Nilivyonusurika kifo nikiwa mtoto zaidi ya mara 3

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
415
1,032
Habari zenu,

Ndugu zangu kwenye ukuaji tunapitia hatua mbalimbali za maisha, kipindi nikiwa mdogo nishanusurika kifo zaidi ya mara 3, kusema kweli nilikuwa mtundu sana nisiyesikia chochote,na michezo yangu ilikuwa hatari sana,tena ya kutosha.

Naanza kama hivi. Mara ya kwanza. Kipindi nikiwa na miaka 3 nilishaingiaga kwenye friji nikaka huko zaidi ya dakika 45,wazazi walinitafuta sana wakajua nimepotea au nimeishiwa,maana kipindi kile watoto walikuwa wanaibiwa sana.

Sasa baada ya kunitafuta kwa dakika 45 wakachoka,wakaona waende police kutoa taarifa,sasa kabla hawajaenda baba akaona apate maji ya baridi,ndipo hapo akanikuta kwenye friji baridi limenikolea viungo vyote vimelegea,vidole vishakakama wakaniwaisha hospital ikawa pona yangu.

Mara ya pili. Kipindi tukiwa watoto tulipenda kucheza kombolela, na kipindi kile ukibutua kopo unaonekana shujaa,sasa wakati nakimbia kujificha kumbe jirani alifumua chemba lake la mavi lilikua limejaa,na hakutoa taarifa kwa majirani.

Wakati nakimbia nilijua shimo bado limefunikwa, kipindi nakimbia nilikuwa naangalia nyuma ghafla ile nageuka mbele USO kwa USO shimo lipo mbele yangu, nikaruka kwa nguvu ile nafika ng'ambo ya pili nikakosa BALANCE nikawa narudi kinyume nyume kama mtu aliyesukumwa mlimani.

Sasa wakati narudi kinyume nyume huku nateleza kuelekea shimoni,nikapapasa pembeni nikagusa mawe ya chemba ndiyo yalionisaidia kukishika,huku miguu ikiwa ndani ya mavi mpaka kwenye magoti,wakaja watu kunivuta ndo ikawa pole yangu

Mara ya tatu. Hii ilikuwa moshi,ilikuwa juma Juma tatu ya ubarikio(moshi ubarikio jumapili,sasa Jumatatu waliobarikiwa huenda sokoni kununua vitu kwa ela waliopewa zawadi siku ya ubarikio).

Sasa baada ya kununua zawadi zetu ile tunarudi nyumbani ilikuwa mida ya saa 11 jioni na mpaka kufika nyumbani kuna zaidi ya km 18,kuna pick up ikatupita tukaona tudandie tulikuwa watoto 4,sasa ile chuma ya kuweka miguu ikangooka tukaanza kuburuzwa,kweli tuliburuzwa ile akili inatukaa sawa tukaachia mikono kwenye lile chuma ndo ikawa pole yetu,tulichubuka mapaja,tumbo na kucha za vidole zilingooka.

Maisha ni mapito.
 
Nina mtoto wa kiume aisee ni nunda hatari,kuna siku nilikuwa nampa dawa ya malaria kanigomea Katu katu,piga makofi wapi nikaachana naye baadae akachukua akanywa mwenyewe
Wanasemaga Maji hufuata Mkondo

Jiandae kumdhibiti kwa mengi zaidi siku za usoni
 
Kipindi nipi darasa lapili niliwapiga watoto wenzangu(niliwaonea tabia yangu hio enzihizo kuonea wenzangu)

Basi baada yakuruhusiwa nikawapiga tena njiani

Wenzangu(tunaoenda njiamoja)wakashindwa kunisubiri wakatangulia

sasa njia yanyumbani unashuka kimlima nilio wapiga wanapita njia yajuu mimi wananiangalia kwabondeni.

Nilipofika bondeni kidogo wakaanza kunitukana hasira zikanipanda nikaanza kupanda kimlima kwakukimbia ili nikawapige vizuri tena

Aisee wakaanza kunirushia mawe sijakaasawa jiwe limetuwa utosini nilipiga mayowe balaa nikona Dunia inazunguka

Ghafla hata dakika haijaisha utosi ukatoka bonge lanundu sijielewi kabisa natembea huku nakule

Walewajinga wakakimbia wakaniacha nalia tuu nikiitawenzangu wanyumbani hawanisikii washafika mbali

Nikapiga mahesabu nikakumbuka mitakazaa kunababa mdogo anaishi huko ikabidi nikimbie kwenda kwake mana kichwa kinazidi kuvimba tuu kilanikigusa nundu imezidi nami nazidi kupiga mayowe wakunisaidia hakuna

Nilipofika kwa babamdogo hakutaka kunihoji sana nilipo mwambia tuu nimepigwa jiwe ndionikawa hivi chap akanichukua nakunipeleka hospitali napikipiki yake

Mamá namzee akawapigia simu wakaja kunichukua nishatibiwa tayali, ilesiku ndio niliona kifo live bila chenga

Wale wapuuzi niliwapelekesha sana hadi tunamaliza lasaba mana wangeniua
 
kweli tuliburuzwa ile akili inatukaa sawa tukaachia mikono kwenye lile chuma ndo ikawa pole yetu,tulichubuka mapaja,tumbo na kucha za vidole zilingooka.

Maisha ni mapito..
Utundu kazi duuuh uminishinda tabia Mimi nekua tototundu Ila we tototundu zaidi,
 
Pole sana Mkuu

Mimi nilikuwa mpole mno hadi Wazee walitamani nikawe Paroko nihubiri Injili tu

Mke mwenyewe walifanya kunitafutia tu miaka ile ya 73
wazee wanakupenda sana,hadi kukupa mke.

Sometimes bora kuwa mpole unaepuka maswahibu mengisa sana,maana mikono na miguu ilivunjika sana.

Yani nimewasumbua sana wazazi.
 
wazee wanakupenda sana,hadi kukupa mke.

Sometimes bora kuwa mpole unaepuka maswahibu mengisa sana,maana mikono na miguu ilivunjika sana.

Yani nimewasumbua sana wazazi.
Miaka ya zamani ilikuwa kawaida kutafutiwa Mke.

Mambo yalianza kubadirika miaka 1995 kuja Juu

Of course utundu ukizidi unaweza kukufanya hata uwe mlemamvu kama unatokea familia za kimaskini na ukavunjika mikono ama miguu wakati wa kucheza
 
Miaka ya zamani ilikuwa kawaida kutafutiwa Mke.

Mambo yalianza kubadirika miaka 1995 kuja Juu

Of course utundu ukizidi unaweza kukufanya hata uwe mlemamvu kama unatokea familia za kimaskini na ukavunjika mikono ama miguu wakati wa kucheza
Kupanda juu ya miti ya mzambarau tushadondoka sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom