Niliyojifunza kupitia mbio za Mwenge 2019

Niliyojifunza kupitia mbio za Mwenge 2019

Nchi hii bado maskini sana. Kuna sehemu hata dar ukiona watu wanavyoishi utagundua hali bado.
 
Salaam wote!

Katika hangaika zangu za hapa na pale nilipata fursa ya kushiriki katika mbio za mwenge kwa baadhi ya mikoa ya Tanzania mwaka huu na kama tunavyojua Mwenge hukimbizwa Wilayani mpaka vijijini na unapokesha basi Mwenge hukesha sehemu iliyochangamka na Mara nyingi inakuwa kwenye Kata.

Nilipata bahati ya kuwa kwenye mbio za Mwenge Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Njombe, Ruvuma, Mtwara na kisha Lindi hii ikiwa ni mkoa mzima mpaka vijijini kunapokuwa na Miradi ya maendeleo inayozinduliwa au kukaguliwa.

Katika Mikoa yote niliyopita Mikoa ya Kusini ina umasikini wa kupindukia mno, nikianza na Iringa na Njombe pamoja na kwamba ni wazalishaji wa chakula na mbao kwa wingi lakini huko vijijini ni tabu tupu, bado watoto kwenda shule bila viatu na nguo zilizochanika ni kawaida sana, watoto kukaa kwenye mawe darasani ni kawaida pia, huko Ludewa na Makete maisha ni magumu sana, ukiwatizama wananchi unawahurumia wamekata tamaa na hawajui kesho yao japokuwa ni maisha ya kawaida kwao.

Maisha ya wananchi wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi yanafanana na hata tamaduni zao ni kama zinafanana kwa kiasi kikubwa, Ruvuma ni Mikoa Mkubwa na kama tujuavyo ni wazalishaji wa chakula lakini huko Nyasa, Mbinga vijijini ni shida sana, kuna umasikini wa kutupwa, watu wa Kusini wanapenda ngoma mno, ukifika mgeni ambae sio mwenyeji utashangaa kuazia wakubwa mpaka watoto, wanaume kwa wanawake wanapenda ngoma na mdundiko.

Kiwango cha maambikizi ya Ukimwi kiko juu sana, japo kuwa kwa sasa Iringa, Njombe na Mbeya inaongoza kwa maambukizi lakini nakwambia wanawake wa Mikoa ya Kusini hawatakunyima ukiwaomba kwa kulinganisha na Mikoa ya Kaskazini niliyopita. Ruvuma, Mtwara na Lindi kumkuta binti Mdogo ana mtoto ni kawaida kabisa, Wenyeji wa Mtwara na Lindi elimu kwa mtoto wa kike sio kipaumbele kabisa!

Nikiwa Ruvuma,Lindi na Mtwara nilijaribu kutembelea mabanda ya kupima HIV na kujaribu kuwauliza wahudumu wa Yale mabanda kuhusiana na maambukizi, nilijibiwa maambukizi kwa vijana yako juu na hawajali kuambiwa ana maambukizi.

Mtwara na Lindi wanampenda sana Ndugu yao Harmonize, hata kama wanacheza ngoma ikipigwa nyimbo yake wote wanaacha kucheza ngoma wanakimbilia inakopigwa nyimbo yake. Huko Tandahimba kuna shida ya Maji kupita kiasi, Wamama asubuhi wanapishana wakiwa na baskeli na madumu ya Maji huku wamebeba watoto mgongoni. Masasi maisha yako juu sana kama hapa Dar vyakula mpaka nyumba ni kama hapa Dar.

Mikoa ya Mtwara na Lindi wadada wanaojiuza wanakuwa ni wale wahudumu wa bar, hii nimeikuta Masasi, Newala, Nanyumbu, Tandahimba na sehemu za Mijini za hiyo Mikoa kwahiyo ukimtaka muda wowote unamchukua unaenda kupiga Ila utamlipa pesa yake na utamlipa meneja wa bar kwa muda ambao hayupo kazini.

Wakauu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wanaogopa sana mbio za Mwenge, Mwenge unapokuwa kwenye eneo lake wanakuwa wenye hofu wakiogopa miradi yao kukataliwa na wanamnyenyekea sana Kiongozi wa mbio za Mwenge ambae anapofika anakuwa na taarifa zote kupitia usalama wa taifa mkoa au wilaya.

