la MBULU tangu wakati wa Nyerere, hatutaki kitu kinaitwa maslahi ya chama au watu binafsi, tunajua demokrasia, Mwaka 1965 Nyerere alimleta Chief Sarwat kama mgombea wa TANU Mbulu wananchi wakamwambia huyo ni wako umetoka naye Dar es Salaam, sisi tunaye kijana wetu wa hapa tutamtuma Bungeni, wakamsimamisha Dodo.Hiyo ndo historia ya misimamo ya wananchi wa Karatu, Babati na Hanang' wakati huo hizo zikiwa tarafa za Wilaya ya Mbulu.

NOTE:Ungekuwa na mawazo hayo ya kuhukumu basi usingechagua CCM mwaka jana kwasababu JK na CCM hawakumaliza matatizo ya jamii kama maji na afya katika majimbo waliyopewa, lakini pia si hukumu halali kwasababu hata babu yetu marehemu Nyerere aliongoza taifa hili kwa miaka 24 na hakumaliza tatizo la umaskini. "Development is a Process"

Natumai kwa haya machache ndugu yangu KASHAGA utabadilika kimtizamo na utaacha kuhitimisha jambo kwa ushahidi mdogo.

Nawasilisha.​
 
Jk hana uwezo wa kuwa deal mafisadi, dr slaa anawachana laivu kwa najina, kiongozi shupavu na asiye na uoga.

Dr. Slaa anawachana kweli mafisadi tena live, lakini mbona hachukui hatua ya kuwapeleka mahakamani kama anaona JK hawezi? Nyie munadanganywa bure, wenzenu wanavuta pesa kibao toka kwa mafisadi, nyie mumekaa kuwashangilia tu. Hivi ktk hali ya kawaida kabisa ulitaka JK achukue hatua gani wakati mropokaji wenu kamtaja kuwa JK naye ni miongoni mwa mafisadi? Hana hata akili ya kujua kuwa mwisho wa siku JK ndio anayetakiwa kuchukua hatua. Huo ulikuwa ni mpango mahsusi kapanga na mafisadi ili kukwamisha zoezi la kuwachukulia hatua mafisadi.
 
Jenerali
Umeandika kwa kirefu lakini unapoteza mantiki pale unapokwepa hoja ni muhimu vikatolewa vithibitsho kuwa Dr slaa amefanya vizuri Maana wapo watu humu tayari wataanza kuamini si kiongozi mzuri hasa ninapoona wengine humu wanatoa maneno yenye jazba tuwaombe wana karatu watupe utendaji Wa Dr Slaa ili kufuta hoja hii na kuiweka kwenye kapu la propaganda
Tuwe Makini kutetea tukipendacho
Well said Songasonga.
 
Mkuu nasubiri kwa hamu ajibu kuhusu hiyo 30% maana hawa watu wanawapotosha sana wananchi na siye tulio nje ya nchi,, unaweza mtu ukadhani kweli kumbe ni uzushi mtupu.

Wamezoea hawa. Nasubiri anipe jibu nitoe data zilizo sahihi, na baada ya hapo nitapenda kumtambua rasmi kwa namna nitakayoisema humu ndani. Enough is Enough... Semeni ukweli, tujadili mambo ya ukweli, sio kuleta uongo humu ndani. Siku Taifa hili likitumbukia ktk migogoro ya kisiasa kwa uchochezi wa namna hii, watakaoathirika ni ndugu zetu, na sio wageni kama munavyowaramba miguu kama mufanyavyo sasa.
 
kwa sababu post yako inaonekana inauelekeo wa kimajungu, hatuna budi kukuchangia kama ifuatavyo:
kwanza inaonekana wewe ni mvivu wa kufikiri, na pengine unasahau haraka sana. Ningekuona wa maana zaidi kama ungefanya research kwanza kwa utaratibu mzima ulivyotakiwa kuwa na pia kupata maoni ya raia wenyewe wahusika kuhusu mbunge wao, alafu ndio uje kupost hoja hapa. Vinginevyo inaonekana kama majungu tuu kwa Dr. Slaa. Sijui umetumwa na kile kitengo cha propaganda??
hivi wakati unaandika hukujiuliza hata kidogo jimbo lilikokuwa la Mkapa au Kikwete lilikuwaje na likoje sasa?? unataka kumaanisha hayo majimbo sasa yana full umeme, maji na barabara zote zina lami????? au hukuliona hilo unaliona kwa Slaa peke yake??
unapomlinganisha na ndesa, unataka kuwaambia nini watz wengine???? kwamba serikali haiwezi kuleta maendeleo kwa sababu ni wajibu wa mbunge kuleta kuleta hayo maendeleo kwa hiyo mchague wabunge matajiri???
think twice before you write!
 
