Niliyoyaona Jijini Mwanza

Niliyoyaona Jijini Mwanza

Hivi lile soko likilokuaga la nguo especially ile mitumba ilokua inamwagwa pale makoroboi lilihamishiwaga wapii??? 🤔
Siku ya kufungua yale ma baloo nilikuaga natingajee kusagula viwalo vya mtumba juzikati nilipita nikaambiwa lilihamishwa !!
Nafikiri waliamishiwa pale mlango mmoja kama sikosei(sina uhakika sana).

Lile soko lilikuwa linafurika watu balaa hasa watoto wakike.
 
Wakuu wazima?

Nafikiri kuna kapost kangu niliwah post humu kuuliza sehem nzuri ya kupumzika kwa hapa Mwanza.
Sasa kwa kipindi hiki cha wiki 2 nilizokaa huku hay ndo niliyoyaona na kujifunza

1. Wanawake wanapiga kazi sana huku(wanajishughulisha) mida ya jioni barabarani utakutana nao sana wakiuza either matunda, dagaa, samaki, maharagwe yaliyochemshwa tu, nyanya na vikorombwezo vingine4, pia wanachoma mahindi na kuyauza.

2. Wengi wa wasichana huku ni waoga sana hasa kwa strangers.

3. Draft la huku wengi hucheza French( hawajui kuhusu British).

4. Kila wanapokaa hudhani wote ni wa huku hivyo huongea tu kilugha.

5. Hotels and Lodge za huku no bei rahis sana sana huanzia 30k.

6. Mwanza ni mji mzuri sana, una mandhari nzuri kuliko Arusha( kwa mtazamo wangu)

Asanteni wakuu
nilifika mwanza mwaka jana june kwa mara ya kwanza nilishangaa ni mji mzuri na mkubwa tu na watu wengi Arusha haifikii mwanza.
 
Arusha isingekuwa usela mavi wa wale machalii clearly hii battle ya Arusha vs Mwanza wala isingekuwa ngumu. Tatizo la Arusha ni vijana wengi wana usela wa miaka ya 90 karne hii..

Arusha ipo mbele ya Mwanza kwa karibia kila kitu, kitu pekee kinachoichafua Arusha ni tabia za vijana wengi wenyeji wa hapo hawana lugha wala charisma ya kuwapokea na kukaa na wageni. Wao kwao mgeni wanamwona ni Mzungu tu.
 
Mwanza ni pazuri kuliko Arusha,
Arusha wana usela mavi wa kisenge sana.

Mwanza unatembea usiku kucha pale mjini husumbuliwi na mtu, hata watoto wa wakoma wamepoa.

Arusha ikifika saa 3 kila mtu kajifungia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Tatizo watu wanaotoka mikoa tofauti na A town (ukiondoa Kilimanjaro) wana inferiority complex wakikutana na vijana/wakazi kutoka A town.

Wengi wanakosa kujiamini na kudhani wanabaguliwa kumbe hakuna mtu mwenye time nao.

Unaweza gundua hili kwa urahisi tu hasahasa miongoni mwa vijana chini ya miaka 35. Kwa wazee hauwezi kuona hili. Hii naifananisha vile Watanzania wengi walivyo na inferiority complex wakikutana na waKenya.

Hapa Arusha tourism imesaidia pakubwa vijana wengi kuwa na self confidence kwasababu yamwingiliano na wageni.

Jambo la msingi na lakukumbuka, sisi Watanzania wote ni watu poa. Haina haja yakujiona dhaifu au kudhani wakazi wa Arusha wanawachukia wakazi wa maeneo mengine ya Tanzania.

Tanzania ni moja.
 
Mwanza ni pazuri kuliko Arusha,
Arusha wana usela mavi wa kisenge sana.

Mwanza unatembea usiku kucha pale mjini husumbuliwi na mtu, hata watoto wa wakoma wamepoa.

Arusha ikifika saa 3 kila mtu kajifungia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kama unafuatilia na ulikaa nao watu wa Arusha mara nyingi wao ndo wanasifia mji wao na usela wao hakuna mtu ana wasifia ..


Ndo maana hata comedian wao wanahype sana mji wao mwisho wa siku wanaonekana kama matahira Yale mavazi hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvaa vile
 
Back
Top Bottom