Yako mengi nimejifunza kupitia mbio za Mwenge mwaka huu niishie hapa kwanza!

Unamuonaje JPM si atafanya kitu kikubwa kwa watu maskini hawa? Ni wishful thinking yangu kwa sasa, lakini given time, JPM atafanya kitu kikubwa kwa watu hawa katika kipindi cha utawala wake. Pia unajua kuelezea mambo vizuri sana utadhani ni mwandishi wa habari. Mungu atawapa neema watu hawa, iko njiani inakuja siku moja!
 
Hapana ndugu yangu hata hapa nimeyaleta tu baadhi kwakuwa tunatumia hizi ID fake vinginevyo nisigejaribu! Ningeweza kuweka hapa picha na baadhi ya video fupi nilizorecord za baadhi ya matukio lakini vinaweza kunitambulisha na kuniingiza matatizoni kwakuwa baadhi ya maeneo hawaruhusiwi watu wengine kuingia ndani Mfano wanapojadili mradi gani wapitishe au wasipitishe unapokuwa a dosali, wanapopitia nyaraka za manunuzi na ujenzi au watu wamakumbusho wanapokuwa wakiwamegea taarifa husika so kuja vitu nikivieleza vitanitambulisha kwakuwa hata wakuu wa Mikoa, Wilaya na wakurugenzi utolewa nje.
A Whistleblower..Beware of Big Brothers, Je unaonaje mwenge una faida au hasara katika Jamhuri ya Muungano??
 
Ila wageni wanaoenda Njombe,Iringa na Mbeya ambako maambukiz yako juu hawatumii mipira? Sababu dhaifu sana hii.
Ama kuhusu mtoa mada,amezungumzia umaskini wa Mikoa ya kusini hasa vijijini kwamba ni wa kutupwa. Bahati nzuri Tanzania tunafahamiana vizuri tu. Ukiondoa mkoa wa Kilimanjaro,hali ya maisha vijijini kwa kila mkoa ni mbaya sana na inafanana.
Hivi,vijiji vya mkoa wa Dodoma,Singida,Tabora,Mara,Manyara,Arusha,Mwanza,Shinyanga,Geita,Simiyu kutaja michache vina nini hasa kuweza kusema vina unafuu kuliko vijiji vya Walima korosho wa Mtwara,Walima Chai wa Njombe,Iringa?
Mtoa mada anaandika kana kwamba vijiji vya mikoa mingine vina utajiri. Ukweli ni kwamba vijiji vya mikoa ya Kusini vina unafuu mkubwa kuliko kule kwenye matembe ya wafugaji.
Itoshe tu kusema mtoa mada kaamua kuiponda mikoa husika kwa sababu anazozijua yeye,lakini kama kwa umaskini wa vijijini,Mikoa ya kusini ina unafuu kuliko hata vijiji vya mikoa mingine,ila yote kwa yote,vijijini maeneo yote,hali ya maisha bado hairidhishi,na karibia viko sawa kwa sawa.
ni kama vile umenifilisi!!
kuna kasumba moja kubwa ipo kuhusu mikoa ya kusini na watu wake, huwa nastaajabu chanzo hasa ni nini?. ningeshangaa sana kama nisingeyasoma hayo niliyoyasoma kutoka kwa mtoa mada.....hili nililiona tangu nikiwa sekondari. na kama hujatembea kwa hakika kuna watu wanadanganya mno, sijui inawafaidisha nini?!!!!!! yaani mtu atazunguka mwisho wa siku 'laana' zote na za kila namna lazima azishushie mikoa ya kusini hususani lindi na mtwara.....hapo nafsi yake inatulia! sisemi kwamba haina tabu zake lakini kwanini zizidishwe huko tu?!!!!!!

1. UMALAYA: jamani, yaani lindi na mtwara ndiyo wanawake wanapatikana hovyo tu?!!! ina mantiki kwa wasiyoyajua maeneo mengine kama kagera, dodoma n.k. lakini kwa dunia ya sasa ilivyo, kwa vyovyote, sehemu inayongonoka zaidi lazima na maambukizi yatakuwa juu zaidi. period! takwimu za maambukizi ya UKIMWI, kwa miaka kadhaa, nafikiri zimeiweka mikoa ya lindi na mtwara mbali kabisa....na hakuna ubishi kuwa muingiliano wa watu sasa ni mkubwa mno sehemu hizo kutokana na fursa mbalimbali zilizopo na zinazoendelea kuibuliwa. mtoa mada anatoa sababau kuwa watu wa huko hawapendi kupima, amehitimisha hivyo kwa kile alichokiona katika vituo vya kupima siku aliyopita alipokuwa anakimbizwa na mwenge.....shughuli za mwenge tunazijua na nina uhakika hata hajapata muda wowote wa kutosha kuangalia au kufuatilia mambo kwa kina! na kama ni dereva ndiyo kabisaaaa!

2.UMASKINI: hii sehemu ndiyo huwa inanichekesha, kunishangaza na kunisikitisha zaidi. inanichekesha sababu kwa umaskini huu sikioni cha maana kinachoendelea katika vijiji vingi vya tanzania....dhiki kila kona kutokana na mbinyo wa kisiasa, kisera, kiutamaduni na kimazingira unaovikabili vijiji karibu 90% vya tz. nikiona akili inahamishiwa katika kushindanisha maskini hawa badala ya kuyashughulikia matatizo yao ya msingi, nabaki na kicheko tu, si cha furaha lakini! ukweli ni kuwa vijiji vingi vya lindi na mtwara vina unafuu mkubwa tu kuliko vijiji vya mikoa kibao tu ninayoifahamu...lkn ukweli huu hausemwi. nimewahi kufika eneo flani mikoa ya katikati hapo ambayo haijatajwa na mtoa mada, watu wanaweka booking hadi katika lori linalopeleka mazao mjini....abiria wanakaa juu ya magunia. inanishangaza na kunisikitisha sababu watu , tena wasomi, wanalishwa na kutema vitu kiupendeleo wa wazi kabisa.

NINA HAKIKA:
1. kama nyumba zinazoezekwa kwa kinyesi cha ng'ombe zingekuwa zinapatikana lindi na mtwara, basi ubaya huo ungevuma hadi mbingu zingepata habari.
2. kama wale watu wanaoishi maporini na kula nyama mbichi na magome ya mti hadi leo wangekuwa wanapatikana lindi na mtwara, basi hadi mbingu zingesikia habari hiyo.
3. kama uuaji wa watu wanaohisiwa wachawi, uchunaji wa ngozi za binadamu, kukata viungo albinos, kupiga nondo za kichwa, kuuwa watoto n.k. yangekuwa yanafanyika lindi na mtwara basi mbingu zingepata habari.

bado najiuliza hivi vita ya MAJI MAJI, yenye dhima yote ya muungano ambayo ilikuja kuwa falsafa kubwa ya mwalimu Nyerere, ingekuwa imepiganwa maeneo mengine tofauti na lindi, mtwara na ruvuma MVUMO wake ungekuaje?!!!!!!! majibu sina.

kuna tatizo kuhusu kusini, huo ndo ukweli.......kusini haipendwi, imepaa bahati afika ya kusini tu basi!!!!

mi kwetu kibaha lakini kikazi nipo mikoa ya kusini kwa muda mrefu sasa!
 
Unamuonaje JPM si atafanya kitu kikubwa kwa watu maskini hawa? Ni wishful thinking yangu kwa sasa, lakini given time, JPM atafanya kitu kikubwa kwa watu hawa katika kipindi cha utawala wake. Pia unajua kuelezea mambo vizuri sana utadhani ni mwandishi wa habari. Mungu atawapa neema watu hawa, iko njiani inakuja siku moja!
Yaah JPM ana mapungufu yake ila Serikali imejitahidi upande ujenzi wa barabara. Sehemu nyingi zimejengwa barabara kwa kiwango cha lami.
Yaah kitaaluma ni mwanahabari (Journalist) japo siifanyii kazi.
 
