Niliyojifunza kupitia mbio za Mwenge 2019

nipekidogo

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
1,587
3,026
Salaam wote!

Katika hangaika zangu za hapa na pale nilipata fursa ya kushiriki katika mbio za mwenge kwa baadhi ya mikoa ya Tanzania mwaka huu na kama tunavyojua Mwenge hukimbizwa Wilayani mpaka vijijini na unapokesha basi Mwenge hukesha sehemu iliyochangamka na Mara nyingi inakuwa kwenye Kata.

Nilipata bahati ya kuwa kwenye mbio za Mwenge Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Njombe, Ruvuma, Mtwara na kisha Lindi hii ikiwa ni mkoa mzima mpaka vijijini kunapokuwa na Miradi ya maendeleo inayozinduliwa au kukaguliwa.

Katika Mikoa yote niliyopita Mikoa ya Kusini ina umasikini wa kupindukia mno, nikianza na Iringa na Njombe pamoja na kwamba ni wazalishaji wa chakula na mbao kwa wingi lakini huko vijijini ni tabu tupu, bado watoto kwenda shule bila viatu na nguo zilizochanika ni kawaida sana, watoto kukaa kwenye mawe darasani ni kawaida pia, huko Ludewa na Makete maisha ni magumu sana, ukiwatizama wananchi unawahurumia wamekata tamaa na hawajui kesho yao japokuwa ni maisha ya kawaida kwao.

Maisha ya wananchi wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi yanafanana na hata tamaduni zao ni kama zinafanana kwa kiasi kikubwa, Ruvuma ni Mikoa Mkubwa na kama tujuavyo ni wazalishaji wa chakula lakini huko Nyasa, Mbinga vijijini ni shida sana, kuna umasikini wa kutupwa, watu wa Kusini wanapenda ngoma mno, ukifika mgeni ambae sio mwenyeji utashangaa kuazia wakubwa mpaka watoto, wanaume kwa wanawake wanapenda ngoma na mdundiko.

Kiwango cha maambikizi ya Ukimwi kiko juu sana, japo kuwa kwa sasa Iringa, Njombe na Mbeya inaongoza kwa maambukizi lakini nakwambia wanawake wa Mikoa ya Kusini hawatakunyima ukiwaomba kwa kulinganisha na Mikoa ya Kaskazini niliyopita. Ruvuma, Mtwara na Lindi kumkuta binti Mdogo ana mtoto ni kawaida kabisa, Wenyeji wa Mtwara na Lindi elimu kwa mtoto wa kike sio kipaumbele kabisa!

Nikiwa Ruvuma,Lindi na Mtwara nilijaribu kutembelea mabanda ya kupima HIV na kujaribu kuwauliza wahudumu wa Yale mabanda kuhusiana na maambukizi, nilijibiwa maambukizi kwa vijana yako juu na hawajali kuambiwa ana maambukizi.

Mtwara na Lindi wanampenda sana Ndugu yao Harmonize, hata kama wanacheza ngoma ikipigwa nyimbo yake wote wanaacha kucheza ngoma wanakimbilia inakopigwa nyimbo yake. Huko Tandahimba kuna shida ya Maji kupita kiasi, Wamama asubuhi wanapishana wakiwa na baskeli na madumu ya Maji huku wamebeba watoto mgongoni. Masasi maisha yako juu sana kama hapa Dar vyakula mpaka nyumba ni kama hapa Dar.

Mikoa ya Mtwara na Lindi wadada wanaojiuza wanakuwa ni wale wahudumu wa bar, hii nimeikuta Masasi, Newala, Nanyumbu, Tandahimba na sehemu za Mijini za hiyo Mikoa kwahiyo ukimtaka muda wowote unamchukua unaenda kupiga Ila utamlipa pesa yake na utamlipa meneja wa bar kwa muda ambao hayupo kazini.

Wakauu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wanaogopa sana mbio za Mwenge, Mwenge unapokuwa kwenye eneo lake wanakuwa wenye hofu wakiogopa miradi yao kukataliwa na wanamnyenyekea sana Kiongozi wa mbio za Mwenge ambae anapofika anakuwa na taarifa zote kupitia usalama wa taifa mkoa au wilaya.

Yako mengi nimejifunza kupitia mbio za Mwenge mwaka huu niishie hapa kwanza!
 
Tutatowa mitumba kutoka Lindi,Mtwara na Iringa na kuwauzia mabeberu mwakani.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kwa tathmini yako, kukimbiza mwenge kuna manufaa (yapi) au ni utumiaji mbaya wa rasilimali?
 
Wabishi sana kupima, takwimu za mikoa hiyo usiichukulie serious sana
Nakubaliana na wewe, nilipokuwa Iringa, Njombe na Ruvuma mabanda ya kupima yalikuwa na foleni ndefu sn mpaka usiku sana watu walijaa kupima bila hata kutangaziwa lkn Lindi na Mtwara ilikuwa mpaka wanatangaziwa wakapime lakini bado mabanda yalikuwa wazi bila watu isipokuwa Masasi ndio upimaji ulikuwa juu mpaka usiku
 
Kwa tathmini yako, kukimbiza mwenge kuna manufaa (yapi) au ni utumiaji mbaya wa rasilimali?
Majibu yako pande zote mbili, gharama ni kubwa ingawa kila mkoa unagharimia shughuli za mwenge unapokuwa mkoni kwake na wilaya inagharimia pia, kwa upande mwingine kuna ufujaji Mkubwa wa fedha unaibuliwa na mwenge kwenye miradi ya maendeleo, na ninaamini km Mkulu ataifanyia kazi ile ripoti kuna wakurugenzi wengi watapigwa chini kwa kushindwa kusimamia miradi na wengine kushiriki kutafuna fedha za miradi.
 
Hyo nafasi ya kukimbiza mwenge umeipataje? Weka sifa maana Wazenj wengi wamehusika
 
Ni kweli Mkuu, nadhani kwakuwa wageni wanaoenda kule hutumia mipra vinginevyo ingekuwa hatari kwa maambukizi kwasababu kukunyima papuchi kwao ni kama dhambi
Ila wageni wanaoenda Njombe,Iringa na Mbeya ambako maambukiz yako juu hawatumii mipira? Sababu dhaifu sana hii.
Ama kuhusu mtoa mada,amezungumzia umaskini wa Mikoa ya kusini hasa vijijini kwamba ni wa kutupwa. Bahati nzuri Tanzania tunafahamiana vizuri tu. Ukiondoa mkoa wa Kilimanjaro,hali ya maisha vijijini kwa kila mkoa ni mbaya sana na inafanana.
Hivi,vijiji vya mkoa wa Dodoma,Singida,Tabora,Mara,Manyara,Arusha,Mwanza,Shinyanga,Geita,Simiyu kutaja michache vina nini hasa kuweza kusema vina unafuu kuliko vijiji vya Walima korosho wa Mtwara,Walima Chai wa Njombe,Iringa?
Mtoa mada anaandika kana kwamba vijiji vya mikoa mingine vina utajiri. Ukweli ni kwamba vijiji vya mikoa ya Kusini vina unafuu mkubwa kuliko kule kwenye matembe ya wafugaji.
Itoshe tu kusema mtoa mada kaamua kuiponda mikoa husika kwa sababu anazozijua yeye,lakini kama kwa umaskini wa vijijini,Mikoa ya kusini ina unafuu kuliko hata vijiji vya mikoa mingine,ila yote kwa yote,vijijini maeneo yote,hali ya maisha bado hairidhishi,na karibia viko sawa kwa sawa.
 
Mtoa mada naomba unisaidie maswali yafuatayo
1.ni sifa zipi anatakiwa awe nazo mtu ili kuwa kiongozi wa mbio za mwenge
2.ni kwann hawa viongozi wa wilaya au wakurugenzi wanamuogopa sana huyu mkimbiza mwenge hali yakuwa yeye wala syo wa kudumu ktka huo mwenge
3. huyu kiongozi wa mwaka huu kabla ya kuteuliwa alikuwa idara gani huko serikali
4.kuna athari gani inatokea endapo ule mwenge utazimika na upepo pale kiwanjani maana wlinzi wanakuwa makini kuukinga ule mwenge dhidi ya upepo
5.Hayo mafunzo ya kuukinga huo mwenge huwa yanatolewa wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom