Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Naona ATCL wameamua kwamba wataenda China kupitia Bangkok, Thailand Bangkok. Njia hii ina ushindani sana, haitakuwa na faida kwao kupitia Bangkok na kushindana na mashirika makubwa ambayo yameweka mizizi sana kwenda au kupitia Bangkok pamoja na Ethiopian Airways and Kenya Airways.
Ninawashauri kwamba wawe innovative katika kubuni njia ambapo wanaweza kuvuta abiria hata kutoka nchi jirani badala ya mentality ya Kitanzania ambapo jirani yako akifungua genge la nyanya mtaani kwenu na wewe unaenda kufungua genge la kuuza nyanya pembeni yake badala ya kuuza bidhaa ambayo wale wanaonunua nyanya kwa jirani yako wataitaka kwako!
ATCL wafikirie route kama kwenda China kupitia Hong Kong, au Mumbai, au Delhi au Bangalore badala ya kufuata mkumbo wa kila shirika linaloenda China kupitia Bangkok. Hatuhitaji kuuza nyanya kwa kuwa jirani anauza nyanya. Tuuze vitunguu na chumvi.
Wakienda China kupitia Hongkong, Bangalore, Delhi kwa mfano, unaweza kukuta wanavuta abiria kutoka nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda Zambia nk ambazo watapeleka regional flight kwa ajili ya hiyo connection, na kupata pia abiria wanaoenda huko ambao labda inabidi waende hadi South Africa au Addis Ababa kupata hiyo connection.
ATCL kwenda China kupitia Bangkok unajiweka katika wigo wa kukosa abiria pale Bangkok kwa kuwa wana options nyingi sana. Jiulize, kwa nini abiria watumie ATCL na sio Kenya Airways au Ethiopian Airways? Anzisha route kwa namna ambayo unawa-compel abiria kutumia ATCL, sio unawapa ATCL kama option nyingine kati ya nyingi zilizopo.