Tatizo baadhi ya watu wanadhani nimekuja kukebehi kitu ambacho si kweli, nilichoeleza ni kile nilichoona na kujifunza huko, na sikueleza yote, yapo ya hovyo zaidi nikiyasema nitashambuliwa sana! Na haimaanishi kwamba mahali pengine au Mikoa mingine haiko hivyo lakini nani anaeweza kuzungumzia kitu asichokijua na kukiona kama haitakuwa story za kutunga tunga tu?
sawa, unaweza kutujuza na ulichojifunza kwenu pia ili tufaidike pia?!!!! naamini kwenu unakujua vizuri kuliko hata hizo sehemu chache ulizokimbiza mwenge!
 
sawa, unaweza kutujuza na ulichojifunza kwenu pia ili tufaidike pia?!!!! naamini kwenu unakujua vizuri kuliko hata hizo sehemu chache ulizokimbiza mwenge!
Mkuu Kwetu ni Mbeya nimezaliwa na kukulia Isanga na badae Kasulu kidogo mpaka nilipomaliza primary baada ya hapo muda mwingine wote maisha yangu tunafukuzana hapa Dar Lakini familia yangu kwa ujumla iko hapo Isanga, Mbeya naijua kwa kiasi nako pia kuna shida kama huko kwingine.
 
Unamuonaje JPM si atafanya kitu kikubwa kwa watu maskini hawa? Ni wishful thinking yangu kwa sasa, lakini given time, JPM atafanya kitu kikubwa kwa watu hawa katika kipindi cha utawala wake. Pia unajua kuelezea mambo vizuri sana utadhani ni mwandishi wa habari. Mungu atawapa neema watu hawa, iko njiani inakuja siku moja!
Magufuli hana sababu ya kuwapa kitu,hata masai nao watadai wapewe kitu.Kitu cha kuwapa watanzania wote ni kuwawekea mazingira mazuri ya biashara yao,mfano korosho ikiwa bei nzuri watauza watapata pesa watajenga,wataanzisha biashyara nk.Habari hii inaonesha bado tunasafari ndefu.
 
Umasikini ni mtaji wa kisiasa kwa chama chetu. Hebu usituchafulie mkuu
Kinachochekesha zaidi bajeti ya kupokea mwenge haipungui 40M kwa wilaya za vijijini halafu ni matumimizi ya kupokea kukesha na kukabidhi tu yaani siku moja tu . Nadhani hizi gharama zingeelekezwa kwenye vitabu ama madawati kila mwaka tungemaliza hilo tatizo dani ya miaka 3-4. Tunahamia kitu kingine ila kwa hivi mwenge hauna tija.
 
Mchakato wa kuwapata wakimbiza mwenge huanzia wazira wa kazi na maendeleo ya vijana. Pili wakuu wa wilaya na wakarugezi wanahofia kwasababu kama kiongozi wa mbio za mwenge akiukataa mradi huyo kiongozi husika anakuwa kwenye wakati mgumu kupoteza nafasi yake na hasa kama kuna ufujaji wa pesa.

Tatu huyu mkimbiza mwenge wa mwaka huu anafanyakazi Taasisi flani ya kiserikali kwa upande wa Zanzibar na kama sijasahau ana taaluma ya Uhandisi na katika lile kundi watano nilifanikiwa kujua kazi zao na taaluma zao pia

Kwa miezi mitatu niliyokuwa na mwenge sijaona ukizimika na sidhani kama utazimika kwakuwa kukitokea upepo unazungukwa usizimike na mafunzo kwa ujumla yanasimamiwa na Idara usalama wa Taifa na kila Mkoa lazima wawepo watu wa usalama wa Taifa wanaoulinda usiku na mchana mpk wanapokabidhi Mkoa mwingine!
Usalama hawalindi mwenge kazi yao ni itifaki na ulinzi kwa wakimbiza mwenge wa kitaifa. Mwenge unalindwa na polisi ffu .
 
Kwahyo huyu mkimbiza mwenge yupo fit zaid ya Simbu lakin mbona muda mwingi wanatembea na magari huko kukimbia sijui wanakimbiaga wapi
Mwenge unatakiwa kukimbizwa si chini ya mita 100 mpaka sehemu mradi ulipo. Hivyo wakikaribia mradi mnashuka wote kwenye magari mnaanza kukimbia kufuata mradi ulipo. Wengine wanaweza kukimbia hata 500m lakini usipungue 100m.
 
Magufuli hana sababu ya kuwapa kitu,hata masai nao watadai wapewe kitu.Kitu cha kuwapa watanzania wote ni kuwawekea mazingira mazuri ya biashara yao,mfano korosho ikiwa bei nzuri watauza watapata pesa watajenga,wataanzisha biashyara nk.Habari hii inaonesha bado tunasafari ndefu.
Ni kweli Mkuu, malalamiko ya watu wa Lindi na Mtwara ni bei ya zao la korosho kutowanufaisha wakulima, nilioongea nao wengi wamelalamika kwa walichotendewa na Serikali mwaka juu kwenye korosho
 
Mwenge unatakiwa kukimbizwa si chini ya mita 100 mpaka sehemu mradi ulipo. Hivyo wakikaribia mradi mnashuka wote kwenye magari mnaanza kukimbia kufuata mradi ulipo. Wengine wanaweza kukimbia hata 500m lakini usipungue 100m.
Uko sahihi Mkuu, lakini pia kumbuka hiyo inakuwa ni shughuli ya siku nzima na kila siku mpaka mwenge utakapozimwa, kiukweli wanafanya kazi kubwa ya kukimbia kimbia kila baada ya muda flani wanapofika kwenye mradi na nafikiri ndio maana wameweka pia kigezo cha umri.
 
Mtoa mada wew nilikuona pale nyangao na shati lako la kitenge
 
Mkuu Kwetu ni Mbeya nimezaliwa na kukulia Isanga na badae Kasulu kidogo mpaka nilipomaliza primary baada ya hapo muda mwingine wote maisha yangu tunafukuzana hapa Dar Lakini familia yangu kwa ujumla iko hapo Isanga, Mbeya naijua kwa kiasi nako pia kuna shida kama huko kwingine.
Sasa si utakua umeshajulikana mpaka sasa wasifu huu
 
Magufuli hana sababu ya kuwapa kitu,hata masai nao watadai wapewe kitu.Kitu cha kuwapa watanzania wote ni kuwawekea mazingira mazuri ya biashara yao,mfano korosho ikiwa bei nzuri watauza watapata pesa watajenga,wataanzisha biashyara nk.Habari hii inaonesha bado tunasafari ndefu.
Nimesema atawafanyia kitu, siyo kwamba atawapa kitu. JPM hana kitu cha kuwagawia wa-Tanzania isipokuwa ana karama ya kuwafanyia kitu cha kipekee kabisa!
 
Yaah JPM ana mapungufu yake ila Serikali imejitahidi upande ujenzi wa barabara. Sehemu nyingi zimejengwa barabara kwa kiwango cha lami.
Yaah kitaaluma ni mwanahabari (Journalist) japo siifanyii kazi.

Naomba nikuhakikishie kuwa kama ipo siku tutabahatika kuchagua Rais ambaye ni Malaika kutoka mbinguni, hilo tatizo la mapungufu tutakuwa tumelikomesha kabisa.
Kuhusu habri uliyoandika, ni kweli mtirirko wake namna ilivyo unaonyesha kuwa ni wewe ni professional, vingnevyo ulitakiwa uwe exceptionally gifted katika kuandika. Una uwezo wa kufikisha ujumbe vizuri sana. Mimi nimekuwa mpenzi sana wa kusoma novel na vitabu tangu nikiwa darasa la pili na hivyo nina uwezo mkubwa wa ku-predict nani ni professional writer/journalist na nani siyo. Ubarikiwe kwa makala nzuri na kuonyesha kutoka ndani ya roho yako namna ulivyoguswa na maisha ya ndugu zetu hawa. Nilivyosoma tu habari yako nilipata kitu kikubwa kwamba pamoja na uwezo wako mzuri wa kuelezea matukio uliyoyaona, bado pia yalikugusa kutoka ndani ya roho yako. Majaliwa, Samia na JPM,..., tuuombee huu utatu mbarikiwa, Mungu azidi kuwabariki. Anapowabariki hawa, anakuwa amebariki chain nzima ya uongozi mpaka wenyeviti wa Serikali za mtaa!
 
Back
Top Bottom