safari ya kwenda loliondo ilinipa nafasi ya kufika jimboni Karatu na kujionea mambo mengi yaliyonivunja moyo na kunikatisha tamaa kabisa juu ya uwezo wa Dr Slaa! nilikutana na msururu wa kinamama wakiwa na ndoo wakienda sehemu za mbali kutafuta maji,pia kwa macho yangu niliweza kuona foleni ndefu sana za maji hii ilithibitisha kuwa kuna shida kubwa ya maji,pia niliweza kuona watoto wengi wa shule wakiwa hawana viatu miguuni,pia wananchi kwa ujumla walionekana wamekata tamaa ya maisha na nyuso zao zilionyesha hivyo! nikajiuliza hili si ndio jimbo la bwana slaa ambalo aliltumikia kwa miaka mingi,sasa kwanini alishindwa kutatua hizi kero za wananchi?? miaka yote alikuwa anafanya nini kama mbunge? kama jimbo dogo hili limemshinda je nchi angeiweza? nilijiuliza maswali mengi sana ambayo nilishindwa kuyapatia majibu kabisa
(Hii ni email niliyofowadiwa na rafiki yangu Mussa Mosha anayemiliki kampuni ya utalii pale Arusha na mfuasi mzuri wa chadema)

Hapa mimi mtanzania mwenzio sikuelewi hata kidogo, Mbona majimbo yaliyomengi nchini hayana maji, umeme, barabara, huduma bora za afya, usafiri wa hadhi nk nk? Nani anastahili lawama ya kutokuwepo hizi huduma za kijamii Karatu, Dar Es salaam, Bagamoyo, Tandahimba nk, Ni Serkali tawala ya CCM iliyokaa madarakani kwa miaka 50 au Slaa anayejaribu kuonyesha udhahifu wa hii serikali mfu? Acha ushaabiki, tafakari na utapata jibu.
 
Wana Chadema, hebu mukae na kujiuliza hivi ni sahihi kwa Mwanasheria wenu, Mh. Mabere Marando kumtetea FISADI mkubwa, Yusuf Manji? Hivi zile pesa anazolipwa kwa madai ya kazi hiyo munaona ni sahihi? Ni sawa sawa na kununua baiskeli ya magurudumu mawili kwa USD. 1 Mil, je itaingia akilini hii? Lifanyieni kazi hilo halafu tukutane tena humu ktk JF kulijadili. Tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo.
 
Kazi ya pili kwa wana Chadema. Hebu fanyeni utafiti wa nani anayelifadhili gazeti la UMOJA?
 
Kazi ya tatu kwa wana Chadema, naomba muifanyie uchunguzi, hivi ni kweli Chadema haina uhusiano na Mafisadi?
 
Kwa kweli mimi nashindwa kuwashangaa watu wanaopoteza muda kuchangia thread zisizo na tija yoyote zinazoanzishwa na kashaga & co.
Dawa yao ni kusoma utumbo wao halafu unachapa lapa!!

Nafikiri wana JF wanasahau. Tulishakubaliana kwamba hoja yoyote inayoletwa hapa jamvini na Kashaga na kundi lake, no comments please halafu mwenyewe atafunga vilago!!!

Tiba
 
Hapa mimi mtanzania mwenzio sikuelewi hata kidogo, Mbona majimbo yaliyomengi nchini hayana maji, umeme, barabara, huduma bora za afya, usafiri wa hadhi nk nk? Nani anastahili lawama ya kutokuwepo hizi huduma za kijamii Karatu, Dar Es salaam, Bagamoyo, Tandahimba nk, Ni Serkali tawala ya CCM iliyokaa madarakani kwa miaka 50 au Slaa anayejaribu kuonyesha udhahifu wa hii serikali mfu? Acha ushaabiki, tafakari na utapata jibu.

Kuna ubaya gani akianza na jimbo la Karatu?
 
Acheni kukurupuka hapa kama Mzee wenu Dr. Slaa, nenda kasome vizuri majukumu ya Mbunge halafu ndio uje kuchangia humu, hivi unadhani una debate na wakurupukaji kama nyie? Mzee kakurupuka mpaka ktk mambo ya "human nature"? Halafu mumekaa munashangila tu badala ya kumwambia ukweli ili ajirekebishe, nyie ni watu wa ajabu saaana. Inaonekana hii ni tabia yenu ktk Chama chenu cha wana-harakati.

Kumbe Chechetuka, Salimia na Kashaga ni mtu mmoja yule yule!!!!!!

Tiba
 
Wana Chadema, hebu mukae na kujiuliza hivi ni sahihi kwa Mwanasheria wenu, Mh. Mabere Marando kumtetea FISADI mkubwa, Yusuf Manji? Hivi zile pesa anazolipwa kwa madai ya kazi hiyo munaona ni sahihi? Ni sawa sawa na kununua baiskeli ya magurudumu mawili kwa USD. 1 Mil, je itaingia akilini hii? Lifanyieni kazi hilo halafu tukutane tena humu ktk JF kulijadili. Tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo.

Bahati mbaya mimi sio mwana CHADEMA lakini kuna haja ya kutofautisha nafasi ya Marando kama mwanasiasa na Professional yake. Anamtetea Manji kwa nafasi yake kama mwanasheria ingawaje siamini kama Marando anakubaliana na Ufisadi wa Manji (kama kweli huo ufisadi upo).

Tiba
 
Kama hiyo haitoshi, Mtu na Waziri mhusika, wapo kufungua Bomba la Maji ili akina mama wapate maji kwa urahisi.

Kama BAJAJI vile kwa akina mama Waja wazito...... Heheheee!!!!!

mugumu.jpg

Hawa walinzi wanamwachia Huu Jamaa kubeba ndoo akianguka nayo! kwanza kashindwa kuinyanyua zaidi ya hapo
 
Sasa nimejua kwanini unaandika pumba, kumbe ni Mgonjwa! Pole tunasubiri michango yako baada ya kupata tiba tutumie kama sampuli ya kutathimini uwezo wa dawa katika kunyavua akili za watu, sijui kwanini umeenda mwenyewe bila Makamba au Hiza maana wote wagonjwa hao.
 
pole sana

usidanganye watu. kwenda kwa babu kuna kupitia jimboni karatu ya wapi? kama ulitoka arusha ulipitia mto wa mbu, selela, engaruka, engaleselo sale then kwa babu. kama ulitokea mara then ulipita waso au mbugani hadi kona ya digodigo. ni wapi kote huko kuna jimbo la karatu? mto wa mbu na vijiji kadhaa nilivyotaja ni monduli na vingine ni ngorongoro. duh! watz noma.
 
Yeye kama mbunge wa pale kwa miaka zaidi ya kumi alipambana vipi na hizo changamoto? huwezi kujivuna utaliletea taifa neema ikiwa kwako yamekushinda! wako wabunge wanaoweza kujivuna kutatua kero mbalimbali sasa yeye alifanya nini miaka yote?

karatu hakuna shida ya maji ni uongo. huyu mtoa maada si mwangalifu. kapitia karatu ipi kwenda kwa babu? ni monduli kwa blaza huko na asidanganye watu. ndo maana wazungu hutembea na ramani. anunue simu yenye map next time ajue miji apitayo.
 
Huyu nia yake ilikuwa tofauti na heading ya thread yake,tumeshamjua ...sasa EL na utajiri wake ameifanyia nini Monduli...maana ndo kwa asilimia kubwa inapitiwa na njia ya kwa babu
 
Hiyo safari ya Loliondo umepitaje jimbo la KARATU? mto wa mbu ni MONDULI pia unapita Engare sero ambayo ni LONGIDO na hata hiyo Loliondo ni jimbo la NGORONGORO...usipotoshe watu

"there are many ways to kill a rat" so usikariri mzee there are many ways mzee
 
Back
Top Bottom