Niliyoyaona Jijini Mwanza

Wahindi wenyewe kuna wengine hawajui kuongea kihindi hata kidogo...wanaongea lugha za ukanda wao mfano watu toka tamil nadu lugha tofauti kabisa na hao wa Mumbai
Yeye amekariri kisa tu media zao huwa zinapanga Nini akisikie Basi. Nature ya binadamu Ni Ile Ile regardless of location sema labda hivi mabadiliko haya kuingiliana na elimu Yana displace values za watu
 
Naongea kilugha wala sivungi, bora mie housegirl we msela mavi una nini zaidi ya kuvuta bangi na kuvaa kata kundu,
Wewe jaribu tu utajuta kuja mjini ukubwani🤣
 
Jamani tuache huu ukoloni wa kuita kilugha? Lugha ni lugha zote tu na tuseme kama Kisukuma, Kinyakyusa au Kijerumani na Kama hatujui tunasema. Tukisema kilugha Km kukejeli na kuona ujinga
 
Kila mkoa unawatu wa hovyo.

Au umesahau hapo Dar es Salaam kuna vijana wa hovyo wanajiita panya road?

Sasa watu wakianza kuandika uhalifu uliowakuta wakiwa miji mingine hapa Tanzania hatutafika mwisho?

Kingine. Mambo ya ubabe enzi za ujana ni kawaida tu. Tena vijana umri miaka 16 - 20?

Hiyo age vijana wengi wadogo wakiume ni kawaida kuonyeshana ubabe wa hapa na pale. Hasahasa shuleni.

Na mimi nasema hiyo ni sawa tu. Miaka hiyo ndiyo miaka ambayo vijana wadogo wanajifunza namna yakuwa wakakamavu lakini pia namna yakujilinda kama kundi.

Ni survival skills. Kama hutokei mtaa utashindwa kuelewa.

Mwisho hongera kwa kumbukumbu nzuri ulipokuwa A town.
 
Ila watu wanaosemaga Mwanza ni Mji mzuri Huwa wananishangaza sana
Kwa hiyo kama wewe unaona Mwanza siyo mji mzuri unataka kila mtu awe na mawazo kama yako? Au wewe kwa mtazamo wako kwamba Arusha ni mji mzuri unataka kila mtu akubaliane na wewe? This is the world of differences. Ukipendacho wewe mwingine hakipendi! Mimi mwenyewe nakushangaa kufananisha kamji ka Arusha na jiji la Mwanza!
 
Hakuna kitu kama hicho...vijana wa Arusha Wana matatizo ya ushamba na too much ego inayowafanya washindwe kuishi vyema na watz wengine...
 
🤣🤣🤣Kwakweli nilikuwaga nawasikia ila kwa nayoona kwa ndg hawa,, Arusha ni mibange na wasela mavi,,, niko njiro mkuu njoo unipige
Hapa tunajadili mada na si vinginevyo.

Umeleta madai vijana wa Arusha wanavuta bangi. Nikasema sawa hilo ni dai lako.

Lakini unapaswa uthibitishe. Usipofanya hivyo basi wajumbe hawawezi kukuchukulia kwa uzito unaostahili.

Pia unazungumzia nije nikupige. Je, hiyo inatija yoyote katika mada tunayojadili?
 
Kujaribu nini kuvuta bangi?? Pombe yenyewe tu situmii, hiyo bangi labda ipikwe mboga
Usijaribu kuongea kilugha kwa simu ukija mjini kilugha ongea huku...

Hiyo bangi wala usijaribu hata kwenye mboga utawehuka na kutatembea uchi mjini watu wateseke kukusitiri
 
Hakuna kitu kama hicho...vijana wa Arusha Wana matatizo ya ushamba na too much ego inayowafanya washindwe kuishi vyema na watz wengine...
Vijana wengi wanaotoka mikoa mingine tofauti na A town wakiwa college/university hujiona dhaifu mbele ya wanafunzi wenzao kutoka Arusha.

Unafahamu kwanini?

Kwasababu vijana waliozaliwa Arusha wanapata advantage yakukutana na wageni wanaotoka mataifa ya Ulaya na Amerika na hii inawapatia nafasi yakufahamu mambo mapya tangu wakiwa wadogo.

Vijana hawa wakienda shule nakukutana na vijana kutoka mikoa mingine isiyo na utalii basi huona wanajidai au wakorofi.

Ni kama vile wewe ukirudi kijijini kwenu waskaji wa kijiji wanakuona wewe mtukutu na much know.

Uko na swali jingine nikufafanulie?
 
Usijaribu kuongea kilugha kwa simu ukija mjini kilugha ongea huku...

Hiyo bangi wala usijaribu hata kwenye mboga utawehuka na kutatembea uchi mjini watu wateseke kukusitiri
Huyu dada ana ushamba mwingi.

Au dishi limeyumba.

Hafahamu anachosimamia anadhani kuropoka ndiyo kushinda hoja.

Mara analaumu bangi mara anataka ajaribu kama mboga.

Nilimwambia hapo juu namna yake yakufikiria haipo sawasawa.
 
Usijaribu kuongea kilugha kwa simu ukija mjini kilugha ongea huku...

Hiyo bangi wala usijaribu hata kwenye mboga utawehuka na kutatembea uchi mjini watu wateseke kukusitiri
Mbona naongea na cha kunifanya hakipo, hata saiv nimetoka kuongea kilugha changu vizuri tu, bangi ni yenu mi hainihusu
 
Mbona naongea na cha kunifanya hakipo, hata saiv nimetoka kuongea kilugha changu vizuri tu, bangi ni yenu mi hainihusu
Wewe endelea tu ipo siku utajuta kuja mjini ukubwani😅
 
Yaan hata maneno yako yanaonesha haujiamini na kujikubali...kuna watu unaona ni Bora zaidi yako so unakuwa na shobo nao...

Trust yourselves bro...Haya mambo ya kuishi ukiwa unajistukia sio mazuri kwa maendeleo binafsi....na vijana wengi wa Arusha mna ili tatizo...ndo maana mnajiingiza kwenye bang, kuolewa na vibibi...kuiga umarekani ambao hata hao wamarekani wanajithidi kuusolve..nk nk
 
Kwenye kilugha ni uongo, Mwanza imejaza watu wa mikoa mbali mbali. Hasa mkoa wa Mara, lugha itumikayo ni kiswahili tu.
anaweza akawa sahihi licha ya wageni wengi kuvamia mwanza lakini wasukuma bado wapo wengi sana naupendelea xana kuongea kilugha, busweru,buhongwa namaeneo yapembeni mwa jiji bado kunawazawa wengi xana....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…